Maraga asajili kesi ya dharula dhidi ya uchaguzi, Raila awa mpole ghafla...kunanii

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Raila amekua akiahidi moto na kwamba kutakua na maandamano hayajawahi kutokea kwenye historia ya nchi hii, hapo mnamo tarehe 26 mwezi huu. Amekua akitema cheche na kuweka Wakenya wote kwenye mkao wa mapambano.

- Jana Marekani wakamwonya kwamba asizue vurugu na aheshimu tume ya uchaguzi
- Ghafla leo Raila akageuza gia angani na kusema hajawahi agiza maandamo yoyote siku ya uchaguzi na kwamba wafuasi wake wabaki nyumbani huku wakiwa watulivu na kuzingatia amani (maneno ya ajabu ambayo nimeshangaa yanamtoka mdomoni)
- Ghafla jaji mkuu amesajili kesi ya dharula ya kusitisha uchaguzi wa kesho kutwa

Sasa kwa wadadisi wa masuala ya kisiasa, itakua Raila alipata fununu ya hatua hizi za Maraga? Au kuna nini nyuma ya pazia. Nchi hii bana, yetu macho ilmradi msiichome maana tumeijenga tofali kwa tofali, bati kwa bati.
 
Kama ulivyosema, muhimu wasije wakaichoma, ila vituko na vibweka kama hivyo vinaruhusiwa, ni kama kuweka chumvi kwenye mboga.
 
Lete udhibitisho wa hayo unayoyasema maana ninyi watu mmekuwa waongo hata kumzidi SHETANI!!!!!!!
 
Hamna uchaguzi Tar. 26!
 
Huu uchaguzi kwa maoni yangu ungeahirishwa ili mambo yanayolalamikiwa yaweze kurekebishwa
Mbna unataka tuende nje ya mipaka ya katiba? Katiba inasema uchaguzi ukitupiliwa mbali ufanyike ndani ya siku 60 sidhani walio na hoja ya uchaguzi kufutwa ni kwa maslahi ya nchi hii.........hata hivo sidhani supreme court inaeza airisha uchaguzi bila iebc wenyewe kuomba kuongezewa muda. Kuna issue ya iebc independence na tena kuna hii issue ya court kazi yake ni kutafsiri sheria ila haiezi tunga sheria...mahakama haiezi kukinzana na katiba
 
Kwa mfano hata kama taratibu na sheria za kuendesha uchaguzi kama zilivyotajwa ndani ya katiba hazijatimizwa ndani ya hizo siku 60 uchaguzi ni lazima ufanyike hivyo hivyo?, ungemsikiliza balozi wa Marekani jana alipokuwa anazungumza kwa niaba ya mabalozi wenzake wa nchi za magharibi alishauri kwamba wanaotaka uchaguzi usimamishwe waende mahakamani wakajenge hoja sio kufanya fujo.
Kama ulivyosema, muhimu wasije wakaichoma, ila vituko na vibweka kama hivyo vinaruhusiwa, ni kama kuweka chumvi kwenye mboga.
 
Commisioner wa Tume kasema kwa hali ya sasa kuna pande mbili ndani ya tume, uchaguzi hauwezi kua huru na haki, what do you think pal?
 


Maadamu D.Trump ni Raisi wa USA hakuna Vita itatokea Kenya wala Afrika, aliyekuwa anachochea na kuleta Vita Afrika ni Obama na Clinton, hawa ndiyo devils waliomuua Gadafi hata Vita ya Kenya 2007 ni Obama ndiyo aliyoleta!

Sasa hivi kuna Amani Duniani baada ya Obama kuondoka, Isis kwisha, Boko haramu kwisha, Kony Uganda kwisha hata Kongo na Burundi zimetulia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…