Marehemu Ayubu Kiguru: Shabiki mkubwa wa Sunderland football club miaka ya 1960

Mzee Mwita alishafariki kumbe! Oooh namfahamu alikuwa akiishi Magomeni Mikumi. R. I. P.

Kaka ...
 
Unaweza kutukumbusha kisa cha kitwana kucheza nafasi mbili yaani mshambuliaji na golikipa nafasi ambazo alizimudu vyema ilikuwaje?
 
Ok Shukran
Wanamajlis,
Kwa wale wanaopenda kusoma historia ya soka la zamani nimeongeza vitu
katika makala ya Athmani Kilambo.

Nashukuru kuwa JF imenipa nafasi ya kumkumbuka Kilambo ambae yeye
siku zote akiniita kwa nickname yangu ya ''Sidney,'' lakini yeye akitamka,
''Signal.''

Ichukulieni hii kama taazia yake:
Mimi sikuzote nikimuita, ''Kaka Kilambo:''
Mohamed Said: KUTOKA JF: MAREHEMU ATHMAN KILAMBO: YOUNG AFRICANS NA TIMU YA TAIFA MSHINDI WA GOSSAGE CUP 1964 NA 1965

Jumapili iliyopita nilikuwa na Captain Malik kwa kipindi kirefu.


Wakwanza kulia ni Captain Malik

Captain Malik alikuwa Captain wa Yanga nadhani katika miaka
ya awali ya 1960 na ndiye aliyempokea Kilambo Yanga akitokea
Bagamoyo na kumtia moyo kuwa anaweza kupata nafasi kikosi cha
kwanza.

Juzi alinihadithia mkasa uliotokea Ilala Stadium.

Yanga walikuwa na mechi na wachezaji wote walikuwa weshaingia
uwanjani lakini Kilambo alikuwa kachelewa.

Hakuna aliyekuwa anamjua Kilambo wakati ule hivyo akazuiwa lango
kuu ikabidi Captain Malik aende akampitishe mlangoni.

Sifa moja kubwa ya Captain Malik ni kuwa yeye ni Encyclopedia ya
historia ya mpira Tanzania.
 
Umesema ulikuwa unaenda mazoezini na vitabu vya kusoma wakati wenzako wanapiga danadana.

Naomba kuuliza: what became of your formal education?

Ulisoma shule wapi na kama ulienda chuo chuo gani, shahada ya kwanza na ya pili kama zipo zilikuwa za nini na wapi.

Siko sana interested na shule ama vyuo na shahada za kujiendeleza ukubwani, nataka zile ulizosoma moja kwa moja toka utotoni bila kusimama na kuunga unga tafadhali. Ahsante.
 
Buyaka,
Ndugu yangu sina elimu yoyote usitabike.

Elimu yangu inayonisaidia ni hii nilosoma kwa Maalim Haruna
yeye alinifunza mlango wa mnakasha, yaani mijadala na adabu
zake na vitu vingine vidogo vidogo.

Ilm hii ndiyo inayoniwezesha kuwa hapa JF.
 
Nikisoma khabari hizi za wakongwe kwanza majina yao ya asili na ya utani napata burdan hassan gobos omar Chogo mohamed chuma huku mkweche kule katolila Ibrahim kiswabi thuweni ally alloo mwitu Shaaban baraza. Basi hupata hamasa ya kujua wasifu wao.
 
Ahsante sana mwana kariakoo mwenzangu
 
Ukisha jua zitakusaidia nini? Bw. Mohd Said ameandika kuhusu mambo ya michezo na wale aliyocheza nao pamoja na wanamichezo/mashabiki wa kweli wa enzi hizo sasa huko unakokwenda ni wapi???????
 
Duuuuh!!!!!!!!!!!!!! wewe utakuwa mgeni JF
 
Nikisoma khabari hizi za wakongwe kwanza majina yao ya asili na ya utani napata burdan hassan gobos omar Chogo mohamed chuma huku mkweche kule katolila Ibrahim kiswabi thuweni ally alloo mwitu Shaaban baraza. Basi hupata hamasa ya kujua wasifu wao.
Guasa,
Hassan Gobbos
Yanga wakimwita King Hassan wa Morocco.
Alloo Mwitu na Hamisi Askari waliletwa kutoka Kigoma na
Hamisi Kilomoni waje wacheze Simba.

Wote wawili walikuwa wanacheza nyuma.
Chogo jina lake ni Juma alianza mpira Young Kenya.

Hii ''Chogo,'' ni sababu ya kichwa chake.
Kulikuwa na Said Ndomo.

Hii ''Ndomo,'' ni kwa ajili ya mdomo wake.

Said alianza mpira katika club ya mtaani New Port kisha akenda
Cosmopolitan.

Kwenye maziko ya Kilambo nilikutana na Said baada ua kupoteana
kwa muda mrefu sana.

Nadhani yeye kanishangaa mimi kwa kuona nimezeeka kama mimi
nilivyomshagaa yeye.

Kulikuwa na Mustafa Mabuge kwa kuwa miguu yake ilikwenda upande
kwa ajili ya funza.

Ndiyo hiyo ''Mabuge.''
Yeye alikuwa beki na mbili wa Cosmo ya 1960s mwanzoni.

Huyu alikuwa mwana Gerezani mwenzangu.
 
