Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Watu wanakufa sasa kwa njaa Gaza na kuna malori ya misaada kwa mamia kwenye mipaka ya Gaza ambayo yameshindwa kuingia huko kikwazo ikiwa ni ruhusa ya Israel.
Marekani kwa kujionesha kuwahurumia wanaokaribia kufa njaa imekuwa ikidondosha misaada michache ya michache ya chakula na sasa imesema inatarajia kujenga bandari ili kurahisisha ufikishwaji wa misaada huko.
Bandari hiyo inayotajwa kuwa ni ya muda haitaweza kuanza kazi mpaka baada ya miezi miwili pale itakapokamilika.
Kuna umuhimu gani wa kujenga bandari kupeleka misaada hapo baadae badala ya kuilazimisha Israel ifungue mipaka na kupitisha malori ya misaada ambayo yamekuwa kwenye foleni ya kusubiri muda mrefu.