Marco Chali: Wimbo wa 'Freedom' sio wa Mr. Blue

Marco Chali: Wimbo wa 'Freedom' sio wa Mr. Blue

Hapa pananipa shida kidogo
Me nadhani daxo angeendelea kumdai blue hela yake ya wimbo lkn sio kusema eti wimbo bado ni wake wakati hata ukienda mkito unaambiwa FREEDOM-BLUE FT SUGU

Wimbo wa Blue tena aliimba na sugu baada ya kuombwa sana na sugu mwenyewe sijui kwanini watu wanaleta ushabiki wa kijinga
 
mwenye hiyo nyimbo aiweke hapa

Nyimbo hii hapa Blue ft sugu iangalie imewekwa toka 2015 youtube... leo inaimbwa tena na sugu kwa biti ile ile na chorus ile ile then nyimbo inakua ya sugu na watu wanashangilia!

2016 sugu anafuta sauti ya bluu na kuingiza yake na kujimilikisha nyimbo halafu wanawake zake wanashangilia
 
katika hili Sugu hajaonyesha UKongwe kabisaa. Yaani aliitwa akapewa Collable then kaamua kuufanya wake that is too low for him. By the way hajautendea haki wimbo wa Freedom ukilingnisha na original version, kiwango chake kipo chini kwasasa. Ni bora aka concentrate na mambo yake ya siasa huku akiendelea kutafakari juu ya Faiza Ally na drama za kumvua nguo hadharani.
 
"Kwahiyo jamaa [Blue] akawa ameipenda tukampa
akasema atamshirikisha Mr Two"

Hapa Marco chali kajimaliza mwenyewe mmempa wimbo alafu leo mnasema sio wa kwake. Tunajua mmemgeuka sababu ya pesa ila Sugu ni mwizi na atabaki kuwa hivyo alafu anajifanya mtetezi wa haki za wasanii.
Huyo chali mwenyewe anasema hapo kuwa Blue hajatoa pesa yoyote...sasa ndio maana sasa anamkana? kwa hiyo Blue angekuwa ametoa pesa ndio angeitwa kuambiwa arudishe pesa ?
 
Tatizo la blue ni kosa alilolifanya miaka mingi iliyopita kosa lenyewe ni KUACHA SHULE.....

na hili ni janga kwa wasanii wetu wengi...

shule shule shule...
elimu elimu elimu....

mwenzake sugu hata kama shule hajapita ni kuwa yuko karibu na kina tundu lissu, marando angalau sheria anazijua jua... na kukaa kaa bungeni nako kunasaidia

sasa mwenzangu na mie huyu anashinda na nyandu tozi na bob micharazo kuna anayejua sheria hapo??

b-o-b-micharazo.jpg

Jamaniiii umenchekesha mpaka nimepaliwa na kiranga uwiii
eti anashinda na nyandu tozi..maana nimewapatia picha wakiwa kijiweni wamekalia yale matairi chakavu ya magari huku wanashushiana mistari wenyewe halafa wanatoa kionjo kwa sauti "MICHARAZO BABY" hahahahhaha
 
Huyo waziri kivuli wa habari, utamaduni, michezo na sanaa kaiba nyimbo ya dogo na huyo Marco Chali aache kutetea ujinga wa Mheshimiwa.
 
katika hili Sugu hajaonyesha UKongwe kabisaa. Yaani aliitwa akapewa Collable then kaamua kuufanya wake that is too low for him. By the way hajautendea haki wimbo wa Freedom ukilingnisha na original version, kiwango chake kipo chini kwasasa. Ni bora aka concentrate na mambo yake ya siasa huku akiendelea kutafakari juu ya Faiza Ally na drama za kumvua nguo hadharani.
We jamaa akili zako nashindwa kuzitofautisha na akili za mende aliyekunywa sumu umeshaambiwa beat ni mali ya Marco na sugu ndiye aliyepewa hyo beat sugu akamchangua blue, blue akaja kuingiza mashairi yake kwenye huo wimbo blue akaja kupitia mlango wa nyuma akaenda kuachia mkito wakati anautoa Marco na sugu hawakuwa na taarifa, Sugu ndipo akarudi kuogea na Chali kumuomba atoe vition nyingine ndiyo maana kwenye video Marco alionekana mwenye wimbo
 
Huyo waziri kivuli wa habari, utamaduni, michezo na sanaa kaiba nyimbo ya dogo na huyo Marco Chali aache kutetea ujinga wa Mheshimiwa.
Kama wimbo ni wa blue mwambie atupe risiti za malipo!
 
