Marekani kupigana vita na China 2025, Jenerali wa Marekani bw. Mike

Ni kweli, hapo kuna ujumbe jamaa ameufikisha. Wanadiplomasia wa China lazima wauchambue ujumbe una maana gani huu.
 
Ni kweli China itapa vizuizi vikali katika hiyo OP yake anayo taka kufanya hapo Taiwan.

Alichofanya kweli ni kazi yake, lakini je madhara ya ujumbe wake kuvuja ni yapi kwa taifa lake katika diplomasia ya haya mataifa mawili? Au madhara hakuna kwa huo ujumbe?
 
Ndo maana Japan anajenga Base karibu na Taiwan
Japan nao ni kama hawapo mbali na huu mgogoro kwa kuwa wanafahamu fika pia nao wana mgogoro na China wa ardhi.
 
Tusubiri tuone mkuu, Je ni kwamba maafisa wa Jeshi la Marekani hawafahamu madhara ya kuanzisha vita na taifa la kinyuklia au wameamua kupuuzia hilo?
 
Sitaki kuamini kama US hajipangi ipasavyo kwa Taiwan. Na hii itakuwa tofauti kabisa na kule kinachotokea Ukraine. Hii huenda ikawa ni piga nikupige, China ni lazima akubali ardhi yake pia imwage damu. Lazima vyuma vitue Hong Kong.

Hiki ni kipindi ambacho ambacho Taiwan atajisuka sana kiulinzi eneo la anga na majini. Marekani hanaga show mbovu kwenye masuala ya hujuma kama hizi.
 
Ndo maana Japan anajenga Base karibu na Taiwan
Haya mataifa makubwa ya kikomunisti yana tabia za kumega ardhi, nchi ndogondogo zinajihami mno dhidi yao.

Hapo Taiwan kuna siku kitawaka tu. Na hii kwa namna zote Taiwan ameshajiandaa, usipojiandaa kwa kutafuta washirika wa kuwa karibu yako kuna siku watakuvamia na watachukua eneo lako.
 
Ni kweli kabisa kuwa China ana wakati mgumu kuhusu swala la Taiwan, lakini je tiafa la marekani hali fahamu madhara ya kuanzisha vita na taifa la kinyuklia?
Mimi kwangu mbinu ya wao kuwauzia silaha Taiwan ni bora zaidi kuliko wao kushiriki hio Vita kwa taifa la kinyuklia wewe unaonaje?
 
Swala la China na mataifa yaliyo na mgogoro na yeye wa kimipaka haina uhusiano na ukomunisti wao maana hii ni historia ya miaka mingi sana toka kipindi cha falme zao na kipindi cha ukoloni.
 
1. Russia alisema atakayemsaidia Ukraine atakutana na mkono mzito, kila leo misaada inaenda Ukraine. Kwanini Russia asimchape US?

2. Biden alisema Russia akiivamia tu Ukraine wanalipua bomba la mafuta, na ni kweli US aliripua hilo bomba.

US tusimchukulie wa mchezo mchezo. Mtu ambae kila kona ya dunia yupo ameweka base, na takribani miaka 50 sasa kila mwaka ana vita na operations kibao anazifanya, jamaa yupo vizuri.

Sasa hivi amekiwasha huko Ukraine. Na bado vile vile alikuwa tayari kukiwasha Taiwan dhidi ya China. Nitajie mjinga gani hapa duniani anaweza akawa na guts kama hizi?.

Leo hii Iran, S.Korea pawake moto, unafikiri Russia anaweza kunyanyua miguu yake kuwasaidia hao? Lakini US anaweza akapambana huko Ukraine, Taiwan pia akapeleka misaada, na bado uko Korea au Japan kukinuka akapeleka misaada na majeshi kupambana.

Nenda google, bajeti ya ulinzi ya US, chukua bajeti za ulinzi z UK German France, China, Russia, Canada n.k zijumrishe kwa pamoja na hawafiki nusu ya bajeti ya ulinzi jamaa.
 
Hio bajeti sio kwa ajili ya ndani nchini mwake ni pamoja na kwenye base zake

Mfano wewe bajeti yako ya malezi ni elfu 9 na una mtoto watoto watatu ila mwenzio akawa na bajeti ya elfu 4 kwa mtoto mmoja

Nani atakuwa vizuri hapo kwenye kumtunza mtoto?
 
Haya ndio yale ya mtoto wa Museven sasa Africa tunaonekana ovyoo , ila hawa dunia ya kwanza vipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…