Marekani yaanza kutumia 'soft power' yake kuzuia moto wa kukataa ushoga kushika kasi Afrika

Marekani yaanza kutumia 'soft power' yake kuzuia moto wa kukataa ushoga kushika kasi Afrika

Nioneshe ni wapi Papa katetea ushoga.

Screenshot_20230314-212117.png
 
Wala hapo sijaongolea values.
Nimeongelea kubadisha tawala, mageuzi na kuachana kutunushiana misuli na West.

Nimekuambia Urusi haiwezi kuendelea zaidi ya hapo ilipofikia sasa chini ya aina ya udikteta walio nao kwa sasa.

Maendeleo pia yanahitaji order, utaasisi na predictability . Udikteta wa chama huko China unaweza kuweka mazingira hayo. Hiyo ina maana kwamba mtu anayetaka kuwekeza au kufanya biashara China kuna mambo mengi sana anaweza kuyatabiri na kuweka katika mipango yake jinsi ya kudeal na risks zinazoweza kujitokeza, hii ni kwa sababu haitegemwi Xi Jinping ataamka tu na kutoa matamko au maamuzi kiholela. Russia udikteta ni wa mtu mmoja, maono yake na maamuzi yake mwenyewe, siku kichaa chake kikimpanda anaamua lolote. Siloviki iko kupiga muhuri tu maamuzi yake n kutenda yampendezayo kama kurusha wapinzani ghorofani, kuwalisha polonium, kunyang'nya mali zao au kuwafunga kwa kesi za kutengeneza.
Kwa hiyo hapa unasema kwamba China, India, Brazil, na nchi yoyote itakayotaka kuendelea ni lazima ikubali 'values' za Magharibi? Bila hivyo hapatakuwepo na maendeleo? Chumi zao hazitakuwa nzuri?

Hiyo China mbana tayari wanaiona kuwa tishio kwa 'values' zao; imekuwaje kama mchina anaendelea kiuchumi lakini bado ni tishio kwa hizo 'values' zinazomwezesha kuwa tishio?

Kwa nini sasa wanatafuta njia za kumdhibiti?
 
Wiki hii tu Saudi Arabia imetangaza kununua ndege 78 za Boeing 787 kwa dolla billion 37 ambalo ni dili kubwa zaidi kuwahi kufanywa duniani katika biashara ya ndege, wewe endelea tu kuota ndoto za mchana. Hata hiyo China huko inachokitafuta huko Urusi ni gesi kwa bei ya kutupa tu, soko la thamani kubwa zaidi la bidhaa za China ni US na EU.
Katika makosa Marekani na binamu zake watajutia miaka mingi ijayo, ni pamoja na kuzifanya Russia na China kuwa na urafiki wa karibu sana.

Jua halijazama, Iran na Saudia nao wanajadili kumaliza tofauti zao. It's like someone has decoded satan's code.
 
Ukweli ni kwamba mabadiliko haya hayawezi tena kuzuiwa kwa mabavu ya nchi chache zilizojipa unyampala wa kuichunga dunia wapendavyo wao.
 
Kama Martin Luther aliweza kujitoa kwenye Ukatoliki baada ya kutofautiana nao mambo fulani fulani ya kitheologia basi hata hapa TZ iwapo wakatoliki wataona kanisa mama linakwenda kinyume cha Injili ya kweli ya Yesu Kristo linaweza kujitenga.

Japo waanglican wa TZ hawajajitenga, lakini Waanglicana wa TZ na Afrika kiujumla wamekataa katakata kukubaliana na Ajenda ya ushoga inayopigiwa chapuo na kanisa la Anglican la uingereza

Hilo jambo la kujitenga ili kuanzisha kanisa wanaweza wazungu na sio sisi watu weusi, umaskini ni nusu ya ukafiri.
 
I don't condone ushoga ila nguvu ambayo miafrika inatumia kupinga hili swala ni sawa na kuua nzi kwa nyundo.

Viongozi ya Afrika pamoja na udhalimu wao wote imejua ikipinga ushoga tu hadharani miafrika inasahau kila kitu na kuwaunga mkono. Hii ni kutafuta cheap popularity and miafrika fall for it.

Kuna mambo mengi sana ya msingi yanayogusa maisha ya kila mtu ila watu hawatumii nguvu kuyapazia sauti kama ambayo wanapazia sauti ushoga jambo linalogusa wachache mno. Kwa akili hizi Afrika bado sana.
 