Ukisha jua zitakusaidia nini? Bw. Mohd Said ameandika kuhusu mambo ya michezo na wale aliyocheza nao pamoja na wanamichezo/mashabiki wa kweli wa enzi hizo sasa huko unakokwenda ni wapi???????
Abunuwasi,
Iko siku niko Marekani nafanyiwa utambulisho kabla sijapanda jukwaani
kuzungumza.

Mzungumzaji kanipamba mwisho wa kunipamba.

Ghafla inanijia picha ya marehemu mama yangu nina miaka mitano tuko
sokoni kwa muuza vitabu ananinunulia kitabu cha ''Jifunze Kusoma.''

Anamlipa muuzaji ananikabidhi kitabu na tulipofika nyumbani yeye ndiye
mwalimu ananianzisha alif kwa kijiti.

Kuna kitu kilipanda hadi kooni kikanikwama machozi yanataka kunitoka.

Najiambia, ''Ingekuwaje mama yangu, mwalimu wangu Bi. Mwanaidi biti
Sheikh
leo ungelikuwa hapa ukaniona mie mwanao nahadhiri chuo kikuu
Marekani na hawa Wazungu wameitana kuja kunisikiliza...''

Laiti mzungumzaji angeliendelea zaidi ningelihadhirika.
Ningeliwamwagia chozi...

Abunwasi,
Hayo mimi ninakutananayo kila siku wala yasikupe tabu.

Huyo anaugua maradhi ya nafsi na ni mabaya sana kwani tiba yake ni ghali
mno.

Ngoja nihitimishe.

Alikuja Mhariri wa Oxford Univeristy Press kutoka Nairobi kuja turekebishe vitu
fulani katika kitabu nilichoandika ili wakichape.

Tumeifanya kazi tushamaliza.
Kumbe huyu bwana ana kitu kinamchonyota.

Muda wote tukisema Kiswahili.

Sasa anafunga lap top yake ananiuliza, ''Mr. Said hiki kitabu uliandika kwa Kiswahili
halafu ukampa mtu akuwekee kwa Kiingereza?''

Jibu langu lilikuwa hapana.
Nikataka tufahamiane ili siku nyingine anipe kazi.

Nikamwambia nina First Class Merit Pass English Oral Cambridge Examination 1970.

Mimi nilimwia radhi kwa kuwa alikuwa akisikia Kiswahili changu kina ''heavy accent,''
ya usemaji wa Kidaresalama ikamjia fikra nyingine.
 
Iko siku niko Marekani nafanyiwa utambulisho kabla sijapanda jukwaani
kuzungumza.
hahahahahahaaaaaaaaaaa.....

Naona umerudi kivingine, nilidhani ulisema hujasoma vya ajabu!

JF hapa tupo waponda zege na wauza ulanzi na wahandisi na mawakili na madaktari na wauza simu na kila aina ya watu na tunajadili masuala ya kijamii kwa pamoja.

Sasa wewe uliyejinasibu kwamba uko hapa unatoa somo kwa sababu tangia utotoni ulikuwa unaenda mpirani na vitabu wakati wenzio wanacheza dana dana, basi hebu niambie synopsis ya elimu yako ni nini. Ulisoma msingi wapi, sekondari wapi, chuo kama ulienda ulienda lini, ulienda wapi na ulisomea nini Mohammed Said.

Utaonaje aibu kusema elimu yako wakati umejinadi kwamba ulikuwa unaenda uwanjani na vitabu wenzako wanacheza mpira? hahahahahaaaaaaaa...... !
 
Nimepata kujua namna gobbos alivyopata kuitwa pia nini kilitokea mpaka kukawa na yanga raizoni (rise on )na wengine kujiita kandambili au gongo wazi?
 
Bu'yaka,
Kweli sijasoma na sioni aibu kukwambia kuwa sijasoma.

Wewe kwa kuwa mgeni hapa majlis ndiyo hili jibu langu
linakustaajabisha.

Kuna mtu kakuuliza we mgeni?
Sababu mie nafahamika kuwa hamna shule hapa.

Ila toka utoto nikipenda kusoma.

Huyo George Orwell mie nimemsoma nikiwa na umri wa
miaka 15.

Unataka nijipe sifa nisokuwanayo?
Hii ndiyo itakuwa aibu.

Aibu siyo kusema kweli.

Kuwa natoa darsa hili mbona liko wazi?
Huku si kujinasibu.

Niko hapa majlis miaka mingi sasa nikitoa darsa.

Unataka nikueleze kuwa nilisoma mashule makubwa makubwa
ya Dar es Salaam wakati si kweli?

Au nimesoma chuo kadha wa kadha hapa nyumbani kisha Uingereza,
Marekani na kwengineko wakati si kweli si nitakuwa najifedhehesha?

Na ikiwa kweli nimesoma huko hii itakuwa si uungwana kwani itakuwa
najinasibu.

Waswahili sisi tumefunzwa na wazee wetu kutojinasibu kwani hiyo si
katika mafunzo ya adabu njema.

Kwani kwenu umefunzwaje?
Nipe ruhusa nikuelekeze jambo.

Unapoweka nukta zinatakiwa ziwe tatu...
Hizi ndizo kanuni za uandishi...

Huweki msururu......
Watu watakucheka watajua lipo tatizo la skuli...

Lakini mimi sitocheka kama ulivyocheka wewe.
Hapa ni mahali pa kufunzana mengi pamoja na adabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…