Marealle afungua kesi kutaka bibi yake afukuliwe mahala alipoishi miaka 80

Marealle afungua kesi kutaka bibi yake afukuliwe mahala alipoishi miaka 80

Population pressure ya kilimanjaro unapima kwa vigezo gani?
Unafahamu half of the region wala hakuna aliyehamia?
Unajua kwamba mkoa unapoona kumejaa ni kwa wachaga wa Marangu?
Kuanzia Njia panda ya himo mpaka -Mwanga-Same- Hedaru na Mazinde kule umeona watu ?

Toka Same mpaka Hedaru unaendesha gari kilometa 40 bila kukuta nyumba wala kamji, wewe upo nyuma ya keyboard unaamini kilimanjaro imejaa?
Gusa uone kama hakuna mwenyewe
 
Hawa ni ndugu tena nawajua nini kushindwa kuelewana ? au mmekumbuka kuwa dada yenu alizkwa na dhahabu zake?

Hizi ndizo laana za ukoo, wataacha ukoo unaandamwa na kesi milele.
Nmemkumbuka yule kibo marealle

Ova
 
Hayo maeneo mengi yanapatikana bure bure Kama enzi hizoo,
pesa pesa ndugu, maeneo yamepanda Bei.
Maeneo yamepanda bei wapi?

Mashamba bwerere yenye rutuba ya kutosha. Ukiiuza hiyo simu yako unanunua ekari 2.
 
Kuweka Mipaka kwa kufukua kaburi la ndugu yenu. Ukoo mmoja.. yaani familia inafukua kaburi la mwanafamilia hiyo hiyo. Wachaga hapa wamezingua
Russia ni ndugu na Ukraine, nini kinaendelea pale Krimea.
China na Hong Kong ni ndugu, nini kinaendelea kwao?
 
Russia na ukraine wanatoka ukoo mmoja?

China na hongkong wanashea mama mdogo mmoja ?
Ni mahawara, case closed.

Russia and Ukraine ni Slavic relatives, tatizo elimu umekataa unabeti muda wote.

Hong Kong ilikuwa koloni la Uingereza hadi 1997 iliporejeshwa kwa Uchina chini ya kanuni inayojulikana kama "nchi moja, mifumo miwili." Mpango huu ulipaswa kuhakikisha kiwango cha juu cha uhuru wa Hong Kong, ikiwa ni pamoja na mifumo yake ya kisheria na kiuchumi, kwa miaka 50 baada ya kukabidhiwa.
 
Ni mahawara, case closed.

Russia and Ukraine ni Slavic relatives, tatizo elimu umekataa unabeti muda wote.

Hong Kong ilikuwa koloni la Uingereza hadi 1997 iliporejeshwa kwa Uchina chini ya kanuni inayojulikana kama "nchi moja, mifumo miwili." Mpango huu ulipaswa kuhakikisha kiwango cha juu cha uhuru wa Hong Kong, ikiwa ni pamoja na mifumo yake ya kisheria na kiuchumi, kwa miaka 50 baada ya kukabidhiwa.


acha maelezo mareefu ya kuunga unga na viingereza vingi.

jibu maswali yangu kwa lugha nyepesi kama maswali yalivyo.

1 - Russia na ukraine wanatoka ukoo mmoja?

2- China na hongkong wanashea mama mdogo mmoja ?
 

Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro,imeliamuru baraza la Ardhi wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro,kurejea upya mgogoro wa Ardhi wa familia maarufu ya chifu Marealle kwa kutembelea eneo linalobishaniwa na wanandugu hao na kurekodi upya mipaka na kisha kutoa maamuzi chini ya mwenyekiti mwingine wa baraza hilo

Jaji kuu,Lilian Mongella katika kesi namba 51/2023 ya mrufani Frank Mareale dhidi ya Ackley Mareale ambao wote ni wanandugu, Jaji Mongella alisema mahakama imepitia ushahidi na maamuzi ya Baraza la Nyumba na Makazi la Mji wa Moshi chini ya Uenyekiti wa Reginald Mtei yaliyotolewa mei 5 mwaka huu na kusema kuwa maamuzi hayo yalikuwa na kasoro za kisheria.

