Marais Bora wa muda wote wa Tanzania ni Nyerere halafu Kikwete

Marais Bora wa muda wote wa Tanzania ni Nyerere halafu Kikwete

Nyerere alikuwa kiongozi mzuri kwa wakati wake tunashukuru wa hilo, ila kibaya alichotufanyia ni kutuachia jumba mbovu ambalo kwa kweli limekuwa ni mzigo kwetu watanzania.

Tungeshukuru sana kama jumba hili angelifanyika overhaul wakati bado hajatoka madarakani sababu kila anayekuja anaogopa kuligusa lisije likamwangukia, Mzee Mwinyi, Mzee wa Lupaso, Mzee wa Msoga, Mwendazake na hata Mama yetu bado vilevile anaogopa kuligusa- kivuli chako mwalimu kinawatisha wakati sisi watanzania tunazidi kuumia. Mzee wa Msoga alijaribu jaribu kiasi kutaka kuliporomosha ili alijenge upya lakini akakwama akaachana nalo.

Sasa je jumba hili tutamsukumia nani alifumue na kutujengea jipya ? tutaumia mpaka lini?

Kwa ufupi hili jumba bovu lishatuchosha, Mwalimu ungeondoka nalo then ukatujengea jingine zuri tungeshukuru sana ili sisi watanzania uliotupenda tungeishi kwa amani na upendo kuliko hivi sasa ndani ya jumba hili tunawindana kama wanyama wa mwitu kisa tu madaraka, uuchawa nao umekomaa, vurugu mtindo mmoja....jumba halina milango na madirisha, kila mtu anatoka na kitu chake anaenda kuuza yaani ulinzi haupo.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Shida hata mnaotaja Nyerere Wengi hamku feel utawala wake....
Nyerere kulikuwa na magazeti ya serikali Tu na redio ya serikali..
Kila mnachoambiwa kiko edited Kwa lengo la kupamba serikali...hakuna TV wala internet....
Chochote anacho agiza Rais ni sheria hapo hapo...hata aliagiza uchapwe fimbo.... inasemekana kina Samuel Sitta aliwachapa fimbo walipogoma Udsm.....

Sisemi haya kupinga Kuwa alikuwa Rais Bora... natamani wanaosema Rais huyu Bora na Yule sio Bora wapime Kwa mizania sawa...Binafsi Mkapa nimekuja kumpa thamani zaidi baada ya kifo chake ...Kikwete thamani yake ilionekana baada ya kuondoka Ikulu.....sisemi yupi Rais Bora but hata Samia thamani yake itaongezeka akisha toka Ikulu naamini
Hawakumbuki madhila ya utekelezaji wa Operation ya Vijiji vya Ujamaa.
Hawakumbuki madhila ya mgambo kwenye utekelezaji wa msako wa watu wasiolipa kodi ya kichwa au utekelezaji wa Sheria ya Uzembe na uzururaji.
Kutopata ajira bila ya kwanza kujiunga na "Chama".
Kwa wale wasiojua maana ya "Chama" ni CCM kabla ya hapo ni TANU.
 
Nyerere alikataa uchawa Kama ilivyokuwa kwa Kikwete mambo ya kusifiwa sifiwa Hawa watu walikuwa hawataki kabisa!!
Ni hakika kwamba ulikuwa hujazaliwa enzi za Nyerere. Bendi za muziki zote zilikuwa zinamsifia yeye na misemo kama 'zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa Chama' ndiyo ilikuwa kibwagizo cha mikutano.

Uchawa upi tena uliutaka?
 
Shida hata mnaotaja Nyerere Wengi hamku feel utawala wake....
Nyerere kulikuwa na magazeti ya serikali Tu na redio ya serikali..
Kila mnachoambiwa kiko edited Kwa lengo la kupamba serikali...hakuna TV wala internet....
Chochote anacho agiza Rais ni sheria hapo hapo...hata aliagiza uchapwe fimbo.... inasemekana kina Samuel Sitta aliwachapa fimbo walipogoma Udsm.....

