Marais Wastaafu wa Tanzania, wajengewa nyumba na Serikali

Marais Wastaafu wa Tanzania, wajengewa nyumba na Serikali

Lissu atakuwa rais October hiihii hivyo atazuia ujenzi wa Hilo hekalu usiwe na wasiwasi.
Lissu hawezi kuwa Rais wa Watanzania. Chadema kajengeni ofisi kwanza. Ni aibu kubwa kwa chama kikuu cha upinzani, kinacho tafuta dola kukosa ofisi ili hali mnapata ruzuku zaidi ya 300mil kila mwezi.
 
Mtumishi anatakiwa
1. Kupata annual increment kila mwaka
2. Kupanda daraja kila baada ya miaka 3
3. Kulipwa nauli ya likizo kila baada ya miaka 2
Ambacho huyu mtawala wa sasa hajafanya kwa miaka 5. Halafu kuna watu wanampigia makofi kwa hii double standard anayoionyesha.

Uchaguzi huu pia utapima uwezo wetu sisi wananchi wa kuchambua pumba na mchele.
 
Halafu mtu atauliza kwanini tunataka katiba mpya!

Sisi wengine tumepata bahati ya kuishi kwenye vibanda vinavyofanana na nyumba tuwasemeeni wengine, watanzania walio wengi makazi yao yanasikitisha sana jamani, kwanini tusiwaone hao? Kwanini wasisaidiwe hao? Mbona nchi zingine serikali inadeal na kuboresha makazi ya watu!

Serikali ya nchi hii tunaomba iwajali wananchi wa kawaida ambao ni walipa kodi, si kila mtu ataweza kuwa Rais apewe hiyo mizawadi, lakini kila mtu ni mlipa kodi.
 
View attachment 1603958
Raisi mstaafu awamu ya pili akikabidhiwa nyumba aliyojengewa na serikali Masaki Dar Es Salaam
View attachment 1603960
Muheshimiwa Magufuli akikagua ujenzi wa nyumba ya raisi mstaafu awamu ya nne anayojengewa na serikali Kawe beach Dar Es Salaam
Ni haki yao kwa mujibu wa sheria ila kuwakabidhi hadharani inajenga chuki kati wa maskini wa nchi hii na watawala.

Wastaafu hupokea pension kimya kimya na hawa wapewe nyumba zao kimya kimya
 
Siku Ya Kufa Nyani Miti Yote Huteleza!!
Mtahangaika Sana Kuonyesha Yasiyotakiwa Mkitafuta Huruma. 😏😏😏😏😏
 
Hii ni ili wamtetee asipelekwe the Hague perfect timing.
 
Hii sheria ingekuwa kwa watumishi wote wa umma.
🤣🤣🤣🤣 kama huna nyumba,Acha kushinda Jf ukipiga soga, tafuta hela ujenge nyumba. Au kama vipi pambana na wewe uwe Rais basi, ingawa najua huwezi.
 
Ambacho huyu mtawala wa sasa hajafanya kwa miaka 5. Halafu kuna watu wanampigia makofi kwa hii double standard anayoionyesha.

Uchaguzi huu pia utapima uwezo wetu sisi wananchi wa kuchambua pumba na mchele.
Usiwe na shaka kabisa. Nina uhakika mkubwa kabisa uchaguzi wananchi wengi hawatampigia Magufuli kura. Atapata kura chache sana kupita marais wote. Ila sasa yeye mikakti yote ameishaitekeleza: atafanya hujuma. Ameshaandaa namna atakavyochakuchua na muda tu unasubiriwa. Labda itokee jambo moja: Wananchi wakinukishe. Najua watazima njia nyingi za mawasiliano hasa social media lakini bado tusiondoe uwezekano wa wananchi ku-react safari hii.
 
Maana yake nini
Hata Mimi sielewi! Yaani utumishi wa miaka kumi unajengewa nyumba, unapewa ulinzi, magari, pensheni na matibabu na kujengewa kasri la kifalme! Mbona Hawa wazee wengine waliolitumikia taifa kwa miaka 40+ wakistaafu hawajengewi na badala Yake wanazinguliwa kwa kutokulipwa
pensheni zao Hadi wengine wanafariki wakizihangaikia? Kwanini wasijengewe hata kajumba la vyumba vitatu wakajisitiri na kupewa pensheni zao on spoti Mara tu utumishi wao unapokoma wanakalishwa Hadi miaka mitano bila kulipwa?
Hili halijakaa sawa hata kidogo! Wastaafu waamke na kuukataa ccm oktoba kwa ubaguzi huu wa wazi!
 
🤣🤣🤣🤣 kama huna nyumba,Acha kushinda Jf ukipiga soga, tafuta hela ujenge nyumba. Au kama vipi pambana na wewe uwe Rais basi, ingawa najua huwezi.
Ama wewe ni tunda la ufisadi au mnufaika wa ufisadi ndio maana unaandika hivi ukidhani unamtetea huyo anayejikomba kwa wastaafu kumbe unawazidishia wapigakura hasira ili wakapige kura za hasira za kuukataa ccm!
Wao walilishwa, kuvalishwa, kutibiwa na kuwasomeshea watoto wao Bure kabisa! Na mishahara yao na viinua mgongo vyao na zawadi kubwa kubwa hawakuzigusa kabisa! Watafananaje na wafanyakazi wa kada Kama za ualimu wanaolipwa kiduchu? Halafu unawafokea wapigakura badala ya kuwabembeleza! Utayapata majibu yao oktoba 28!
 
ukitafakari ni kwa nini Nyerere aligoma kujengewa Nyumba na jeshi utajua kiundani alikuwa ni mtu wa aina gani !!..

Angekataa ile nyumba isingejengwa. Hayo mengine ni janjajanja tu za kidunia zisizo na manufaa.
 
Hao kipindi chao cha kukwapua si walishajenga mahekalu, acheni kutuletea sarakasi zisizo na mashiko, au ndo rushwa za uchaguzi hizi.
 
Back
Top Bottom