Nimekuambia Urusi haiwezi kuendelea zaidi ya hapo ilipofikia sasa chini ya aina ya udikteta walio nao kwa sasa
Utanifanya nikupuuze kwa mipasho kama hii isiyokuwa na mantiki yoyote.
Maendeleo pia yanahitaji order, utaasisi na predictability . Udikteta wa chama huko China unaweza kuweka mazingira hayo. Hiyo ina maana kwamba mtu anayetaka kuwekeza au kufanya biashara China kuna mambo mengi sana anaweza kuyatabiri na kuweka katika mipango yake jinsi ya kudeal na risks zinazoweza kujitokeza, hii ni kwa sababu haitegemwi Xi Jinping ataamka tu na kutoa matamko au maamuzi kiholela
Naona tatizo lako linaanzia hapa, kudhani kwamba bila uwepo wa mitaji toka Magharibi, nchi nyingine haziwezi kuendelea. Huku ndiko kukariri kunakofanya watu wapoteze fahamu.
Unasahau kwamba mfumo huo ndio hao wakubwa wanaoupigania ubaki vilevile ili waendelee kuitawala dunia.
Dunia inajiondoa kwenye ujinga huo.
 
Kusema ukweli

North America wala hawana time na ushoga ni sisi tu ndio tunakuza hiyo agenda.

Watazama. Movie ndio wanapiga kelele na huo ushoga wakati kwa ground katika nchi zao mambo ni tofauti kabisa
 
Wiki hii tu Saudi Arabia imetangaza kununua ndege 78 za Boeing 787 kwa dolla billion 37 ambalo ni dili kubwa zaidi kuwahi kufanywa duniani katika biashara ya ndege, wewe endelea tu kuota ndoto za mchana. Hata hiyo China huko inachokitafuta huko Urusi ni gesi kwa bei ya kutupa tu, soko la thamani kubwa zaidi la bidhaa za China ni US na EU.
Kwa hiyo, kwa kufanya biashara hiyo Saudi Arabia imekuwa nchi inayofuata 'values' za Magaharibi; na kwa maana hiyo Saudi watapata maendeleo zaidi ya Urusi wanaotkataa kuendeshwa na Magharibi?

Hivi mbona ni kama unachanganya mambo kiasi hiki sasa?
 
Mimba za utotoni.

Chanjo ya uviko.

Hili la ushoga I am sure hawatakataa.

Kwa utawala huu linapita.
 
Nimekupuuza.
Kwa hiyo, kwa kufanya biashara hiyo Saudi Arabia imekuwa nchi inayofuata 'values' za Magaharibi; na kwa maana hiyo Saudi watapata maendeleo zaidi ya Urusi wanaotkataa kuendeshwa na Magharibi?

Hivi mbona ni kama unachanganya mambo kiasi hiki sasa?
 
Kusema ukweli

North America wala hawana time na ushoga ni sisi tu ndio tunakuza hiyo agenda.

Watazama. Movie ndio wanapiga kelele na huo ushoga wakati kwa ground katika nchi zao mambo ni tofauti kabisa
Shwari vipi?

Mtafute Pence, Makamu wa Trump usikie alivyoshambuliwa kwa kumsema yule waziri wa Biden shoga anayeshughulikia maswala ya usafirishaji, kuhusu kuchukua kwake likizo ya uzazi kwenda kumlea mtoto.
 
I don't condone ushoga ila nguvu ambayo miafrika inatumia kupinga hili swala ni sawa na kuua nzi kwa nyundo.

Viongozi ya Afrika pamoja na udhalimu wao wote imejua ikipinga ushoga tu hadharani miafrika inasahau kila kitu na kuwaunga mkono. Hii ni kutafuta cheap popularity and miafrika fall for it.

Kuna mambo mengi sana ya msingi yanayogusa maisha ya kila mtu ila watu hawatumii nguvu kuyapazia sauti kama ambayo wanapazia sauti ushoga jambo linalogusa wachache mno. Kwa akili hizi Afrika bado sana.

Pamoja na shida tulizonazo basi tusiongeze shida zingine, hizi tulizonazo zinatosha, kama ushoga ni raha basi wasitulazimishe raha hiyo bali wabaki na raha yao hukohuko kwao, isitoshe ni lini jambo zuri mtu akalazishwa kulichukua??.

Shida tulizonazo zinatutosha hatutaki shida zingine za kishenzi.
 
Hamna mtu anakulazimisha. Hata mashoga bongo kama yule askari zenji hajalazimishwa. Ushoga ni jambo la faragha, US inaweza tangaza all they want mwisho wa siku ni hiari yako mwenyewe.

Tatizo langu ni reaction yenu, kuna changamoto kibao mitaani watu wapo kimya, mnatumia nguvu zote kupinga jambo dogo sana, unaweza kuta mtaani kwenu pote hamna shoga ila mpo hapa kutokwa povu, wakati huo huo hamna maji wala umeme wala barabara mmetulia kama hamuoni vile. Y'all have to reconsider your priorities.
 
Back
Top Bottom