Ile Samson Option - Wikipedia wanayosema watafanya wakitishiwa uwepo wao hata Iran wanayo.Kivipi?
Ungeuonyesha huo uwezo wa Iran kuigeuza Israel kuwa majivu angalau ungejitendea haki. Ni ndoto ya miongo mingi ya Iran kuifuta Israel, je ni kipi imekifanya hadi sasa ambacho kina angalau hizo dalili?
Unaweza kunikumbusha ni wakati gani Israel aliyaongea hayo? Na ni wakati gani Israel alieahi kusema anayo na ni lini Iran alisema anayo?Ile Samson Option - Wikipedia wanayosema watafanya wakitishiwa uwepo wao hata Iran wanayo.
Sio kwa taifa kama Iran mzee!Nadhani hapa hukupasoma ukapaelewa,Israel anaweza akafanya uhuni kupitia hizi devices akajeruhi watu bila kujali siha zao kama ni wananchi wa kawaida au wanajeshi wakati taifa likiwa ktk taharuki ya tukio hili aka-attack vibaya Muajemi akagaragara mavumbini.
Vita ni mbinu na Zayuni kwa upande huu ameweza.
Madhara ya kuhudhuria Masjid na kuacha kufanya swala ndiyo haya, unajikuta unaiona dunia katika uhalisia wake ma kuuongea ukweli kama ulivyo ingawa ni mchungu.
Usitoke kwenye moody, leo umekuja vizuri, endelea kutiririkaAya ya kwanza kabisa Iko wazi:
"Hili si suala la ushabiki wala kiimani."
Kumbe yako na Masjid au dini yanatokea wapi?
Hivi unaweza kuonyesha popote nilipowahi kuandika au kushabikia dini yoyote?
"Kwamba wewe ni mfia dini usidhani ni kila mtu!"
😂😂😂😂Mkuu alikuwa nayo nafasi hiyo angekomaa sasa na kabla ya kushambuliwa.
Tatizo kubwa ametulia aguswe kwanza Ili ajibu.
😂😂😂😂ogopa sana watu wako million 9 ambao ni wananchi pamoja na Jeshi humo humo lakini wana nguvu sawa na China,Russia,America pia
Usitoke kwenye moody, leo umekuja vizuri, endelea kutiririka
Kwani wamesharudi kwa Mungu? Kama bado inamaana kuna uwezekano akabutuliwa na Muajemi, sio?Tukirudi kwenye Imani kwa maana ya maandiko,ni kweli MUNGU aliwapa mapigo mawili makubwa iwapo wataenda kinyume naye, Magonjwa(Tauni) pamoja na kuwekwa mikononi mwa Adui,lakini wakirejea kwa MUNGU basi hakuna Taifa litaweza kuwashinda kivita,akili na uwezo wa juu wa kupambanua mambo.
Iran bado hajapata sababu ya kufanya hivi.
Au mkongwe unaona ipo sababu ya Iran kuingia kwenye vita moja kwa moja dhidi ya Israel?
Mpuuzie tu mkongwe, huyo mtu kwake yeye kila mtu anayeikosoa Israel ni Muislam!Mkuu, kulikoni nitoke kwenye moody? Sijawahi wala haiwezi kutokea. Hili nalo kifua mbele nikikuomba uthibitisho, hauta upata.
Nimekuomba kwa dhati yàngu kunionyesha andiko langu moja tu lolote nikishabikia dini ndani au nje ya JF.
"Ikikupendeza tafadhali."
Kila niki search unakuja ule uzi wa "Kula tunda kimasihara"Mkuu, kulikoni nitoke kwenye moody? Sijawahi wala haiwezi kutokea. Hili nalo kifua mbele nikikuomba uthibitisho, hauta upata.
Nimekuomba kwa dhati yàngu kunionyesha andiko langu moja tu lolote nikishabikia dini ndani au nje ya JF.
"Ikikupendeza tafadhali."
Mkongwe, ukifanya hivi na mimi itabidi nije na screenshot inayoonesha wanachokisema Persians kuwa nini watafanya Israel ikileta ubwege.
USA na Iran hawawezi kuingia kwenye vitaIran bado hajapata sababu ya kufanya hivi.
Au mkongwe unaona ipo sababu ya Iran kuingia kwenye vita moja kwa moja dhidi ya Israel?
