Afrika hatuna jeuri za kujiita ally wala nini, ukizingatia hata makombora tunanunua kutoka kwao, angalia nchi zenye uwezo wa kutunisha misuli, kwa mfano Iran na Korea Kaskazni, wao wana viwanda vya kujitengezea makombora. Sisi tunaagiza kila aina ya zana za kivita. Hamna chochote kinachouniwa huku Afrika, hata simu anayotumia Magufuli wenu kule ikulu imeagizwa kutoka kwa hawa jamaa, mifumo yote ya mawasiliano, anachosema hata kwa siri anatumia vyombo vyao....hehehe
Vifaa tunavyonunua kutoka kwao huwa vya kutishia nyau wenzetu Afrika lakini sio wale, au unajidanganya hizo ndege chache za JWTZ zinaweza kumkuna sehemu yoyote Mmarekani akiamua kutembeza kibano Tanzania. Yaani ndege moja ya kisasa ya Marekani imetosha kuwapiga kichapo jeshi lenu na mshindwe kuidungua, itakua inashusha mabomu kwenu na kurudi kwenye aircraft carrier kuongeza mafuta na makombora na kurudi kuendeleza kichapo.
Kwa hivyo kupiga makelele eti hatutaki waweke hayo mavitu yao kwetu ni ujuha, wayalete tu.....hizo drones.