Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Hilo bwege lililompiga risasi huyo dada ni jitu lis3ng3 tu.. na akili halina...

Unaua mtu , tena mkeo kisa nyumba? Huyo jamaa anyongwe tu..

Tukio la kushtua limetokea Mtaa wa Senzele, Kata ya Bunju B, jijini Dar es Salaam, baada ya Laurent Kweka kudaiwa kumuua mkewe, Jeni Urassa, kwa kumpiga risasi kichwani kisha kujisalimisha Polisi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Alhamisi, Oktoba 1, 2026, majira ya saa 11:30 alfajiri ndani ya nyumba ya wanandoa hao. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya upelelezi.

Kwa mujibu wa Mafwele, Laurent na marehemu walikuwa wanandoa na wote walitoka mkoani Kilimanjaro. Ameongeza kuwa baada ya uchunguzi na taratibu za kisheria kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo, Rebecca Mbasha, ambaye amefanya kazi nyumbani hapo kwa miaka minane, amesema mauaji hayo yanadaiwa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu umiliki wa nyumba.

Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.

Amesema siku ya tukio Laurent aliingia nyumbani na baada ya muda mfupi alimsikia Jeni na baadaye akasikia kishindo. Aliporejea ndani, alimkuta Laurent akitoka chumbani akiwa ameshika bastola na kumwambia, “nimeshamaliza kazi.” Rebecca alipokwenda chumbani alimkuta Jeni akiwa ameanguka chini akiwa na jeraha kichwani.

Kwa upande wake, Jacqueline Nkaya, ambaye ni mama mdogo wa marehemu, amesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na wakati mmoja Jeni aliwahi kutishiwa kuuawa kwa bastola na mumewe, jambo aliloliripoti Polisi.

Amesema Laurent aliondoka na kwenda Kilimanjaro ambako alikaa takribani miezi miwili kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya tukio.

Majirani wamesema hawakuwa na taarifa za migogoro hiyo, wakieleza kuwa familia hiyo ilikuwa ikionekana kuishi kwa amani tangu ilipohamia katika nyumba hiyo Desemba 2025.

Marehemu ameacha watoto wanne, watatu wakiwa shuleni na mmoja bado hajaanza shule.
Chanzo : Global

Vijana tuache kulazimisha mambo tufanye kazi tusing'ang'anie mali za wanawake
nimesikitika sana jamaa kaacha Barcelona anashinda tu ,psv anatoa chuma mbili kila game,pirates wanashinda tu,Liverpool kocha wake ajapoteza game ya 20+ ,yanga anashinda tu ,simba anashinda tu,PSG kila game anafunga goli,intermilan anafunga goli kila mechi , yaani ukiweka Hela unapata viwanja na nyumba nyingi nyingi nimelia sana ,ka nyumba ka moja kweli?
 
Hii kitu km haijakukuta unaeza hisi ni move....niligombana na wife ishi ndogo tu....siku ya pili yake narudi home nakuta chumba ni cheupeee.....kasomba kila kitu kahamishia kwao na kwao kapokolewa vzr tu,...na nikaambiwa kbisa apa hmn kitu kinatoka mpk ndugu zako waje kusuruhisha.....,just imagin ni makabati,friji etc an vile vitu vya ndani tu vnavyohamishika mfano km ningejenga nae??...ingekuaje apo c alkuwa ananiua uyu?...!af baada ya mwaka mmoja anasumbua kurudi ety shetani tu weeee....
 
Hivi lazma kuoa?!
Basi nashauri itokewe elimu vizuri ya prenup aggreements(mkataba wa namna mali zikae kabla ya kufunga ndoa) kuliko hivi kuishi mnachungamilana!
Watu wanaoa kuepuka kuambiwa ni mashoga, au wanaolewa kuepuka kuambiwa ni wasagaji, ilihali wao binafsi ndoa hawazitaki wala ndoa yenyewe haiwahitaji, wanaamua kuishi kinafiki, mwisho scenes za maigizo zinaisha, unakuja uhalisia sasa, ndipo Risasi, magunia ya mkaa au sumu zinahusika.
 
Tukio la kushtua limetokea Mtaa wa Senzele, Kata ya Bunju B, jijini Dar es Salaam, baada ya Laurent Kweka kudaiwa kumuua mkewe, Jeni Urassa, kwa kumpiga risasi kichwani kisha kujisalimisha Polisi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Alhamisi, Oktoba 1, 2026, majira ya saa 11:30 alfajiri ndani ya nyumba ya wanandoa hao. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya upelelezi.

Kwa mujibu wa Mafwele, Laurent na marehemu walikuwa wanandoa na wote walitoka mkoani Kilimanjaro. Ameongeza kuwa baada ya uchunguzi na taratibu za kisheria kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo, Rebecca Mbasha, ambaye amefanya kazi nyumbani hapo kwa miaka minane, amesema mauaji hayo yanadaiwa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu umiliki wa nyumba.

Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.

