Mkuu 'Missile', huwa una mada fikirishi sana unapoamua kuziibua, ukiondoa ile ya siku nyingi inayohusu dini.
Na uzuri ni kwamba huwa unatumia muda kuzipangilia vizuri mada zako kwa mtiririko unaoeleweka.
Katika hili la Marekani na 'soft power' yake, kwa bahati mbaya umejikita sehemu moja tu ya ushoga', ambayo kwa kweli ni sehemu tu ya mihangaiko anayoikabiri Mmarekani wakati huu.
Swala zima ni 'geopolitical', kuliko swala la ushoga pekee. Huyu amekuwa kinara, mwendeshaji wa dunia yenye mtindo wa 'unipolar', sasa anaona umwamba huo unatishiwa; kwanza kwa Urusi kuvamia Ukraine, jambo ambalo pia ulikuwa ni juhudi za kuongeza umwamba wake ambao umeshtukiwa na kutishwa na huyo aliyekuwa amelengwa kudhoofishwa, Urusi. Matokeo ya haya yote, dunia inaenda kwenye mtindo mwingine tena, kutoka 'Unipolar, kwenda kwenye 'multipolar'.
Sitataka kuandika kirefu hapa lakini ngoja nikupe vidokezo fulani vya kuunga mkono mada yako:
1. Tanzania ni juzi juzi tu, imefanya jambo la kipekee kabisa ambalo hatujawahi kulifanya tokea nchi yetu ipate uhuru.Kwa mara ya kwanza tumejificha vichakani na kutopiga kura kwenye Azimio ndani ya Umoja wa Mataifa; kwa kuogopa kuwaudhi wakubwa; matokeo yake ndiyo hiyo zawadi ya mama Makamu wa Rais kuja kututembelea
2. Umeyasikia waliyoyasema wakubwa katika mkutano wao California, ule wa Merikebu za Australia zinazotazamiwa kuanza kuundwa kwenye nchi hiyo hivi karibuni kwa msaada wa Marekani na Uingereza?
Wanasema hivi: "China represents challenge to "World Order" (Rishi Sunak).
Akaendelea kueleza kuwa "China is a country with fundamentally Different Values to Ours".
Ujue maana ya haya maneno ni nini. Hawa wanapigana juu chini kuhakikisha dunia inakuwa na 'values' zao.
Kwa hiyo sasa wanahaha kila mahala kuhakikisha 'values' hizo zinalindwa, ikiwa ni pamoja na huku kwetu.
3. Kurusi kwenye swala hili la ushoga ulilolipa kipaumbele, na pengine ukiongezea na wazungu kuporwa ardhi yao; hivi uliwahi kujiuliza ni sababu zipi hasa Zimbabwe wanaendelea kuwekewa vikwazo vya kiuchumi hadi leo, hata baada ya Mugabe kuondoka?
Mkuu, 'Missile', haya mambo tuyape uzito unaostahili. Hata kama kuna swala la Ushoga linawasumbua, lakini ni lazima tutambue wazi kuwa ni ukoloni tu unarudi kwa njia tofauti.