Sisemi haya kupinga Kuwa alikuwa Rais Bora... natamani wanaosema Rais huyu Bora na Yule sio Bora wapime Kwa mizania sawa...Binafsi Mkapa nimekuja kumpa thamani zaidi baada ya kifo chake ...Kikwete thamani yake ilionekana baada ya kuondoka Ikulu.....sisemi yupi Rais Bora but hata Samia thamani yake itaongezeka akisha toka Ikulu naamini
Nakubaliana nawe mzee mwenzangu, asilimia kubwa ya hawa vijana hawakuwepo enzi za utawala wa awamu ya kwanza.

Hata kujiunga na Chuo kikuu tu ilikuwa mpaka upate clearance ya mwenyekiti wako wa CCM wa mtaa (sikumbuki exact title yao enzi zile).
 
Ni hakika kwamba ulikuwa hujazaliwa enzi za Nyerere. Bendi za muziki zote zilikuwa zinamsifia yeye na misemo kama 'zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa Chama' ndiyo ilikuwa kibwagizo cha mikutano.

Uchawa upi tena uliutaka?
Ulichoandika kinasadifu jina lako.
Hawa kazi yao kutukuza watu kipopoma tu.
 
Nyerere alifanya alichoweza kwa kipindi chake,uchawa ulitokana na mfumo wa chama kimoja na siasa za kikomunisti na vita baridi. Kwa sera mifumo ya wakati huo ilikuwa sahihi. Je Baada ya kubadilisha uendeshaji na mifumo kikatiba,Tujiulize uchawa wa sasa unatokana na nini hasa?ni mwendelezo wa matokeo ya historia au hatujafanya mageuzi sawasawa,haya ni mazao ya mfumo zamani uliozaa za kusifiana , basi kama tunataka mabadiliko/mageuzi kweli kweli ni lazima kuwa na KATBA MPYA ili Kubadili mifumo,mindset na dhana zote kuongeza uwajibikaji.Kauli za unaupiga mwingi zitapungua zenyewe tu au kutoweka kabisa na zitatolewa kiukweli bila unafiki wa kutafuta fursa kwa mwelekeo wa jamii kifalme vinginevyo zitatolewa pale itakapokuwa muhimu sana kwa kuzingatia ukweli.
 
Kikwete ndiye raisi ninayempenda kwa namna anavyoishi maisha yake yeye na familia yake,huwa namfuatilia Sana!kikwete Ni Mastermind,game planer n.k

Raisi Bora kuwahi kutokea nchi hiii Ni JOHN POMBE MAGUFULI!
Miaka mingi Sana itapita kumpata raisi wa aina yake
 
Kikwete alikuwa Rais wetu bora sana..In my Opinion.
 
Mi nawaona NYERERE, MKAPA na mwingine angekuwa Magu ila ubabe ulipitiliza!.

Mi nawaona NYERERE, MKAPA na mwingine angekuwa Magu ila ubabe ulipitiliza!.
Nilimuulizaga mzee wangu mmoja juu ya Uongozi wa Hayati Magufli na Nyerere! Yule mzee alinijibu Nyerere alikuwa mkali sana sawa tu na Magufuli lakini shida ya Magufuli alikuwa mfatiliaji sana , akikuagiza kitu ujue atafatilia mpaka kifanyike kweli.
Kiukweli Nyerere na Magufuli hawa falsafa zao za kisiasa zinakaribiana sana labda kuliko marais wote ambao tuliokuwanao labda kama hamjasima vizuri mwalimu alikuwa mtu wa aina gani.

Sometime huwa najiuliza hawa wanamuita Magufuli katili, fashist sijui, ana roho mbaya na maneno lukuki! Wangekutana na Sokoene wangemuita majina gani?

Just imagine una Rais ni Magufuli, alafu una Waziri mkuu ni Sokoine! Unahisi nn kingetokea?
 
mikataba mibovu ya gas ya awamu yake ndio inatusumbua hadi leo hii!

Mstaafu. J.Kikwete hana baya kabisa kwa upande wangu, period. And of course, he’s the best President of all time(kwangu mimi).
Huu ni ukweli mchungu na ndiye rais aliyechafuliwa Sana Ili aonekane mbaya lakini nakwambia mpaka kesho hatutakuja kuwapata Marais Kama J.K Hawa wawili.
 
Back
Top Bottom