Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Andika kwa ufasaha. Nimerudi pale pale kwenye kipi?

Nimekukumbusha pia badala ya kutumia neno hati ya manunuzi tumia neno mkataba wa manunuzi. Hati na mkatana ni vitu viwili tofauti

Nimekueleza kama mkataba wa manunuzi una jina la mwanaume, hapo ulitaka mwanamke afatilie vipi kuhusu hati? Mwanaume ndio atafatilia na jina litatoka la kwake, sababu kwenye mkataba na transfer forms Kuna jina lake. Hapo hujaelewa wapi?

Pia hati sio wizarani tena, kuna ofisi ya kamishna wa ardhi kila mkoa. Hapo ndio utafatilia hati yako na utapewa hapo, baada ya kumalizana Kila kitu na halmashauri
 
Kuna watu wengine wanakua na hasira mpaka wnmatetemeka , nina ndugu ana hasira mpaka anang'ata ulimi wake unatoa damu au kupiga ngumi ukutani ila kikawaida ni mpole mno
ishini naye kwa umakini na tahadhari siku mkikanyaga waya wenye shoti ndo hamtaamini atacho mfanya mtu.
 
Ninachoweza kusema Kweka amekosea Ila maneno matupu kama “Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati” tena yaliyosemwa na house girl hayatoshi kufanya tuseme ana-play role kubwa kwenye tukio.

Hakuna asiyejua viwanja vingi vya Bunju vimenunuliwa kwa uvamizi kupitia serikali za mitaa husika kuandaa hati za mauzo fake na kuuza maeneo yaliyo wazi kwa bei chee vingine 800K mpaka 1Mill so kama marehemu alikuwa mjanja akawahi kwa bei hiyo na mume akajenga nyumba ya million 50+ then akamletea wenge tutegemee nini?

Tamaa haijawahi kuwa nzuri kabisa!
 
Kama walifunga ndoa inakuaje Mali ya mwanamke!!?je zile Mali za mwanamme alizonunua ni zake peke yake au za wote!!?

Acheni ubinafsi kama wameoana chochote atakachonunua yeyote na vya wote na sio vya mwanamke wala vya mwanamme!!!

Bado risasi zitawahusu sana!
 
ukisema vya uvamizi manake kuna wenye hati za mwanzo? na hata kama mke alinunua hati ipo wapi mana kama angalikuwa anafwata sheria wala haya yasinge mkuta endapo kama alistahili kudai icho mnacho mlinda nacho kuhusu umiliki wa awali.
 
Kuna watu wengine wanakua na hasira mpaka wnmatetemeka , nina ndugu ana hasira mpaka anang'ata ulimi wake unatoa damu au kupiga ngumi ukutani ila kikawaida ni mpole mno

Hasira sio hali ya kawaida. Ukowa na hasira maana yake hakuna nafasi ya kufanya reasoning. Ndio maana hasira kali zinahusishwa na ugonjwa wa akili.

Utimamu wa binadamu ni pamoja na uwezo wake wa kudhibiti hasira. Hasira inaishia kwenye aibu, kudhuru mwili, kuharibu mali na vifo.
 
Huna guts za kunambia niandike kwa ufasaha.Kuna shida gani nilitumia hati ya manunuzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…