Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Wakati wa Kikwete kulitokea watu kuvamia maeneo ya wazi yaliyokaa muda mrefu bila kuendelezwa ya wamiliki wasiokuwa na hati zinazojulikana so wakagawana gawana wachache wenye nguvu walifanikiwa kuyarudisha ile wengi walipoteza.

Ndiyo nikasema huyo marehemu kama kweli alipanunua kwenye wimbi hilo la uvamizi mume akajenga nyumba ya thamani kubwa kwanini yasitokee yaliyotokea?
Kwani habari inasema mume ndiye aliyejenga? Kwa mujibu wa hii habari kiwanja na nyumba ni mali ya bibie🤣
 
Tengeneza fact mkuu acha mambo ya fallacy of generations umefikiaje hilo hitimisho la hakuna ?
Hata kama ni wewe unajiona ukikubali kutia hela zako kuinua jengo kwenye kiwanja alichonunua mkeo?as for me sioni ikiwezekana kabisa!
 
Inas
Tukio la kushtua limetokea Mtaa wa Senzele, Kata ya Bunju B, jijini Dar es Salaam, baada ya Laurent Kweka kudaiwa kumuua mkewe, Jeni Urassa, kwa kumpiga risasi kichwani kisha kujisalimisha Polisi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Alhamisi, Oktoba 1, 2026, majira ya saa 11:30 alfajiri ndani ya nyumba ya wanandoa hao. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya upelelezi.

Kwa mujibu wa Mafwele, Laurent na marehemu walikuwa wanandoa na wote walitoka mkoani Kilimanjaro. Ameongeza kuwa baada ya uchunguzi na taratibu za kisheria kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo, Rebecca Mbasha, ambaye amefanya kazi nyumbani hapo kwa miaka minane, amesema mauaji hayo yanadaiwa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu umiliki wa nyumba.

Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.

Amesema siku ya tukio Laurent aliingia nyumbani na baada ya muda mfupi alimsikia Jeni na baadaye akasikia kishindo. Aliporejea ndani, alimkuta Laurent akitoka chumbani akiwa ameshika bastola na kumwambia, “nimeshamaliza kazi.” Rebecca alipokwenda chumbani alimkuta Jeni akiwa ameanguka chini akiwa na jeraha kichwani.

Kwa upande wake, Jacqueline Nkaya, ambaye ni mama mdogo wa marehemu, amesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na wakati mmoja Jeni aliwahi kutishiwa kuuawa kwa bastola na mumewe, jambo aliloliripoti Polisi.

Amesema Laurent aliondoka na kwenda Kilimanjaro ambako alikaa takribani miezi miwili kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya tukio.

Majirani wamesema hawakuwa na taarifa za migogoro hiyo, wakieleza kuwa familia hiyo ilikuwa ikionekana kuishi kwa amani tangu ilipohamia katika nyumba hiyo Desemba 2025.

Marehemu ameacha watoto wanne, watatu wakiwa shuleni na mmoja bado hajaanza shule.
Chanzo : Global

Vijana tuache kulazimisha mambo tufanye kazi tusing'ang'anie mali za wanawake
Inasikitisha sana LAKINI haya ni maelezo ya upande mmoja.
 
Kaka mbaga jr hakuna kosa lolote ambalo ni la msingi kiasi cha kulitatua kwa kuondoa uhai wa mtu.

Hata kosa liwe kubwa kiasi gani, uhai bado unathamani.


Pumzi hailinganishwi na kitu chochote.


Jamaa anaenda kufia nyuma ya nondo sasa kipi bora hapo?
Hadithiwa au endelea hivi hivi kusoma ya watu ila omba sana yasikukute!
 
Kaka mbaga jr hakuna kosa lolote ambalo ni la msingi kiasi cha kulitatua kwa kuondoa uhai wa mtu.

Hata kosa liwe kubwa kiasi gani, uhai bado unathamani.


Pumzi hailinganishwi na kitu chochote.


Jamaa anaenda kufia nyuma ya nondo sasa kipi bora hapo?
Ishu kama hizi za kuuana haziibuki ghafla tuu, kuna mlolongo wa maumivu nyuma yake, tungemsikia jamaa atleast tungepata la maana la kusema na sio kumhukumu jamaa kwa maneno ya dada wa kazi.
 
Amejisalimisha! Ila madhara ya kesi ya mauji hayajui!
Hapo hana tena nyumba,ni maskini kuliko wasio na nyumba,watoto ni yatima sasa! Akirudi kutoka magereza ni mwaka 2050 hana meno wala haoni
Hasira ni mbaya. Kafanya maamuzi ya kijinga sana majuto ni heri aliyekufa.
 
