WAAFRICA HATUNA BAHATI YA KUPATA VIONGOZI!Huu ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Hawa marais wakiwa madarakani wanakuwa wameisha kukusanyia pesa za kutosha na kujijengea mahekalu mengi. Maana mwinyi na Kikwete wanamiliki vijiji vyao.
Hii nyumba aliyokabidhiwa mwinyi ina thamani ya zaidi ya shilingi bilion saba kwa makisio ya awali.
Sasa fikiria mzee wa miaka 95 anajengewa nyumba yenye thamani hiyo!
Unaona jinsi unavyoprove kuwa mnufaika wa ufisadi? Laiti ungetoka hizo familia maskini ulizojinasibu hutokani nazo ungewaelewa wanaopinga wanamaanisha Nini! Hongera kwa kuyapatia Maisha japo hujawashinda hao wastaafu wenye ukwasi wa kufuru lakini bado wanajengewa! Wanetu wacha wahangaike kusaka ajira ili nao wamiliki vijumba huko mabondeni nao wajaliwe na maji ya mafuriko Kama wakibahatika kujenga hivyo vibanda! Yana mwisho haya usijisahau Sana tajiri!Mimi sio kijana,na kwenye swala la kupambania uchumi wangu nilishatoka zamani sana.
Hakuna sehemu niliyoshangilia matumizi mabaya ya kodi zetu(ingawa sidhani hata kama unalipa kodi),nilichomshauri mwenzako ni kwamba atafute hela ajenge badala ya kusubiri serikali ianze kujengwa nyumba wastaafu wote Kama anavyoota,huku mkiwa busy kujibizana mitandaoni 24hrs.
Tatizo lenu vijana wa siku hizi mnapenda mteremko Sana,mnafikiri maisha ni kukaa na kutype maneno kwenye simu.Maisha Ni magumu kwelikweli kwa watoto wanaozaliwa kwenye familia duni,pambaneni na muache ujinga.
NB:Ushauri si lazima uuchukue, kama hauwapendezi mnaweza kuendelea kusubiri siku ambayo serikali itawajengea.
Hii bajeti ya kujengea watu binafsi nyumba imetoka wapi?
Maana ni kodi za wananchi zimekatwa akajengewa mtu nyumba binafsi kama zawadi
Hawa watu walishastaafu wakapewa stahiki zao in full,then kuna mtu binafsi anachukua hela zetu anawapa nyumba hawa watu kama binafsi..
Justification ni ipi?
Hata kama,je wabunge wetu walipitisha kwa niaba yetu?Hapana
Serikali ni tatizo,yaani mtu anachukua hela zetu kwa his own will anagawia watu for free bila ruksa ya wenye mali
Justification ya hawa wastaafu ikitoka hapo,itakuja kwa mawaziri wakuu wastaafu,halafu then majaji wastaafu,mawaziri wastaafu,maspika wastaafu,etc....our money is gone!
Sheria ilipitishwa lini na wapi? Mbona Mkapa na Kikwete hawakumjengea nyumba mstaafu yeyote yule?
Nikusaidie tuu, sheria ya mafao ya viongozi wa siasa wastaafu Namba 3 ya 1999, kifungu cha 9 kama ilivyo fanyiwa marekebisho 2005 imeelekeza marais wastaafu kujengewa nyumba. Sheria hii ilitungwa ikifuatia kujengewa nyumba Mwalimu Nyerere. Tafuta sheria hiyo usome. Hiyo nyumba ya Mwinyi imeanza ujengwa 2012. Hapo hakuna swala la retrospectivity katika sheria.Na mwinyi amestaafu 1995, nyumba anakabidhiwa leo !!!
Basi sawa sisi wanyonge tuendelee kuimba tano tena Kwa magufuli. Maana tukihoji kidogo tunaonekana tuna wivuUnaona ndio ulofa wenyewe huo, kila usiyekubaliana au kakuzidi kihoja anakula keki ya taifa bure? Je, umepitia mimi nilikopita? Je, unafahamu nafanya nini? Wacha umbeya? Ukweli ni mchungu kama pilipili manga. Tanzania ni ya Watanzania wote wote tunapewa haki sawa kikatiba tuache wivu!
ITV wamesema nyumba ya Mwinyi ujenzi ulianza 2005 kisha ukasimama. Sheria ilipita 1999
Mmeanza 😀Mtu fulani anatafuta justification ya yeye kujijengea hekalu.
Mkapa alimjengea Nyerere Butiama bro.Sheria ilipitishwa lini na wapi? Mbona Mkapa na Kikwete hawakumjengea nyumba mstaafu yeyote yule?
We unafikri waliofanikiwa wote wametokea familia zenye uwezo? Ni swala la malezi tu,hao watoto wako ukiwaambukiza hii mindset yako,amini kwamba hawawezi kutoboa.Unaona jinsi unavyoprove kuwa mnufaika wa ufisadi? Laiti ungetoka hizo familia maskini ulizojinasibu hutokani nazo ungewaelewa wanaopinga wanamaanisha Nini! Hongera kwa kuyapatia Maisha japo hujawashinda hao wastaafu wenye ukwasi wa kufuru lakini bado wanajengewa! Wanetu wacha wahangaike kusaka ajira ili nao wamiliki vijumba huko mabondeni nao wajaliwe na maji ya mafuriko Kama wakibahatika kujenga hivyo vibanda! Yana mwisho haya usijisahau Sana tajiri!
Kwani jk hajajengewa na serikali kabla ya kuindoka madarakani?Butiama ilishajengwa kitambo sana
Hata annual salary increment (nyongeza ya mshahara ya Kila Mwaka) Kwa watumishi wa Umma ipo kisheria. Mbona Kwa wafanyakazi Sheria inapuuzwa na haitekelezwi??? Ubinafsi gani huu??Ipo kisheria kama wengine wanavyopewa magari baada ya kustaafu
Hapana kuna ubinafsi kwenye hili. Mbona watumishi hawajaongezewa mshahara wkt nyongeza ipo kisheria?? Au Sheria inaheshimiwa Kwenye kuwapa maslah wakubwa tuu??Hapo imekaa vyema
Angekataa ile nyumba isingejengwa. Hayo mengine ni janjajanja tu za kidunia zisizo na manufaa.
Hata kama ni sheria ..hizi ni sheria kandamizi zinazo changia kuwakandamiza raia watanzania na kuwanufaisha viongozi watanzania ambao kitabia hawana tofauti na wakoloni ....imagine hao viongozi wote wana maisha mazuri but still wanaongezewa mali yaani wana limbikiziwa mali ilhali kuna wananchi watanzania maji wanayotumia kunywa na kupikia wanachota katika mabwawa ambayo yanatumika kuwanywesha maji mifugoNi sheria mkuu