Marais Wastaafu wa Tanzania, wajengewa nyumba na Serikali

Marais Wastaafu wa Tanzania, wajengewa nyumba na Serikali

Huu ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Hawa marais wakiwa madarakani wanakuwa wameisha kukusanyia pesa za kutosha na kujijengea mahekalu mengi. Maana mwinyi na Kikwete wanamiliki vijiji vyao.
Hii nyumba aliyokabidhiwa mwinyi ina thamani ya zaidi ya shilingi bilion saba kwa makisio ya awali.
Sasa fikiria mzee wa miaka 95 anajengewa nyumba yenye thamani hiyo!
WAAFRICA HATUNA BAHATI YA KUPATA VIONGOZI!
 
Mimi sio kijana,na kwenye swala la kupambania uchumi wangu nilishatoka zamani sana.
Hakuna sehemu niliyoshangilia matumizi mabaya ya kodi zetu(ingawa sidhani hata kama unalipa kodi),nilichomshauri mwenzako ni kwamba atafute hela ajenge badala ya kusubiri serikali ianze kujengwa nyumba wastaafu wote Kama anavyoota,huku mkiwa busy kujibizana mitandaoni 24hrs.
Tatizo lenu vijana wa siku hizi mnapenda mteremko Sana,mnafikiri maisha ni kukaa na kutype maneno kwenye simu.Maisha Ni magumu kwelikweli kwa watoto wanaozaliwa kwenye familia duni,pambaneni na muache ujinga.

NB:Ushauri si lazima uuchukue, kama hauwapendezi mnaweza kuendelea kusubiri siku ambayo serikali itawajengea.
Unaona jinsi unavyoprove kuwa mnufaika wa ufisadi? Laiti ungetoka hizo familia maskini ulizojinasibu hutokani nazo ungewaelewa wanaopinga wanamaanisha Nini! Hongera kwa kuyapatia Maisha japo hujawashinda hao wastaafu wenye ukwasi wa kufuru lakini bado wanajengewa! Wanetu wacha wahangaike kusaka ajira ili nao wamiliki vijumba huko mabondeni nao wajaliwe na maji ya mafuriko Kama wakibahatika kujenga hivyo vibanda! Yana mwisho haya usijisahau Sana tajiri!
 
Wanasema sheria kwamba mtu yeyote aliyeshika nafasi ya uraisi wa JMT baada ya kustaafu anatakiwa kujengewa nyumba isiyopungua vyumba vinne ikiwa na kila kitu ndani.
Hii bajeti ya kujengea watu binafsi nyumba imetoka wapi?

Maana ni kodi za wananchi zimekatwa akajengewa mtu nyumba binafsi kama zawadi

Hawa watu walishastaafu wakapewa stahiki zao in full,then kuna mtu binafsi anachukua hela zetu anawapa nyumba hawa watu kama binafsi..

Justification ni ipi?

Hata kama,je wabunge wetu walipitisha kwa niaba yetu?Hapana

Serikali ni tatizo,yaani mtu anachukua hela zetu kwa his own will anagawia watu for free bila ruksa ya wenye mali

Justification ya hawa wastaafu ikitoka hapo,itakuja kwa mawaziri wakuu wastaafu,halafu then majaji wastaafu,mawaziri wastaafu,maspika wastaafu,etc....our money is gone!
 
ITV wamesema nyumba ya Mwinyi ujenzi ulianza 2005 kisha ukasimama. Sheria ilipita 1999
Sheria ilipitishwa lini na wapi? Mbona Mkapa na Kikwete hawakumjengea nyumba mstaafu yeyote yule?
 
Na mwinyi amestaafu 1995, nyumba anakabidhiwa leo !!!
Nikusaidie tuu, sheria ya mafao ya viongozi wa siasa wastaafu Namba 3 ya 1999, kifungu cha 9 kama ilivyo fanyiwa marekebisho 2005 imeelekeza marais wastaafu kujengewa nyumba. Sheria hii ilitungwa ikifuatia kujengewa nyumba Mwalimu Nyerere. Tafuta sheria hiyo usome. Hiyo nyumba ya Mwinyi imeanza ujengwa 2012. Hapo hakuna swala la retrospectivity katika sheria.
 
