joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 17,420
- 35,765
Tatizo si NANI, SERIKALI NDIO IPO JUU YA KILA KITU NA WANAAMINI KATIKA UHURU WA KUJIELEZA na IPO KTK KATIBA YAO,kama akitokea mtu yoyote au taasisi yoyote ,ikitaka kuminya UHURU WA MTU WA KUJIELEZA,KAMA SERIKALI LAZIMA MCHUKUE HATUA,sababu US wao wanaamini katik uhuru wa kujieleza,lkn kwa Trump mbona wapo kimya.Uhuru wa kujieleza wa mtu aliye madarakani umeminywa na nani?
HAWA NAO SIWASEME TUUU JUUU YA UJIO NAMBA 666, KAMA UFUNUO WA YOHANA UNAVYOSEMA?? ASOMAYE NA AFAHAMU. TULIOOKOKA TUKAE TAYARI, YALIYONENWA NA VINYWA VYA MANABII YANAENDA KUTIMIA. UNYAKUO WAWATAKATIFU NI SAA YOYOTE KUANZIA SASA. MWENYE DHAMBI JITAKASE HARAKA SAANA YESU YUAJA TENA KUCHUKUA WATAKATIFU.Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo ameandika "Kuna matokeo ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo, tunaweka vizuizi vya visa kwa wale wanaohusika na uvurugaji wa uchaguzi nchini Tanzania. Tunabaki kujitolea kufanya kazi pamoja kuendeleza demokrasia na ustawi wa pande zote kwa nchi zetu zote mbili."
View attachment 1681412
Soma pia: Visa Restrictions on Tanzanians for Undermining the Democratic Process and Human Rights - United States Department of State
______________________________________
Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo vya vya kuingia nchini humo maafisa wa Tanzania ambao nchi hiyo inawatuhumu kwa kile wanachokitaja kuwa kuharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka 2020.
Maofisa hao wanatajwa kuhusika kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuminya utekelezaji wa demokrasia.
Hata hivyo taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijabainisha ni viongozi gani hasa kutoka Tanzania waliowekewa vikwazo vya kuingia Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, Waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia wanadai kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo pamoja na uvunjifu wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi.
Marekani inasema kuzimwa ama kuzimika kwa mitandao, kuminywa kwa waandishi wa habari na nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Polisi kunafanya uchaguzi huo kutokua huru na wa haki.
Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa sababu mbalimbali na wengine kukamatwa.
Tume ya uchaguzi nchini humo na hata Serikali kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Palamagamba Kabudi ilieleza kwamba uchaguzi ulikua huru na wa haki.
Marekani inasema pamoja na hatua hii iliyochukua dhidi ya maafisa wa Tanzania, inaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya hoja hiyo, huku ikisema haitasita kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wanaominya demokrasia na kuvunja haki za binadamu.
''Tunaitaka Tanzania, kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuvuruga uchaguzi, kufanya vurugu na kuleta vitisho'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Juhudi za kumpata msemaji wa serikali ya Tanzania kuzungumzia suala hilo mpaka sasa hazijazaa matunda, na tutaendelea kuwatafuta kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo
Haya ni moja ya maamuzi ya mwisho ya utawala wa rais Donald Trump ambaye amebakiza saa chache kuachia mamlaka ya urais. Mpaka sasa haijafahamika iwapo utawala wa rais mpya Joe Biden kama utatekeleza maamuzi hayo. Tayari ofisi ya Biden imetangaza kuwa itatengua sera kadhaa za Trump mara tu baada ya kuingia ofisini kesho.
BBC.
Huyu mzee mbona simwelewi, hebu wafungue Twitter za Trump. Nchi yao haina uhuru wa kujieleza
Kada, hutaki uchaguzi huru ?!Utababaishwa wewe unayewaamini kama mabwana zako
Hicho kibano kwa Tanzania kinafanywa na serikali ya huyo huyo Trump!!! The Americans have no moral authority to preach about democracy in the world when we have witnessed massive voter suppression in their just concluded elections!!