Ahaa wapi ingekuwa yeye ndio ana mchango mkubwa kwenye hiyo nyumba asingekubali tokaa mwanzo hati ya kiwanja iwe kwa jina la mwanaume.unawajua wanawake wa kiafrika ww.
Ukisoma between the lines inaonekana majina yote mawili yalikuwepo kwenye Hati. Nadhani baada ya mvurugano kwenye ndoa Mwanamke alikuwa anataka kuondoa jina la mwanaume LIBAKI lake na watoto.
 
Hadithiwa au endelea hivi hivi kusoma ya watu ila omba sana yasikukute!
Kitu gani chenye thamani kuzidi uhai mkuu ?

Mjinga pekee ndiye atae nyanyua siraha na kuua.

Nitajie hicho kitu chenye thamani zaidi ya uhai hapa !!

Don’t argue with the devil. Unahisi wewe ndiye umetendewa ubaya kuliko wengine.?

Au wewe ndiye unayejua suluhisho la matatizo kuliko kila mtu.?

Wakati mwingine akili yenye busara ni ile inayoshinda mabishano na kulinda maisha.

Unaongea kunikuta ? Mimi yamesha nikuta mazito nikiongelea mazito namaanisha Confiscation.

Unadhani huyu jamaa alie nifanya nifanyiwe Confiscation nlishindwa kumtumia watu wamfanyie umafia ?

Mkuu uhai ni uhai
 
Hahaha. Sasa sisi tuliosomesha wake na wachumba zetu ambao bado hawajaliamsha li "kazeze" na bado wapo "very loyal" tufanyeje mkuu? Tununue bastola kwa tahadhari? Halafu hujagusia kuhusu huyo mdada wa kazi anaonekana anajua sana mambo ya ndani ya mabosi wake.
Maombi yanahitajika.House girl anaweza kuwa anayafahamu ya ndani kama atapewa urahisi wa kuyafikia au akiwe mpekepeke tu.
 
Ishu kama hizi za kuuana haziibuki ghafla tuu, kuna mlolongo wa maumivu nyuma yake, tungemsikia jamaa atleast tungepata la maana la kusema na sio kumhukumu jamaa kwa maneno ya dada wa kazi.
Ni sahihi lakini kuua haikubaliki haijalishi ukubwa wa maumivu kaka mbaga jr.
 
Kuna shida,elimu ndogo, amekutana na fedha,akili inahama!
Akili itakwenda kurudi,akiwa magereza,na akikumbuka mke alikufa na watoto ni yatima,na nyumba imebaki haina mwenyewe!
 
Wamama wa Kichaga hii laana ya umiliki wa mali na tamaa ya mali sijui watatakasa lini. Kulikuwa na ulzima gani wa kutaka hati iwe kwa jina lake tu wakati wao ni wanandoa.
 
Wamama wa Kichaga hii laana ya umiliki wa mali na tamaa ya mali sijui watatakasa lini. Kulikuwa na ulzima gani wa kutaka hati iwe kwa jina lake tu wakati wao ni wanandoa.
Mikopo na mume kuwa na Hawara!
 
Moja kati ya mbinu za kitoto sana wanawake wanazotumia ni kukimbilia kuandikwa majina yao kwenye hati za nyumba, viwanja, hata kadi za magari, mara nyingi ni ushauri mbovu ama kutoka kwa Mama mzazi au marafiki, au pia Watumishi wapigaji, lakini pia Biblia kwa sisi Wakristo imetuasa kuishi nao kwa akili ( kuishi nao kitaalam sana), sio kila kitu unaanika kwake huo ni upumbavu wa kiwango cha lami, na hakikisha muda wote una mchunga kama mtoto, kama ambavyo mtoto kwa mama hakui, ndivyo mwanamke kwa Mume hawezi kukua, Dada zetu wa kichaga wana tamaa sana ya Mali,
 
M
Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.
Mke wake ametokea Kilimanjaro ( Angemalizia kabisa kwa kusema ni .. Mchaga)
Mmachame
 
Nasema hv, mshikaji yupo sahihi
hayupo sahihi. Angemuachia tu nyumba yake na watoto wake yeye akaanza kutafuta maisha yake binafsi. Hichi alichofanya kina hasara kubwa kwa watoto na kwake binafsi. Anaweza kuhukumiwa kunyongwa na kifungo cha Maisha jela wakati huku nje watoto hawana mama wala baba na bado ni wadogo.
 
Mimi nafikiri watuhumiwa wa mauaji kama haya wawe wanapewa nafasi ya kusimulia upande wao na stori hizo ziwekwe public. Kuna mambo mengi yanakua yanaendelea hadi mtu kuchukua hatua nzito kama ya kuua. Kuendelea kufanya mambo haya ni siri ya wapelelezi tunakosea sana.
Yatawekwa public mahakamani chini ya kiapo. Maana hata yakiwekwa public leo pasi na kiapo yet yatakuwa hayaaminiki kama ambavyo taarifa na statements za awali polisi hukataliwa mahakamani. Be patient!
 
Back
Top Bottom