Jamani mbona Kuna umaskini sana vijijini pamoja na kuwepo ardhi Vijana wengi wanakimbia vijijini kwenda miji mingine kutafuta maishaArdhi ya uchagan ni dhahabu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamani mbona Kuna umaskini sana vijijini pamoja na kuwepo ardhi Vijana wengi wanakimbia vijijini kwenda miji mingine kutafuta maishaArdhi ya uchagan ni dhahabu
Wayahudi na wapalestina wanauana huko... Kwa taarifa yako hamna kitu kinaleta ugomvi kama ardhi. Sentimita 20 tu inaweza kukutoa roho.Mali ya Baba inanitoa roho,....Bora nikae peembeni, niinusuru roho yangu mimi, niinusustu Babaa...oiho yangu mimi......Harunaaaa
Mtu amepumzika kaburini, watoto wanataka kuuana kama vile wao wataishi milele
Inasikitisha sana. Huyu mwanamama ni Mwanasheria lakini anashindwa kujua vitu vidogo vidogo vinavyohusu soko la ardhiWizara ya Ardhi haina ardhi inayouza
Ni kujiendekeza na kukosa exposure tuWayahudi na wapalestina wanauana huko... Kwa taarifa yako hamna kitu kinaleta ugomvi kama ardhi. Sentimita 20 tu inaweza kukutoa roho.
Wana utajiri wa fedha ila wana umasikini wa akiliHawa ni ndugu tena nawajua nini kushindwa kuelewana ? au mmekumbuka kuwa dada yenu alizkwa na dhahabu zake?
Hizi ndizo laana za ukoo, wataacha ukoo unaandamwa na kesi milele.
Elezea. Unafahamu potentiality ya ardhi inapimwaje?Ardhi ya uchagan ni dhahabu
Kwakuwa kwenu mli kataa shule na m'meamua kuwa ma shamba boy kwa watu, huwezi elewa utajiri uliopindukia[ukwasi].Utajiri uliopindukia ni utajiri wa aina gani. Wachaga kwa sifa za kijinga?
Watanzania wenye asili ya hapa kwetu wapo wanne tuUtajiri uliopindukia ni utajiri wa aina gani. Wachaga kwa sifa za kijinga?
Boma sio MoshiPale Boma kuna viwanja vya laki 9-mili 2.
Hapo Njia Panda vipo vya 2.5 pia.
Lakini bado siyo sehemu potential.
Moshi inapitwa hadi na Kisemvule na Vikindu kwa thamani
Kwa nini Mahakama Kuu isingemaliza hiyo kesi ya mipaka na badala yake imeaamuru kesi ianze tena upya baraza la Aridhi!? Hii kesi haishi leo wala kesho, mtakuja niambia siku moja!!kuna watu wengine wakitaka kudhulumu mali wanakimbilia kuzika mtu, anachodai Frank Mareale ni sahihi , baraza la ardhi litambue mipaka na si kutoa maamuzi kwa hisia
Ni Arusha?Boma sio Moshi
Ni wilaya ya Hai hukoNi Arusha?
Na Maili Sita ni wapi?Ni wilaya ya Hai huko
Ardhi tumeikuta tutaiacha ya nini kumsumbua marehemu kwa kipande cha futi 6x6 tu katika eneo la ekari mbili!
Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro,imeliamuru baraza la Ardhi wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro,kurejea upya mgogoro wa Ardhi wa familia maarufu ya chifu Marealle kwa kutembelea eneo linalobishaniwa na wanandugu hao na kurekodi upya mipaka na kisha kutoa maamuzi chini ya mwenyekiti mwingine wa baraza hilo
Jaji kuu,Lilian Mongella katika kesi namba 51/2023 ya mrufani Frank Mareale dhidi ya Ackley Mareale ambao wote ni wanandugu, Jaji Mongella alisema mahakama imepitia ushahidi na maamuzi ya Baraza la Nyumba na Makazi la Mji wa Moshi chini ya Uenyekiti wa Reginald Mtei yaliyotolewa mei 5 mwaka huu na kusema kuwa maamuzi hayo yalikuwa na kasoro za kisheria.
"Nimeamua kesi hii ya wanafamilia wa Mareale isikilizwe upya kwa sababu Baraza la Ardhi lilikosea kisheria kwa kushindwa kuonyesha mipaka ya ekari mbili inayogombaniwa"
Katika kesi ya awali iliyofunguliwa na Frank Mareale katika Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi katika Mji wa Moshi, alikuwa na madai matatu moja wapo ni ombi la Baraza hilo litamke kuwa eneo la ekari mbili yeye ni mmiliki halali, Pili Baraza litoe amri ya kufukuliwa kwa mwili wa mama yake mdogo marehemu Veronica Mareale aliyeishi katika eneo hilo miaka 80 na kufariki mwaka 2020 na pia alitaka alipwe gharama za kesi.
Akizungumza nje ya Mahakama,Wakili wa Ackley Mareale,Julius Semali alisema kuwa hana pingamizi na uamuzi wa Mahakama kwani ana uhakika kuwa mteja wake ni mmiliki halali wa eneo hilo kwa kuwa mama yake alipata kihalali na alizikwa katika eneo lake.
Naye Wakili wa frank Mareale,Modest Njau aliishukuru Mahakama Kuu kwa uamuzi wake wa kuiagiza Baraza la Ardhi Nyumba na MakaziMoshi kusikiliza upya kesi hiyo na aliamuru Mwenyekiti wa Baraza na wajumbe wake wabadilishwe.
Njau alidai Mahakama Kuu iliona jinsi haki ilivyokuwa ikitaka kuchezewa katika usikilizwaji wa awali nayeye na mteja wake wameridhika na maamuzi hayo
Mei 5 mwaka huu chini ya mwenyekiti wa Baraza hilo la Ardhi Nyumba na Makazi ,Reginald Mtei lilitupilia mbali madai hayo ya Frank Mareale na kusema kuwa Ackley Mareale ni mmiliki halali wa eneo hilo na sio vinginevyo.
Hiki kizazi msichopita mafunzo ya JKT likitokea la kutokea mnaweza kuacha wake zenu kwenye baridi na kutetea mipaka kweli?Ardhi tumeikuta tutaiacha ya nini kumsumbua marehemu kwa kipande cha futi 6x6 tu katika eneo la ekari mbili!
Ni Hai... Hai na Moshi ni vitu viwili tofautiNi Arusha?
Hayo maeneo mengi yanapatikana bure bure Kama enzi hizoo,Huwa ninawashangaa hawa ndugu zangu ni kipi haswa kinawafanya kuzozania vipande vidogo vya ardhi ya Kilimanjaro wakati nchi yetu ina maeneo mengi yasiyotumika.
Kilimanjaro pamejaa na ni eneo lenye population pressure kwa sasa.
Uliyepita JKT umejitoa kiasi gani kutetea ardhi waliyopewa waarabu Loliondo, Ngorongoro nkHiki kizazi msichopita mafunzo ya JKT likitokea la kutokea mnaweza kuacha wake zenu kwenye baridi na kutetea mipaka kweli?
Nina wasiwasi sana na sera za CCM kutowapeleka JKT au kama hakuna namna basi mpelekwe GAZA na UKRAINE mkapate kujua namna ya kutetea ardhi.