Unaona ndio ulofa wenyewe huo, kila usiyekubaliana au kakuzidi kihoja anakula keki ya taifa bure? Je, umepitia mimi nilikopita? Je, unafahamu nafanya nini? Wacha umbeya? Ukweli ni mchungu kama pilipili manga. Tanzania ni ya Watanzania wote wote tunapewa haki sawa kikatiba tuache wivu!
Basi sawa sisi wanyonge tuendelee kuimba tano tena Kwa magufuli. Maana tukihoji kidogo tunaonekana tuna wivu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Sheria ya kifisadi na ubadhirifu ifutwe hii. Unamjengeaje nyumba mtu ambaye ndani ya miaka mitano mshahara wake ni zaidi ya bilioni mbili bila kodi na gharama zake zote za kuishi zinalipwa na walipa kodi. Ujenzi ulisimama tangu 2005 na nyumba kumalizika 2020!? 😳😳😳
ITV wamesema nyumba ya Mwinyi ujenzi ulianza 2005 kisha ukasimama. Sheria ilipita 1999
 
Mtu fulani anatafuta justification ya yeye kujijengea hekalu.
Mmeanza 😀

Huku Zanzibar utaratibu huu upo tena sio mpaka ustaafu, yaani ukiwa rais tu basi utachagua ukajengewa wapi. Salmin yupo Mazizini, Amani Karume yupo mbweni kajificha, Balahau Sheni kajipeleka shamba kuchunga ng'ombe na mifugo mengine, huy mtalii wanaemlazimisha tayari kashajengewa kabisaaaa Kisakasaka nafikiri.

Huu utaratibu unatakiwa ukome, majitu yapo serikali, yanapokea mishahara minono, na kama haitoshi wana 10% kwenye miradi, wanadhulumu ardhi za watu halafu bado na Nyumba wajengewe?!!
 
Unaona jinsi unavyoprove kuwa mnufaika wa ufisadi? Laiti ungetoka hizo familia maskini ulizojinasibu hutokani nazo ungewaelewa wanaopinga wanamaanisha Nini! Hongera kwa kuyapatia Maisha japo hujawashinda hao wastaafu wenye ukwasi wa kufuru lakini bado wanajengewa! Wanetu wacha wahangaike kusaka ajira ili nao wamiliki vijumba huko mabondeni nao wajaliwe na maji ya mafuriko Kama wakibahatika kujenga hivyo vibanda! Yana mwisho haya usijisahau Sana tajiri!
We unafikri waliofanikiwa wote wametokea familia zenye uwezo? Ni swala la malezi tu,hao watoto wako ukiwaambukiza hii mindset yako,amini kwamba hawawezi kutoboa.
 
Hii issue ndio itaimaliza ccm.....
hapa sio mahali pake.....
wananchi hawa wamechoka balaa....
ujenzi wa nyumba ya raisi ni sheria package...
hv ccm hakuna reasonable think tank!?
 
Upuuzi mwinyi kastaafu miaka 25 imepita nyumba ndio akabidhiwe leo ilitakiwa iwe imediate,hapo mkapa atakuwa kaondoka bila kujengewa
 
Hizo nyumba zimepitishwa na bunge ama ni kama zawadi je hela za kujengea nyumba ni zao ama zetu,? Unajua haya Mambo bhana yanaudhi Sana ee
 
Ipo kisheria kama wengine wanavyopewa magari baada ya kustaafu
Hata annual salary increment (nyongeza ya mshahara ya Kila Mwaka) Kwa watumishi wa Umma ipo kisheria. Mbona Kwa wafanyakazi Sheria inapuuzwa na haitekelezwi??? Ubinafsi gani huu??

Hawa watu ndio waliotupora nyumba za Serikali na kuasisi maufisadi ya Kila Aina. Leo tena wanajengewa majumba wkt Haki za watumishi mnazikanyaga. Lissu ingia ufute Sheria za kipuuzi kama hizi.
 
...kweli ikulu ni pango la walanguzi,ndomana panagombaniwa..


Government is not a solution to our problems...government is a problem.
 
Angekataa ile nyumba isingejengwa. Hayo mengine ni janjajanja tu za kidunia zisizo na manufaa.

Fikiria kama Nyerere angekuwa na mindset unazozisema bhasi leo hii si familia yake ingekuwa kama royals wenye utajiri kibao !!!...

Jitoe ufahamu kadri ya unavyotaka maana ni haki yako kikatiba, sema madhaifu ya Nyerere ikibidi ila moja ya kitu kikubwa ambacho alikuwa nacho

"aliposema hii nchi ni ya watu maskini, aliimaanisha kivitendo kupitia maisha yake mwenyewe"
 
Ni sheria mkuu
Hata kama ni sheria ..hizi ni sheria kandamizi zinazo changia kuwakandamiza raia watanzania na kuwanufaisha viongozi watanzania ambao kitabia hawana tofauti na wakoloni ....imagine hao viongozi wote wana maisha mazuri but still wanaongezewa mali yaani wana limbikiziwa mali ilhali kuna wananchi watanzania maji wanayotumia kunywa na kupikia wanachota katika mabwawa ambayo yanatumika kuwanywesha maji mifugo
 
Back
Top Bottom