Iyerdoi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2012
- 2,717
- 3,895
Tatizo ni uporaji wa chakula hicho unaofanywa na kundi la HAMAS. Kumbuka kwamba HAMAS sio walengwa wa misaada hiyo ila wao kama wapiganaji dhidi ya IDF wanatumia ubabe wa kunyang'anya na kuteka malori yanayosafirisha chakula na vifaa tiba hivyo. Ukileta fyoko-fyoko wanakulamba kichwa chap na kama Dereva na Wahudumu ni watu chini ya wa UN, HAMAS fasta wanasema ni kazi ya IDF.Watu wanakufa sasa kwa njaa Gaza na kuna malori ya misaada kwa mamia kwenye mipaka ya Gaza ambayo yameshindwa kuingia huko kikwazo ikiwa ni ruhusa ya Israel.
Marekani kwa kujionesha kuwahurumia wanaokaribia kufa njaa imekuwa ikidondosha misaada michache ya michache ya chakula na sasa imesema inatarajia kujenga bandari ili kurahisisha ufikishwaji wa misaada huko.
Bandari hiyo inayotajwa kuwa ni ya muda haitaweza kuanza kazi mpaka baada ya miezi miwili pale itakapokamilika.
Kuna umuhimu gani wa kujenga bandari kupeleka misaada hapo baadae badala ya kuilazimisha Israel ifungue mipaka na kupitisha malori ya misaada ambayo yamekuwa kwenye foleni ya kusubiri muda mrefu.