"Nimeamua kesi hii ya wanafamilia wa Mareale isikilizwe upya kwa sababu Baraza la Ardhi lilikosea kisheria kwa kushindwa kuonyesha mipaka ya ekari mbili inayogombaniwa"

Katika kesi ya awali iliyofunguliwa na Frank Mareale katika Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi katika Mji wa Moshi, alikuwa na madai matatu moja wapo ni ombi la Baraza hilo litamke kuwa eneo la ekari mbili yeye ni mmiliki halali, Pili Baraza litoe amri ya kufukuliwa kwa mwili wa mama yake mdogo marehemu Veronica Mareale aliyeishi katika eneo hilo miaka 80 na kufariki mwaka 2020 na pia alitaka alipwe gharama za kesi.

Akizungumza nje ya Mahakama,Wakili wa Ackley Mareale,Julius Semali alisema kuwa hana pingamizi na uamuzi wa Mahakama kwani ana uhakika kuwa mteja wake ni mmiliki halali wa eneo hilo kwa kuwa mama yake alipata kihalali na alizikwa katika eneo lake.

Naye Wakili wa frank Mareale,Modest Njau aliishukuru Mahakama Kuu kwa uamuzi wake wa kuiagiza Baraza la Ardhi Nyumba na MakaziMoshi kusikiliza upya kesi hiyo na aliamuru Mwenyekiti wa Baraza na wajumbe wake wabadilishwe.

Njau alidai Mahakama Kuu iliona jinsi haki ilivyokuwa ikitaka kuchezewa katika usikilizwaji wa awali nayeye na mteja wake wameridhika na maamuzi hayo

Mei 5 mwaka huu chini ya mwenyekiti wa Baraza hilo la Ardhi Nyumba na Makazi ,Reginald Mtei lilitupilia mbali madai hayo ya Frank Mareale na kusema kuwa Ackley Mareale ni mmiliki halali wa eneo hilo na sio vinginevyo
.
Familia za kiMangi ni problematic mikosi balaa na laana kwa sababu hapo awali walitoa binadamu kama sadaka i.e.kuzika watoto wadogo wakiwa hai "kichuminy"....kufukia mabikira wakiwa hai kwenye vichuguu e.t.c.
 
Hao jamaa na kupenda kurithi [emoji28][emoji28],sijawahi kuona jamii inayopenda mali za urithi kama hiyo na kuna wazee wa kupenda kesi huko Same.
Mkuu tunaishi kutafuta kwa kizazi kijacho , hauwezi kuzaa watoto kama una akili timamu usiwaachie chochote kama unacho.
 
Huwa ninawashangaa hawa ndugu zangu ni kipi haswa kinawafanya kuzozania vipande vidogo vya ardhi ya Kilimanjaro wakati nchi yetu ina maeneo mengi yasiyotumika.

Kilimanjaro pamejaa na ni eneo lenye population pressure kwa sasa.
Wapestina na Israel wanagombea kile kipande kidgo cha jagwa kwa sababu zipi?
 
Mkuu tunaishi kutafuta kwa kizazi kijacho , hauwezi kuzaa watoto kama una akili timamu usiwaachie chochote kama unacho.
Mimi lazima niache urithi yaani kama nitakuwa na Watoto wanne basi nitajenga nyumba nne ,hii kutokana na imani yangu .

Ishu ni kwamba ndugu hampashwi kugombana kwa namna yeyote ile.
 
Mimi lazima niache urithi yaani kama nitakuwa na Watoto wanne basi nitajenga nyumba nne ,hii kutokana na imani yangu .

Ishu ni kwamba ndugu hampashwi kugombana kwa namna yeyote ile.
Ni kwel kbisa ila mara nyingi ndugu wanaanza kuzinguana wakisha kuwa na mke ila hiv hiv sio rahisi.
 
Wakirudi Baraza la Ardhi na Nyumba kwa maombi hayo hayo matatu hilo ombi la pili hilo Baraza halitaweza kutoa na kama likitoa basi wakirudi Mahakama Kuu itatenguliwa tena.

Kwa uelewa na ufahamu wangu hilo ombi limeombwa wakati usio sahihi, mahala pasipo sahihi pia.

Ngoja nisubiri mtanange wao nijionee.
 
Mimi lazima niache urithi yaani kama nitakuwa na Watoto wanne basi nitajenga nyumba nne ,hii kutokana na imani yangu .

Ishu ni kwamba ndugu hampashwi kugombana kwa namna yeyote ile.
Amini atatokea mmoja pasua kichwa atake nyumba zote.

Nafuu la haya ni wosia japo nao unaweza kupingwa na yoyote kati ya uliowaacha.
 
Back
Top Bottom