Marekani na Uingereza wafanya mashambulizi dhidi ya Kikundi cha Houthi nchini Yemen

Sio rahisi wenye akili kisoda kuelewa
 
Wayemeni wahuni sana wanawayumi Drone za dollar 500 za kutumia mafuta ya taa ili zipigwe na missile za Kimarekani za Dollar million mpoja.

Hiyo imewatia sana hasira Wamerekani na Waingereza.

Maana kila wakiitunguwa moja wanaona nyingine inakuja, kumbe chambo kile makussudi kiwatie hasarara tu.

Hasira zao wakaenda kuwapiga Yemen.

Hii vita Wamarekani, Mazayuni na NATO wote wanachezewa kama watoto wadogo.
 
Yaani Marekani aliyetuma amri ya Wayemen wapigwe alikuwa hospital anapimwa tezi dume.

Siyo utani jamani, nimecheka mpaka wajuku wananishangaa hapa.

Si mnaufahamu mkao wa kupimwa tezi dume?
 
Hakuna cha kubishana kuhusu Marekani. Unaweza kuainisha ushindi unavyotaka na kudai kwamba Marekani haina uwezo wa kishinda vita - isipokuwa kama ikitumia nyuklia! Sina cha kuongeza.

Tuendelee kushuhudia Marekani ikishindwa tena katika vita hii - kama kweli itashindwa.
 
Tunaendelea kubishana kwa hoja tu mwisho tutaelewana

Anaepigana hapo sio marekani ni marekani kwaushirikiano na Uingereza

Marekani vita pekee aloenda yeye kama yeye ukitoa ile alotumia nyuklia kule japan ni ile ya somalia na vietnam na kote alikimbizwa

Ila acha tuone mwisho wa hii coalition itakuaje ila sioni wakiipiga yemen kama walishindwa mwaka 2014 sioni kama watakua na jipya mara hii
 
Ivi ni kwann USA na UK wasipitie hapo spain kuingia israel mpaka wazunguke kuingilia huku redsea?
FaizaFoxy
 
Sawa. Mimi sikisii. Nina uhakika Marekani itatimiza malengo yake katika vita hii. Halafu kumbuka umbali kati ya Marekani na Yemen ni zaidi ya km 10,000.

Kule Marekani raia wala hata hawana habari kama nchi yao iko vitani na nchi gani vile?…. Lakini Yemen watu wanahaha kukwepa mizinga ya US. Kila M’Yemeni anaijua Marekani.
 
Turkey ni moja kati ya nchi zenye jeshi kubwa na lenye nguvu na vifaa vya kisasa
Ila ni ndumilakuwili
Turkey ni mamluki na mnafiki
Turkey angekuwa na misimamo thabiti kama Iran , mashariki ya kati pangetulia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…