Nunua Toka UK
JF-Expert Member
- Apr 17, 2023
- 303
- 587
Tukio la kibaguzi lililorekodiwa katika uwanja wa michezo wa Minnesota limezua hasira na kuzua mzozo usiotarajiwa baada ya mwanamke anayeitwa Shiloh Hendrix (kwenye picha) kurekodiwa akielekeza maneno ya ubaguzi wa rangi kwa mtoto mweusi mwenye umri wa miaka mitano, ambaye inasemekana ana autism - na baadaye kuchangisha mamia ya maelfu ya dola katika “GoFundMe” kampeni.
Video hiyo ya mtandaoni, iliyorekodiwa katika sehemu ya michezo ya Soldiers Field huko Rochester - Marekani, inaonyesha mwanamke huyo mwenye tatoo akiwa amemshika mtoto wake mchanga huku akikabiliwa na mwanamume anayemshtumu kwa kumwita mtoto mweusi mwenye umri wa miaka 5 'N-word.'
Analipo kabiliwa na mwanaume huyo. Shiloh hakanushi shtaka hilo bali aliendelea kurudia neno niga.
Makabiliano hayo yanaripotiwa kuwa yalianza baada ya kudai mtoto huyo mweusi alichukua toy kutoka kwa mfuko wa nepi wa mwanawe.
Lakini katika hali ya kushangaza, Shiloh alianzisha kampeni ya kuchangiwa katika njia ya mtandao, akidai kuwa video hiyo inayonwonyesha akitoa maneno ya kibaguzi, ilimsababishia yeye na familia kutishiwa.
Kampeni yake iliyopata umaarufu kwa kasi imekusanya zaidi ya $480,000 na lengo la $1 milioni.
Soma zaidi hapa: Shock twist after mom hurls vile slur to 5-year-old on a playground