Marefarii kutoka TZ katika Shirikisho muda huu!

Marefarii kutoka TZ katika Shirikisho muda huu!

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Waamuzi wa Tanzania ndio wanachezesha mechi ya shirikisho ambayo imeanza saa nne kamili kati ya RS Belkane vs Stellenbosch.

Mwamuzi wa kati-Ahmed Arajiga

Wasaidizi:

Salimu Mkono Mohamed
Seif Mpanga Kasimu
Nasir Salum Siyah

NB; Wengine hao wasaidizi wametoka Zanzibar sehemu ya Tanzania.

My take:

Hii mechi ntaiangalia mpaka mwisho mana sina usingizi ili nifanye tathmini kuhusu uwezo wa waamuzi wa Tanzania kwa kile wanachokifanya NBCPL na huko kimataifa ili kuona kama huwa kuna makusudi huku NBCPL!
 
Vipi huko, mbona updates hutoi..? Wanawezaweza.?
tunazungumzia marefa wa kibongo!
 
Vipi huko, mbona updates hutoi..? Wanawezaweza.?
tunazungumzia marefa wa kibongo!
Hahaha! Hadi muda huu dakika ya 37. Belkane 2- Stellen 0.

Mpaka sasa marefa wetu wanaenda vizuri.
Kama kawaida, Arajiga siyo mtu wa kadi za haraka haraka. Kuna jamaa w Belkane kacheza rafu mbaya ila Arajiga kamuonya sana bila kadi!
 
Waamuzi wa Tanzania ndio wanachezesha mechi ya shirikisho ambayo imeanza saa nne kamili kati ya RS Belkane vs Stellenbosch.

Mwamuzi wa kati-Ahmed Arajiga

Wasaidizi:

Salimu Mkono Mohamed
Seif Mpanga Kasimu
Nasir Salum Siyah

NB; Wengine hao wasaidizi wametoka Zanzibar sehemu ya Tanzania.

My take:

Hii mechi ntaiangalia mpaka mwisho mana sina usingizi ili nifanye tathmini kuhusu uwezo wa waamuzi wa Tanzania kwa kile wanachokifanya NBCPL na huko kimataifa ili kuona kama huwa kuna makusudi huku NBCPL!
Vp Kayoko hayupo?
 
Hahaha! Hadi muda huu dakika ya 37. Belkane 2- Stellen 0.

Mpaka sasa marefa wetu wanaenda vizuri.
Kama kawaida, Arajiga siyo mtu wa kadi za haraka haraka. Kuna jamaa w Belkane kacheza rafu mbaya ila Arajiga kamuonya sana bila kadi!
Mpira ni half time. Belkane 2-Stellen.
Kumbe udhaifu wa Arajiga ni kutotoa kadi haraka. Hata wachambuzi wa Azam wamesema kuwa, kwa ile rafu ya mchezaji wa Belkane, Arajiga alipaswa amuonye kwa kadi hata ya njano. Yule mchezaji alicheza rafu mbaya sana kwa kuteleza miguu yote mbele ya mchezaji wa Stellen
 
Dakika ya 67 Belkane anapata goli la tatu. Hili goli imepigwa pasi zile ndefu kwenda kwa straika na akawakimbia mabeki. Mipira kama hii huwa inawasumbua sana malinesmen NBCPL hasa Simba na Yanga wanapocheza na timu ndogo, lakini kwa huku linesman Salimu Mkono kakimbia na muvu na hakukua na offiside, goli likafungwa
 
Dakika ya 71, Arajiga anatoa kadi ya kwanza ya njano kwa mchezaji wa Stellen
 
Dakika ya 75 Belkane wanapata goli la nne lakini linakataliwa ni offside.

Kweli ni offside. Linesman Salimu Mkono anajitahidi kwenda na muvu!
 
natest mzigo nione kitu chaarusha kweli au feki.
👇
Baba Abdu amchapa makofi mama Abdu wa magogoni kwa kuzurula hovyo.

haa,,,kumbe chenyewe bana ni og.
 
Dakika ya 80 Belkane wanapata goli la nne.

Arajiga anatoa kadi ya pili ya njano kwa Stellen mana alimchezea rafu mchezaji wa Belkane aliyefunga goli. Inawezekana angekosa labda ingekuwa penati
 
Dakika 84 Belkane wanapata goli la tano. Stellen 0
 
Back
Top Bottom