Marekani waongeza muda wa kupata visa ya Marekani kwa watanzania hadi kuwa miezi Sita

Marekani waongeza muda wa kupata visa ya Marekani kwa watanzania hadi kuwa miezi Sita

Kwa mujibu wa Ernest B. Makulilo wa EBM SCHOLARS kwa sasa muda wa kuprocess visa ya kwenda Marekani kwa raia wa Tanzania ni miezi Sita.

Kwa lugha nyepesi ni ukiomba visa ya kwenda Marekani leo utapokea majibu ya maombi yako baada ya miezi Sita (Februari 2024)

View attachment 2706482
watakuwa wamemuona majaliwa urusi wakaamua kuweka vikwazo. tunachotakiwa kufanya sasa ni kujiunga mazima na russia ili wachoke kabisa.
 
Halafu ukimuona basi, hata huwezi kumfikiria huyu anaweza kufanya hivyo.

Wale ma Counselor ubalozini tatizo lao kubwa ni watu wanaotaka kuzamia kimoja Marekani.

Na huyu dada alikuwa anajiamini kabisa kwamba yeye anakuja likizo kusalimia wiki chache, kisha anarudi nyumbani, na nyumbani ana kazi yake nzuri inamngoja, ana strong family ties, in fact angetaka kuishi Marekani mimi ningemfanyia mpango wa green card ya familia, alikuwa hataki mwenyewe anasema haitakiwi wote tukae huku Marekani, familia inahitaji watoto Tanzania pia, sasa akaona maswali yote haya invasive ya nini? Akawa anataka kughairi safari.

Mpaka leo nikimkumbushia na kumdadisi alifikiria nini kusema vile anacheka sana.

Hapo nilijifunza kitu kikubwa sana kuhusu human dignity.

Kumbe wale ma Counselor Wamarekani nao wanajua human dignity ni nini, na kuna maswali mengine yakivuka mpaka ukawarudisha kwenye mstari kama una principle wanakuelewa mpaka kukuomba msamaha wenyewe.

Msijaribu kugeza lakini, kila mtu na "nyota" yake [emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Mkuu unaamini katika nyota? Ila kutokana na hzo emoji za kucheka,labda you are just playing! But am curious.
 
Explain kk!
Nikiandika nyota, maana yake ni kitu ninachokisema mimi.

Nikiweka kwenye quotations "nyota" maana yake nanukuu kauli za watu, dhana sijaikubali binafsi, kitu so called, nimekiweka hapo kufikisha ujumbe lakini mimi si changu, sijakikubaki hivyo, naripoti, lakini, ni njia rahisi ya kufikisha ujumbe.
 
Sijatoka bure leo. Najifunza sana almost katika kila andiko lako. Shukrani.
 
Warudishieni kikumbo na wao kuja Serengeti ,Kilimanjaro, Zanzibar etc wasubiri visa miezi sita.

Tuone kama hawajapunguza jeuri.

Miaka kadhaa nyuma, kuna siku dada yangu mdogo alikuwa anataka kutoka Tanzania kuja likizo kutusalimia ndugu zake US. Ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza kuja US.

Alivyofika ubalozi wa US kuomba visa, yule Counselor anayetoa visa akawa anamuuliza maswali invasive. Yani yale ya kuhakiki kama atarudi, ana kazi, na mengine mengi ya kizushi zaidi waziwazi kabisaaa.

Yule dada akili zake anavyozijua mwenyewe, alivyoona maswali ya kijinga yanazidi, akamuwakia yule Counselor.

Akamwambia I am offended by your presumptuos and invasive questions. Naghairi safari sasa hivi, nipe passport yangu. Huko Marekani nakwenda kusalimia tu ndugu zangu, si safari ya lazima sana.

Yule Counselor akastuka sana, inaonekana ilikuwa kitu cha ajabu sana kupata Mtanzania anayeweza kuji assert hivyo.

Hapo hapo yule Counselor akaanza kumuomba msamaha yule dada yangu mdogo. Akamgongea visa.

Kuanzia siku hiyo, yule dada akawa anakuja na kutoka Marekani anavyotaka. Mpaka sasa hivi kachoka mwenyewe safari za likizo Marekani.

Labda Tanzania tunatakiwa kuji assert zaidi kama alivyofanya huyo dada yangu mdogo, kufanya some sort of reciprocity.

Tatizo ni kwamba, reciprocity works among equals. Sisi kama tunahitaji sana hela za watalii wa Kimarekani, kuwalazimisha wangojee miezi sita kuja kutalii wataghairi na kwenda sehemu nyingine.

Na sisi Tanzania tunaona hatuwezi ku afford kukosa hela za watalii wa Kimarekani.

Inabidi tuwakubalie wachukue visa on arrival Tanzania.
Ubishi dunia hii ni muhimu sana. Ukilegea wanakukula nyama. UK iliwahi kuziletea za kuleta ndege za Nigeria. Wanigeria wakapiga marufuku British Airways kukanyaga kwao. Waingereza wakajirudi wakayamaliza. USA ilipiga marufuku parachichi za Mexico. Wamexico nao wakapiga marufuku mahindi ya USA kuingia Mexico. Ikabidi wakae wayamalize. Sisi hapa hata kumwita balozi na kumpigia kelele sidhani kama tunaweza.
 
Mimi ninafikiri Tanzania ikifanya ubishi hii jeuri itapungua.

Tatizo watu waoga sana.
 
Na hiyo miezi Sita ni kupewa majibu kama umekubaliwa au lah. Tetesi = Marekani wamechukizwa na kitendo cha baadhi ya viongozi wa Africa walio hudhuria kwenye kikao na Put-OUT.
 
Back
Top Bottom