Marekani na Uingereza wafanya mashambulizi dhidi ya Kikundi cha Houthi nchini Yemen

Marekani na Uingereza wafanya mashambulizi dhidi ya Kikundi cha Houthi nchini Yemen

Kitu geopolitics. Alliances. Mnagawana uwajibikaji. Sio unaonekana mkorofi au kiherehere peke yako.

Marekani ina uwezo mkubwa sana kiuchumi, kiteknolojia na kijeshi lakini inatafuta uhalali wa kuambatana na wengine ili kuhalalisha mashambulizi dhidi ya “adui wa wote” (common enemy).
Sio rahisi wenye akili kisoda kuelewa
 
Wayemeni wahuni sana wanawayumi Drone za dollar 500 za kutumia mafuta ya taa ili zipigwe na missile za Kimarekani za Dollar million mpoja.

Hiyo imewatia sana hasira Wamerekani na Waingereza.

Maana kila wakiitunguwa moja wanaona nyingine inakuja, kumbe chambo kile makussudi kiwatie hasarara tu.

Hasira zao wakaenda kuwapiga Yemen.

Hii vita Wamarekani, Mazayuni na NATO wote wanachezewa kama watoto wadogo.
 
Yaani Marekani aliyetuma amri ya Wayemen wapigwe alikuwa hospital anapimwa tezi dume.

Siyo utani jamani, nimecheka mpaka wajuku wananishangaa hapa.

Si mnaufahamu mkao wa kupimwa tezi dume?
 
Hakuna cha kommon enemy Americant anajijua licha yakua na yote hayo ila kwenye vita ya kweli hua hatoboi

Nandio maana katika historia ya Americant hakuna vita aloenda mwenyewe akashinda ukiachana na ile ya Japan tena alishinda baada ya kutumia nyuklia

Americant bila washirika na bila nyuklia hajawahi kushinda vita yeyote na popote pale duniani tokea kujuulikana kwake

Kiufupi Americant inaujua udhaifu wake isipokua na nyuklia ama isipokua na wakuongozana nae

Bisha kwa fact
Hakuna cha kubishana kuhusu Marekani. Unaweza kuainisha ushindi unavyotaka na kudai kwamba Marekani haina uwezo wa kishinda vita - isipokuwa kama ikitumia nyuklia! Sina cha kuongeza.

Tuendelee kushuhudia Marekani ikishindwa tena katika vita hii - kama kweli itashindwa.
 
Tunaendelea kubishana kwa hoja tu mwisho tutaelewana

Anaepigana hapo sio marekani ni marekani kwaushirikiano na Uingereza

Marekani vita pekee aloenda yeye kama yeye ukitoa ile alotumia nyuklia kule japan ni ile ya somalia na vietnam na kote alikimbizwa

Ila acha tuone mwisho wa hii coalition itakuaje ila sioni wakiipiga yemen kama walishindwa mwaka 2014 sioni kama watakua na jipya mara hii
 
⚡️Yemen: Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa nchini #Yemen, Mahdi Al-Mashat:

Uchokozi usio na msingi wa Marekani-Kizayuni-Waingereza ni ukiukaji wa sheria zote na watalipa gharama.

Tutaendelea kuzuia meli za Israel au zile zinazoelekea Palestina inayokaliwa kwa mabavu, bila kujali uchokozi dhidi ya watu wa Yemeni.

Tunawawajibisha Wamarekani na Waingereza kwa ajili ya uwekaji kijeshi wa meli za kimataifa, na tutathibitisha kwamba Yemen ni "makaburi ya wavamizi"
Ivi ni kwann USA na UK wasipitie hapo spain kuingia israel mpaka wazunguke kuingilia huku redsea?
FaizaFoxy
 
Tunaendelea kubishana kwa hoja tu mwisho tutaelewana

Anaepigana hapo sio marekani ni marekani kwaushirikiano na Uingereza

Marekani vita pekee aloenda yeye kama yeye ukitoa ile alotumia nyuklia kule japan ni ile ya somalia na vietnam na kote alikimbizwa

Ila acha tuone mwisho wa hii coalition itakuaje ila sioni wakiipiga yemen kama walishindwa mwaka 2014 sioni kama watakua na jipya mara hii
Sawa. Mimi sikisii. Nina uhakika Marekani itatimiza malengo yake katika vita hii. Halafu kumbuka umbali kati ya Marekani na Yemen ni zaidi ya km 10,000.

Kule Marekani raia wala hata hawana habari kama nchi yao iko vitani na nchi gani vile?…. Lakini Yemen watu wanahaha kukwepa mizinga ya US. Kila M’Yemeni anaijua Marekani.
 
Turkey ni moja kati ya nchi zenye jeshi kubwa na lenye nguvu na vifaa vya kisasa
Ila ni ndumilakuwili
Turkey ni mamluki na mnafiki
Turkey angekuwa na misimamo thabiti kama Iran , mashariki ya kati pangetulia sana
 
Back
Top Bottom