Hawa wamarekani wanaposema uchaguzi wao Biden hakushinda kihalali, maana yao ni kwamba kwa kuwa wamarekani wasio weupe [ weusi na Latinos] wengi walijitokeza kupiga kura na wagombea wao kushinda hivyo uchaguzi haukuwa halali!!! Weusi na Latinos wameungana kupiga vita mbinu zao za voter suppression na sasa wanaona power inawaponyoka na ndio maana unasikia hizo vurugu za WHITE SUPREMACISTS!!! Hawa weupe wanasahau kuwa marekani ni nchini ya wakuja [ immigrants] na hata wao ni wa kuja pia!!! Wenye asili ya nchi hiyo wamewekwa kwenye RESERVES!!!!!
Sidhani kama hao Marekani hawafikirii hicho unachofikiria, hapa ni swala la ishara zaidi kuliko hata adhabu yenyewe...labda wangeweza kufanya hatua nyingine ikawa inawaumiza hata wasiohusika.Ahaaa... Yani mtoto wa Mahera apate tabu kisa baba kazuiwa kwenda USA?
Kwani hapa nyumbani maisha hakuna?
Hivi kwanza katika wale viongozi wa juu wa NEC kuna mwenye shida kwenda USA? kufanya nini?
Eti wasije USA, ni mbinguni kule?
Tatizo si nani, SERIKALI NDIO IPO JUU YA KILA KITU NA WANAAMINI KATIKA UHURU WA KUJIELEZA na IPO KTK KATIBA YAO,kama akitokea mtu yoyote au taasisi yoyote ,ikitaka kuminya UHURU WA MTU WA KUJIELEZA,KAMA SERIKALI LAZIMA MCHUKUE HATUA,sababu US wao wanaamini katik uhuru wa kujieleza,lkn kwa Trump mbona wapo kimya.
KWA HIKI WALICHOMFANYIA TRUMP MANAKE WAMEICHEZEA KATIBA,KWA KUMINYA UHURU WA KUJIELEZA.
Simjui,je huyo aliye mfungia yupo JUU YA KATIBA?Nani wamemfanyia nini Trump ?
Tatizo si nani, SERIKALI NDIO IPO JUU YA KILA KITU NA WANAAMINI KATIKA UHURU WA KUJIELEZA na IPO KTK KATIBA YAO,kama akitokea mtu yoyote au taasisi yoyote ,ikitaka kuminya UHURU WA MTU WA KUJIELEZA,KAMA SERIKALI LAZIMA MCHUKUE HATUA,sababu US wao wanaamini katik uhuru wa kujieleza,lkn kwa Trump mbona wapo kimya.
KWA HIKI WALICHOMFANYIA TRUMP MANAKE WAMEICHEZEA KATIBA,KWA KUMINYA UHURU WA KUJIELEZA.
Zipo za aina nyingi sana, mfano kuna demokrasia ya vyama Vingi na demokrasia ya vyama viwili kama Ilivyo kwao, vipi sisi leo tukianza kuwalazimisha wawe na utitiri wa vyama vya siasa kama sisi?Kuna demokrasia za aina ngapi😂😂 tunakuwa vichekesho
KATIBA YA US IMECHEZEWA AU HIJACHEZEWA?Wamarekani wao hawaamini serikali yao ipo juu ya kila kitu ndio maana kila siku wanaifungulia kesi na kuishinda
Ulitaka serikali ya Marekani imsaidiaje Trump?
Nani katika serikali ya Marekani anatakiwa ahakikishe uhuru wa kujieleza wa wananchi wote (pamoja na wa Rais) hauminyiwi?
[emoji23][emoji23][emoji23]Basi tuendelee kutafuta ugali hayo mengine tuwaachie wao wenyewe waonyaneSidhani kama hao Marekani hawafikirii hicho unachofikiria, hapa ni swala la ishara zaidi kuliko hata adhabu yenyewe...labda wangeweza kufanya hatua nyingine ikawa inawaumiza hata wasiohusika....
Simjui,je huyo aliye mfungia yupo JUU YA KATIBA?
MANAKE KATIBA MMEMPA KILA MTU UHURU WA KUJIELEZA.