Mabunge yaliyopita wabunge wa upinzani hususani Chadema walikuwa mstari wa mbele kudadisi na kuujulisha umma pale sintofahamu yoyote inapotokea, anasema mzee Mgaya.
Hebu fikiria mbunge anapata ajali Dodoma tena imehusisha gari tatu na pikipiki na zote zimekokotwa hadi polisi lakini wapiga kura wake na wananchi hawapati taarifa? Anauliza Mgaya.
Hata PM mh Majaliwa amesikitika sana kwa serikali kutotaarifiwa juu ya ajali hiyo na hata wapiga kura wake ambao wangeweza kumuombea badala yake wanaarifiwa tu msiba tena baada ya wabunge wa CCM kuanza kuhoji yuko wapi mwenzetu Nditiye?
Mzee Mgaya anaomba udhaifu huu uliotokea kwenye ofisi ya Katibu wa bunge usijirudie tena.
Mgaya anamalizia kwa kusema " Tumeanza kuwakumbuka akina Mnyika "
Maendeleo hayana vyama!