Muajemi nae yupo vizuri ana uzoefu mkubwa sana kwenye mambo ya vitaMkuu unaona hapa:
View attachment 3120547
Unaona pana salama hapo?
Ukayaona na haya:
"Ya kwamba watakusaka pamoja kukuondoa wao duniani bila kujali muda wala gharama. Ya kuwa kwenye hilo tangia mataifa yao yamekuwapo kwenye hilo hawajawahi kushindwa!
Yale yale ya akina Osama bin Laden, Mula Omari, General Farrah Aideed, Saddam Hussein, Muamar Gaddafi nk."
Mkuu Iran alibakiwa na option #2 pekee Kwa mawazo yangu.
Kila niki search unakuja ule uzi wa "Kula tunda kimasihara"
Wewe ni mtu ambaye huamini ktk mabadiliko.. Bwana mdogo amini usiamini mambo hubadilika. Kukalriri na kutojiamini ni ujinga kama ujinga mwingineHili si suala la ushabiki wala kiimani. Uungwana siku zote ni kujitendea haki mwenyewe kwa kuukabili ukweli hata kama ni mchungu.
Sote ni wafu watarajiwa na kwa mola tutarejea. Hata ipo tofauti linapokuja suala la kurejeshwa na binadamu wengine ndiyo maana kelele zinapigwa.
Rejea "Operation Plasma" ya MOSSAD kumhusu Mohamed al-Mabhouh jamanda wa HAMMAS, aliyeuwawa Dubai 19 January 2010:
The Dubai Operation: Mossad, Murderer & Mayhem in the Desert
Hiyo ni case moja yenye kufanana na nyingi za namna hiyo zenye kuwahusisha Israel au Marekani.
Pattern ni hiyo hiyo kote, kila mmoja wa wawili hao akiguswa popote. Si vigumu kutambua iko kama sheria isiyo rasmi (rule of the thumb) kuwa:
"Ukimwua au kujaribu kumwua mwisrael au mmarekani au ukiyatishia mataifa yao au watu wao popote; tokea muda huo, tambua wewe ni mfu unayetembea, na watakuondoa."
Ya kwamba watakusaka pamoja kukuondoa wao duniani bila kujali muda wala gharama. Ya kuwa kwenye hilo tangia mataifa yao yamekuwapo kwenye hilo hawajawahi kushindwa!
Yale yale ya akina Osama bin Laden, Mula Omari, General Farrah Aideed, Saddam Hussein, Muamar Gaddafi nk.
Angetoboa Haniyeh, Nasrallah au Sinwar? Watatoboa Ali Kamenei, yule wa Houthi, au nani?
Kwa sababu mataifa wawili hawa kwenye haya ya kutishiana nyau ni wamoja, ziko namna mbili tu za kushughulika nao kwa mafanikio:
1. Kusalimu amri kama UAE na Saudi Arabia yaishe kama unataka kuishi. Au:
2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.
Hili la pili ndipo alipokosea Hezbollah na ndipo anapokosea Iran kwani hawako tayari kusalimu amri. Ni wazi wamekuwa tayari kufa lakini sasa wame pause na sasa cha mbwa koko kitawakuta.
Kwamba watapigwa surprise? Kwa hakika lile la aina ya "pagers na walkie talkies" si muda mrefu yatawakuta Iran.
Kumbe kipi kipo salama nao chenye technolojia yoyote ya mmarekani? Ni TVs, computers, magari au gadgets zozote zenye chipsets zozote zenye lolote na wamarekani?
Kutowatokea wote wawili bila kukoma (in hot pursuit) na kuwapelekea moto vilivyo sasa yatamkuta Iran kama ya Hezbollah asishangae hatakuwa na uwezo hata kurusha ngumi.
Alipoletewa moto rasmi Hezbollah, maelfu ya wapiganaji wake walikuwa mahututi hosipitalini vipofu, mikono hamna, miguu hamna, matumbo yamefumuliwa, nk.
Kwamba Hezbollah alianzishiwa vita rasmi Hezbollah, makamanda wote wakuu marehemu na hawezi kutumia vifaa vya mawasiliano.
Haihitaji macho ya kinabii kumwona Iran naye yulee ... kama Hezbollah kama kuku bandani akisubiria zamu yake ya kuchinjwa.
"Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu .