Marekani: Apigwa risasi baada ya kugonga mlango usio sahihi

Kutoka nchini Marekani, Mzee mwenye umri wa miaka 84, Andrew Lester anatuhumiwa kumpiga risasi kijana wa miaka 16 aliyekosea anuani ya nyumba aliyokuwa anaenda na kuenda kupiga hodi nyumbani kwake.

Ralph Yarl siku ya Alhamisi alitumwa na wazazi kwenda kuwachukua ndugu zake kwa kupewa anuani ya nyumba, Ralph alikosea nyumba na kufika nyumbani kwa Andrew Lester ambaye baada ya kupiga kengele mlangoni kwake alifungua dirisha na kumpiga risasi iliyomsababishia majeraha.

Andrew Lester ameshakamatwa na polisi kwa makosa mawili ya kushambulia kwa makusudi na uhalifu wa kutumia silaha, na dhamana yake ni Tsh milioni 469. Ralph baada ya kupigwa risasi alipatiwa msaada na wasamaria wema na mpaka sasa yupo hospitali anaendelea kutibiwa.
 
Nilijua tu atakuwa kijana mwenye asili ya kiafrika na kweli...! Huyu babu aadhibiwe vikali!
 
Nilijua tu atakuwa kijana mwenye asili ya kiafrika na kweli...! Huyu babu aadhibiwe vikali!
Mimi ndiyo nikiona mtu ngozi nyeusi anawanyenyekea hao ngozi za kugeuzwa wazungu sijui waarabu huwa namuona punguani.

Hao mbwa koko wana chuki kiasi wanatamani humu duniani mtu mweusi asingekuwepo
 
Mungu anisamehe ila Mzee hiyo sura yake tu inaonesha ni katili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…