Kibongobongo, hiyo ngoma ni ya Mr. Blue manake kigezo cha kutolipa wala huwa hakitumiki kv majority ya wasanii wakubwa huwa hawalipi studio... walipaji wakubwa ni underground!! But in addition, umiliki wa kazi za kisanaa hautambuliwi kwa risiti za malipo!

So long as Mr. Blue alifanya ngoma na kumshirikisha Mr. II na ngoma ikasambazwa hadi kwa kutumia Mr. Blue ft Mr. II; there's no way leo unaweza kusema ngoma co ya Blue kv tu hakulipia beat!!! Ile kusajiriwa Mkito kama ngoma ya Mr. Blue, inatosha kabisa kuhalalisha umiliki kwa Blue unless iwe imesajariwa kwa jina lingine!

Hoja ya msingi hapa ni nani anasema kweli kati ya Blue na Marco Chali! Je, ni kweli Mr. II aliwasiliana na Blue kuhusu kuirudia Freedom? Au Marco alijipa jukumu la kuwasiliana na Blue lakini hakufanya hivyo?!

Hata P Funk alishawahi kutoa beat ya ngoma ya Prof. J kwa Chameleon bila kumshirikisha Prof. J!! Producers wanafanya sana hii!

Kwamba Mr. Blue kiki I don't think lakini nahisi Marco Chali au mdogo wake wanadanganya!
 
Kama wimbo ni wa blue mwambie atupe risiti za malipo!
Wasanii wangapi wamekuonyesha risiti za malipo za nyimbo wanazosema za kwao...? Mwizi ni mwizi tu na huyu Sugu ni ndumilakuwili kweli na Marco Chali njaa inamsumbua tu "Pesa ndio ilimaliza ugomvi wa Ruge na Sugu-R.O.M.A" baada ya kuwageuka vinega wenzake. tulitegenea awatetee wasanii wenzake kama waziri kivuli lakini badala yake yeye ndo anawaibia wasanii wenzake.
 
Kati ya watu wote Sugu hakupaswa kushiriki huu uhuni na Producers...hivi leo hii kama angekuwa Waziri wa Sanaa na Wasanii tungetegemea nini kutoka kwake?
 
SUGU amekwiba wimbo wa dogo hili ndilo naloweza kusema na hao akina Marco Chali Maelezo yao hayaelewiki so far ndo maana mtuhumiwa unamuona yupo kimya akifikir utetezi wa wezi wenzake akina Marco Chali umeeleweka. Hii ni aibu kwa wakongwe kama Prof Jay, A.Y, Jay Moe na wengine na sina hakika kama Master J na Prof Jay wangekuwa wanajua kuwa wanashiriki kwenye video ya mwizi wa "wimbo" SUGU wangekubali kuonekana kwenye ile video.
SUGU a.k.a Mr 2 ajitokeze tu hadharani na amuombe msamaha dogo kwa kitendo alichokifanya kuonyesha ukomavu wake kwenye tasnia ya muziki.
 
Jamaniiii umenchekesha mpaka nimepaliwa na kiranga uwiii
eti anashinda na nyandu tozi..maana nimewapatia picha wakiwa kijiweni wamekalia yale matairi chakavu ya magari huku wanashushiana mistari wenyewe halafa wanatoa kionjo kwa sauti "MICHARAZO BABY" hahahahhaha

watoto wa kinondoni hao hahaha

Blue mnyamwezi wangu nakukubali sana. Potezea hii mambo mtu mzima. Najua utagonga ngoma zingine kali "huu mwakaa". Potezea mtu mzima.
 
"Kwahiyo jamaa [Blue] akawa ameipenda tukampa
akasema atamshirikisha Mr Two"

Hapa Marco chali kajimaliza mwenyewe mmempa wimbo alafu leo mnasema sio wa kwake. Tunajua mmemgeuka sababu ya pesa ila Sugu ni mwizi na atabaki kuwa hivyo alafu anajifanya mtetezi wa haki za wasanii.

Kweli hata zile albamu 16 za Sugu alizoimba aliiba nyimbo!! Na zote hamna iliokuwa in a nyimbo chini ya tisa kweli Sugu mwizi
 
Back
Top Bottom