Marais Wastaafu wa Tanzania, wajengewa nyumba na Serikali

Nyumba za nini.kwani walikuwa wapangaji uswahilini? Wao tembo? ( in Nyerere' s voice)
 
Sheria zenyewe hizi zinapitishwa kimya kimya na wabunge wa ccm. Wazee wa ndiyoooo..
Chadema wakati wa mijadala kama hii huwa wanatoka Bungeni wacha tuendelee na wenye haja ya kubaki Bungeni. Je, unakumbuka wabunge waliopitisha hilo azimio na sheria kupita? Mimi sioni shida waliopita kabla ya JPM walishindwa kuitekeleza lakini sasa hivi tuna Chuma pale Ikulu ambacho kinasimamia nidhamu. Sisi ni tajiri na uwezo tunao tanzania kumenoga rudini nyumbani mlio nje.

 
Mwalimu amejengewa Butiama kabla ya kufariki
Hili swali linajirudia ilhali kuna mjuvi keshajibu; Mwl alijengewa na jeshi kabla hiyo sheria yenu ya 1999 kupitishwa.

Swali ni kwamba, Ben hakutii hii sheria, Jakaya Naye hakutii hii sheria, kwanini huyu afanye kwa haraka hivyo?

Himaya ya Ben na Jakaya zote hawakuwa nazo kabla ya kukalia kiti, ni matunda ya ajira yao ya miaka 10, wote wamejichotea vizuri tu kulingana na nafasi zao, na pengine ikifanyika tathmini ya hizo mali, maswali ya integrity zao kuwa mashakani yakaibuka.

80% ya mshahara wa raisi aliyemadarakani kuwa ndo pension ya kila mwezi ya mstaafu + watumishi n.k bado ni mzigo mkubwa sana kwa walipa kodi.

Kuna wakati maisha huanza na zero, kama vipi kama taifa tu turudi zero, taifa life kisha kwa pamoja tukae kwenye meza ya kuchorea chini ya usimamizi wa jeshi, tusuke upya mipango, tufute majina ya wezi wote kwenye ramani ya nchi halafu tuone kama hiki kizazi cha dotcom na chenyewe kitavurunda
 
Yan atajijengea mji kabisa


Sheria ni msumeno. Tanzania ni tajiri.
Nafahamu mnatamani kama Serikali ingewajengea pale Ufipa, khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Daah! Kweli hawa ndio wanakula keki ya taifa. Sisi wengine tunasikindiza tu
 
Hii sheria haiko sawa. Hii ni fedha ya mtanzania anayevuja jasho na kulipa kodi halafu yeye hafaidiki lakini wale wenye nacho ndio wanufaika. Hapana ifutwe haraka
 
Hii sheria haiko sawa. Hii ni fedha ya mtanzania anayevuja jasho na kulipa kodi halafu yeye hafaidiki lakini wale wenye nacho ndio wanufaika. Hapana ifutwe haraka
Kufutwa hadi akidi ya wabunge itimie
 
Daah! Kweli hawa ndio wanakula keki ya taifa. Sisi wengine tunasikindiza tu
kila usiyekubaliana au kakuzidi kihoja anakula keki ya taifa bure? Je, umepitia mimi nilikopita? Je, unafahamu nafanya nini? Wacha umbeya? Ukweli ni mchungu kama pilipili manga. Tanzania ni ya Watanzania wote wote tunapewa haki sawa kikatiba tuache wivu!
 
Hii sheria haiko sawa. Hii ni fedha ya mtanzania anayevuja jasho na kulipa kodi halafu yeye hafaidiki lakini wale wenye nacho ndio wanufaika. Hapana ifutwe haraka
Mkuu peleka hoja Bungeni ikabadilishwe, as it is right now, there is nothing you can do. JPM is implementing this law.
 
Aiseeh, mishahara minono isiyokatwa kodi malupu lupu ndo usiulize matibu bure zawadi ndo usiseme bado ajengewe jumba. Madaraka matamu aiseeh. Hata kumkosoa aliyepo madarakani pindi akoseapo watangulizi hawawezi.
Pepo inaanza duniani
 
Hawa wazee kitu gani wanachokosa?

Kule Kagera waliomba uwapunguzie bei ya simenti wajenge nyumba ukawakatalia kwa kebehi leo unakwenda kuwajengea nyumba nyingine watu wenye mijumba yao kedekede?

Mzee Mwinyi ana miaka 95 ina maana hakuwa na nyumba?
Kikwete hana nyumba?

Unawajengea hao watu mijumba wasiyohitaji tena ni mikubwa kweli wamekuwa tembo?

Kama hoja ni kuhusu stahiki zilizoko kisheria mbona hujatoa nyongeza za mishahara za wafanyakazi zilizoko kisheria kwa miaka mitano?
 
Safi sana tena sana, sasa turudi kwenye hiyo hiyo sheria, vp inasemaje juu ya nyongeza ya mishahara na kupandishwa madaraja kwa watumishi wa umma?
Mtumishi anatakiwa
1. Kupata annual increment kila mwaka
2. Kupanda daraja kila baada ya miaka 3
3. Kulipwa nauli ya likizo kila baada ya miaka 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…