MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Raila amekua akiahidi moto na kwamba kutakua na maandamano hayajawahi kutokea kwenye historia ya nchi hii, hapo mnamo tarehe 26 mwezi huu. Amekua akitema cheche na kuweka Wakenya wote kwenye mkao wa mapambano.
- Jana Marekani wakamwonya kwamba asizue vurugu na aheshimu tume ya uchaguzi
- Ghafla leo Raila akageuza gia angani na kusema hajawahi agiza maandamo yoyote siku ya uchaguzi na kwamba wafuasi wake wabaki nyumbani huku wakiwa watulivu na kuzingatia amani (maneno ya ajabu ambayo nimeshangaa yanamtoka mdomoni)
- Ghafla jaji mkuu amesajili kesi ya dharula ya kusitisha uchaguzi wa kesho kutwa
Sasa kwa wadadisi wa masuala ya kisiasa, itakua Raila alipata fununu ya hatua hizi za Maraga? Au kuna nini nyuma ya pazia. Nchi hii bana, yetu macho ilmradi msiichome maana tumeijenga tofali kwa tofali, bati kwa bati.