Amesema siku ya tukio Laurent aliingia nyumbani na baada ya muda mfupi alimsikia Jeni na baadaye akasikia kishindo. Aliporejea ndani, alimkuta Laurent akitoka chumbani akiwa ameshika bastola na kumwambia, “nimeshamaliza kazi.” Rebecca alipokwenda chumbani alimkuta Jeni akiwa ameanguka chini akiwa na jeraha kichwani.

Kwa upande wake, Jacqueline Nkaya, ambaye ni mama mdogo wa marehemu, amesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na wakati mmoja Jeni aliwahi kutishiwa kuuawa kwa bastola na mumewe, jambo aliloliripoti Polisi.

Amesema Laurent aliondoka na kwenda Kilimanjaro ambako alikaa takribani miezi miwili kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya tukio.

Majirani wamesema hawakuwa na taarifa za migogoro hiyo, wakieleza kuwa familia hiyo ilikuwa ikionekana kuishi kwa amani tangu ilipohamia katika nyumba hiyo Desemba 2025.

Marehemu ameacha watoto wanne, watatu wakiwa shuleni na mmoja bado hajaanza shule.
Chanzo : Global

Vijana tuache kulazimisha mambo tufanye kazi tusing'ang'anie mali za wanawake
Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.
 
Hahaha. Sasa sisi tuliosomesha wake na wachumba zetu ambao bado hawajaliamsha li "kazeze" na bado wapo "very loyal" tufanyeje mkuu? Tununue bastola kwa tahadhari? Halafu hujagusia kuhusu huyo mdada wa kazi anaonekana anajua sana mambo ya ndani ya mabosi wake.
Wewe andaa bastola haswaa, maana kikilipuka ni ku trigger tu 🔫 unasikia paaah.
Kwishaaaa. 😂😂😂
 
Kaka mbaga jr hakuna kosa lolote ambalo ni la msingi kiasi cha kulitatua kwa kuondoa uhai wa mtu.

Hata kosa liwe kubwa kiasi gani, uhai bado unathamani.

Pumzi hailinganishwi na kitu chochote.

Jamaa anaenda kufia nyuma ya nondo sasa kipi bora hapo?
Ila Wabongo kwa unafiki hamjambo, sio nyie mnaobwataga Mashoga wauawe, sio nyie? Leo mnasema Pumzi hailinganishwi na chochote.

Nasemaje Uaneni tuu, sisi kwetu ni sherehe.
😂😂😂😂
 
Ni quote nilipo ongea hiyo kauli !

usifurahishe genge kwa useless comment.

Em quote statement yangu inayosema hayo madai yako.
 
Msitudanganye,hakuna mwanaume wa kichaga akubali kuoa au kuishi kwenye kiwanja na nyumba aliojenga mwanamke,nasema hakuna,huyo jamaa atakuwa na mchango mkubwa sana hapo,ingekuwa wanaume wa Dar ningukubali...
Hakika Huo ndo ukweli. Uchagani kamwe "mwanaume haolewi".
 
Hii kitu km haijakukuta unaeza hisi ni move....niligombana na wife ishi ndogo tu....siku ya pili yake narudi home nakuta chumba ni cheupeee.....kasomba kila kitu kahamishia kwao na kwao kapokolewa vzr tu,...na nikaambiwa kbisa apa hmn kitu kinatoka mpk ndugu zako waje kusuruhisha.....,just imagin ni makabati,friji etc an vile vitu vya ndani tu vnavyohamishika mfano km ningejenga nae??...ingekuaje apo c alkuwa ananiua uyu?...!af baada ya mwaka mmoja anasumbua kurudi ety shetani tu weeee....
😂😂😂
 
hayupo sahihi. Angemuachia tu nyumba yake na watoto wake yeye akaanza kutafuta maisha yake binafsi. Hichi alichofanya kina hasara kubwa kwa watoto na kwake binafsi. Anaweza kuhukumiwa kunyongwa na kifungo cha Maisha jela wakati huku nje watoto hawana mama wala baba na bado ni wadogo.
Ukiskia "Mbwai na iwe mbwai" ndo ivo sasa. -ama zako ama zangu.
 
Ni quote nilipo ongea hiyo kauli !

usifurahishe genge kwa useless comment.

Em quote statement yangu inayosema hayo madai yako.
😂😂😂 hata km hujawahi kuandika, ila unashadadia, means hukuwahi pinga hilo.
Nasemaje nyie uaneni. Sisi kwetu ni sherehe.
😂😂😂
 
Moja kati ya mbinu za kitoto sana wanawake wanazotumia ni kukimbilia kuandikwa majina yao kwenye hati za nyumba, viwanja, hata kadi za magari, mara nyingi ni ushauri mbovu ama kutoka kwa Mama mzazi au marafiki, au pia Watumishi wapigaji, lakini pia Biblia kwa sisi Wakristo imetuasa kuishi nao kwa akili ( kuishi nao kitaalam sana), sio kila kitu unaanika kwake huo ni upumbavu wa kiwango cha lami, na hakikisha muda wote una mchunga kama mtoto, kama ambavyo mtoto kwa mama hakui, ndivyo mwanamke kwa Mume hawezi kukua, Dada zetu wa kichaga wana tamaa sana ya Mali,
Yule Mwimbaji maarufu aliimba: "No woman, No cry"
 
Back
Top Bottom