Marais Wastaafu wa Tanzania, wajengewa nyumba na Serikali

hivi huku mazense ninako ishi lini nitaondoka?
jibu ni TRA wakinipunguzia mzigo wa kodi labda na mimi nitajenga nyumba kule Kiluvya
 
Sawa mkuu, kama ushauri wangu kwako kwamba utafute hela ili ujenge hiyo nyumba unayoitaka badala ya kushinda Jf, umekuudhi na kujifanya unione kama mnufaika wa ufisadi,basi subiri huyo Rais atakaekuja kukujengea nyumba wewe kama mtumishi wa umma.

NB: Yani unategemea kuna Rais atakaekuja kukataa neema wanayoipata kutokana na nafasi hiyo? Nhiiiiiiiiiiiiii😃.
USIKU MWEMA
 
Naamini wewe ni kijana Tena mhangaikaji Sana unayepambana usimame kiuchumi! Kama ndivyo, unawezaje kumshangilia ujinga huu wa kuwaongezea hao wastaafu zawadi za makasri huku ukiukandamiza upande mwingine wa wastaafu ambao nawe umenufaika na huduma zao? Huoni kuwa huu ni ubaguzi wa makusudi? Na kwanini wajengewe ilihali walijijengea ikulu ndogo vijijini mwao? Usitetee matumizi mabaya ya Kodi zako vinginevyo wanao watakuja kukucheka na kuudharau kimoyomoyo!
 
Hata Mungu alishasema aliyenacho anaongezewa. Jitahidi uwe nacho then Mungu atakuongezea!
 
wakati shule ya msingi mingoyo wanahaha kupata angalau mashimo matatu ya chookwa ajiliya wanafunzi 200 tu.
 
Dah kweli watanzania sisi aliyeturoga sijui ni nani aisee nimepitia coment nyingi hapa na sehemu mbalimbali kuhusu hili jambo la wastaafu marais kujengewa nyumba nimesikitika sana na nimegundua mambo kadhaa,
Kikubwa nilichogundua watanzania wengi tumejawa na wivu mbaya mno uliojengwa na umasikini wa familia zetu yaani tunaona mtu aliyefikia ngazi ya urais tunamchukulia poa tu hatumpi uthamaani kiasi hiki fikiria kama ndo wewe ni rais halafu usitendewe kama hiki wanachofanyiwa wastaafu wetu ? Shame on us. Kabisa
 
Very Interesting...
 
Huu ni wizi wa pesa zetu walipa kodi. Mbona Mkapa hamkujengea nyumba Mwinyi na Kikwete hamkujengea nyumba Mkapa? Huu ni wizi na ubadhirifu mkubwa wa pesa za umma.
 
Mimi sio kijana,na kwenye swala la kupambania uchumi wangu nilishatoka zamani sana.
Hakuna sehemu niliyoshangilia matumizi mabaya ya kodi zetu(ingawa sidhani hata kama unalipa kodi),nilichomshauri mwenzako ni kwamba atafute hela ajenge badala ya kusubiri serikali ianze kujengwa nyumba wastaafu wote Kama anavyoota,huku mkiwa busy kujibizana mitandaoni 24hrs.
Tatizo lenu vijana wa siku hizi mnapenda mteremko Sana,mnafikiri maisha ni kukaa na kutype maneno kwenye simu.Maisha Ni magumu kwelikweli kwa watoto wanaozaliwa kwenye familia duni,pambaneni na muache ujinga.

NB:Ushauri si lazima uuchukue, kama hauwapendezi mnaweza kuendelea kusubiri siku ambayo serikali itawajengea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…