Na hiyo miezi Sita ni kupewa majibu kama umekubaliwa au lah. Tetesi = Marekani wamechukizwa na kitendo cha baadhi ya viongozi wa Africa walio hudhuria kwenye kikao na Put-OUT.
Warudishieni kikumbo na wao kuja Serengeti ,Kilimanjaro, Zanzibar etc wasubiri visa miezi sita.
Tuone kama hawajapunguza jeuri.
Miaka kadhaa nyuma, kuna siku dada yangu mdogo alikuwa anataka kutoka Tanzania kuja likizo kutusalimia ndugu zake US. Ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza kuja US.
Alivyofika ubalozi wa US kuomba visa, yule Counselor anayetoa visa akawa anamuuliza maswali invasive. Yani yale ya kuhakiki kama atarudi, ana kazi, na mengine mengi ya kizushi zaidi waziwazi kabisaaa.
Yule dada akili zake anavyozijua mwenyewe, alivyoona maswali ya kijinga yanazidi, akamuwakia yule Counselor.
Akamwambia I am offended by your presumptuos and invasive questions. Naghairi safari sasa hivi, nipe passport yangu. Huko Marekani nakwenda kusalimia tu ndugu zangu, si safari ya lazima sana.
Yule Counselor akastuka sana, inaonekana ilikuwa kitu cha ajabu sana kupata Mtanzania anayeweza kuji assert hivyo.
Hapo hapo yule Counselor akaanza kumuomba msamaha yule dada yangu mdogo. Akamgongea visa.
Kuanzia siku hiyo, yule dada akawa anakuja na kutoka Marekani anavyotaka. Mpaka sasa hivi kachoka mwenyewe safari za likizo Marekani.
Labda Tanzania tunatakiwa kuji assert zaidi kama alivyofanya huyo dada yangu mdogo, kufanya some sort of reciprocity.
Tatizo ni kwamba, reciprocity works among equals. Sisi kama tunahitaji sana hela za watalii wa Kimarekani, kuwalazimisha wangojee miezi sita kuja kutalii wataghairi na kwenda sehemu nyingine.
Na sisi Tanzania tunaona hatuwezi ku afford kukosa hela za watalii wa Kimarekani.
Inabidi tuwakubalie wachukue visa on arrival Tanzania.