Marangu Coach imefikia hatua hii

Marangu Coach imefikia hatua hii

Jana Jumatano 04/10/2023 basi la Marangu Coach liliondoka Dar es Salaam asubuhi kama kawaida na abiria wakiwa na matarajio ya kufika Moshi kwenye saa 10 hivi bila kujua lililo mbele yao, basi lilipofika wilaya ya Bagamoyo likaharibika ikabidi spea iagizwe toka Moshi iletwe Bagamoyo! Akili mbovu.

Spea haikuletwa kwa ndege wala ungo, Moshi siyo Dar masaa yalipita Mungu Mkuu ikafikishwa na basi likatengenezwa na kuendelea na safari, likaingia mkoa wa Tanga likaharibika tena na likatengenezwa na kuendelea na safari, mpaka saa nne usiku basi lilikuwa wilaya ya Same! Usingizi ukanipata nikazimika na sijui Moshi liliingia saa ngapi ila lilifika salama, hiyo ndiyo Marangu Coach.
Marangu Coach Tajiri wake na mke wake COVID-19 ilifanya mambo yake.
 
Tuliposema mabasi ya kichina ni hovyo tulishambuliwa tukaambiwa hatuendi na wakati, huo upuuzi hutausikia Kilimanjaro Express, wale gari zao nyingi kama siyo zote ni toughened and trusted Scania.
Acha uongo wewe.una chuki zako binafsi.Mbona hizo scania leo sio nyingi barabarani kama haziharibiki.Hakuna gari ambalo halipati itilafu.Tuache kuongea kauli kwasababu ya mawazo yetu binafsi yasiyo sawa.
 
Tuliposema mabasi ya kichina ni hovyo tulishambuliwa tukaambiwa hatuendi na wakati, huo upuuzi hutausikia Kilimanjaro Express, wale gari zao nyingi kama siyo zote ni toughened and trusted Scania.
Labda walikosa bus la akiba
 
Namba A ya scania inafanya poa kuliko mchina wa namba E. Kama nasema uongo nionyeshe mchina wa namba A.

Wanaoendesha ni watoto. Ni yule wa kiume. F*uck covid. Imewakatili sana hii familia aisee. Nilipita kijijini kwao Lekura Mamba last week kumepoa kweli jamani. Mwenye mali ni mwenye mali tu.
Kwahiyo watu waache kupanda gari zuri lenye kiyoyozi wakaangaike na ngarangara la scania namba A kisa linatembea vizuri.hii sio dunia yakuangaika na matumizi ya nguvu bila akili.Hizo tetenus panda mwenyewe.Mchina kaleta mapinduzi makubwa kwenye usafiri nyie bakini uko uko kwenye maugumu yenu.
 
Kuna siku nlikua natoka arusha to dom na shabiby, basi likapata tatzo kabla hata ya kufika makuyuni, spea ilitoka dodoma tulingoja zaidi ya 5 hrs. Nadhan wanakuwa na spea zao pia ndio maana ya kusubiria badala ya kununua karibu na eneo ilipotokea changamoto.
Wangekuwa wananua jirani kisha wanareplace
 
Abiria na nyie sauti zenu hamkupaza vizuri....kuna Siku nilipanda basi kwa dharura hapo magufuli stendi ...hata bagamoyo halikufika likaharibika.Abiria tukawa wakali kama mbogo ikabidi mwenye bus aite bus chap magufuli stand la kampuni nyingine akatufaulisha..
 
Tuliposema mabasi ya kichina ni hovyo tulishambuliwa tukaambiwa hatuendi na wakati, huo upuuzi hutausikia Kilimanjaro Express, wale gari zao nyingi kama siyo zote ni toughened and trusted Scania.

Kwa hiyo unamaanisha enzi barabara zimetawaliwa na basi za Scania, hakukuwa na mabasi yaliyoharibika yakiwa njiani?
 
Marangu Coach Tajiri wake na mke wake COVID-19 ilifanya mambo yake.
Ninalijua hilo ila bahati mbaya kama ilivyo desturi yetu huwa hatuwahusishi wake na watoto wetu kwenye biashara zetu tangu wakiwa wadogo ili wakue nazo kama wafanyavyo wahindi na waarabu, hata angebaki mama na watoto bado ni shida tu.
 
Arusha Dar pana Abood, Bm, Ester, Extra na Bus zingine nyingi tu zipo sawa na wanajali mno abiria..
Unajua kuwa enzi za BM Dodoma / Dar tuu ilivuma lakini nayo ikakata pumzi, hii ya sasa imefufuka, hebu tuone kadri siku zinavyokwenda.
 
Unajua kuwa enzi za BM Dodoma / Dar tuu ilivuma lakini nayo ikakata pumzi, hii ya sasa imefufuka, hebu tuone kadri siku zinavyokwenda.
OK sawa BM safari za Arusha/Dar inafanya vizuri sana office zao wote hao wapo karibu na office za Kilimanjaro ina miaka karibu mitatu naona wapo vizuri tuu sio kuwa wanavuma ila wahudumu wao pale office wale wadada Customer care ni zero...
 
Back
Top Bottom