zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 24,661
- 40,890
Tathmini mpya za wataalamu wa masuala ya ulinzi wa Center for Strategic and International studies (CSIS) zinaonyesha kuwa Marekani imetumia zaidi ya asilimia 65 ya makombora yake ya Patriot Interceptor missiles (PC2 na PC3) pamoja na sehemu kubwa ya makombora ya THAAD katika operesheni za hivi karibuni dhidi ya mashambulizi ya Iran.
Hali hii imeifanya CENTCOM, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, kuanza kuchagua ni makombora yapi yatunguliwe na yapi yaachwe ikiwa hayana tishio kubwa kwa miundombinu au maisha ya watu.
Ki-muktadha, vita ilipoanza mwezi Februari Marekani walikua na makombora ya Patriot missiles takribani 2,230 lakini mpaka sasa zimebaki takribani makombora 800 pekee sawa na 35% pekee.
Athari yake ni kwamba vita vinaingia hatua mpya ambapo si kila kombora litatunguliwa kama ilivyokuwa mwanzo. Kadiri akiba ya makombora ya kujihami inavyopungua, ndivyo gharama na hatari ya mashambulizi yanayofanikiwa kuongezeka. Wapinzani wanaweza kuona hili kama fursa ya kuendelea kutumia mbinu ya "kuchosha" mfumo wa ulinzi kwa mashambulizi ya mfululizo. Ikumbukwe tathmini zinaonyesha Iran ana zaidi ya makombora ya long range kama kheibar shekan zaidi ya 3,000 ikimaanisha kama wakitumia yote kwa mkupuo marekani haitokuwa na uwezo wa kuyadungua zaidi ya robo.
Changamoto nyingine ni uzalishaji. Makombora ya Patriot na THAAD si silaha zinazotengenezwa kwa wiki chache. Kila kombora lina teknolojia ya hali ya juu na linaweza kuchukua miezi mingi hadi zaidi ya mwaka kutengenezwa na kukabidhiwa, huku kuongeza uwezo wa viwanda kuchukua miaka kadhaa. Ndiyo maana Marekani tayari imeanza kuwekeza mabilioni ya dola kuongeza uzalishaji wa makombora hayo.
Kwa kifupi, hata kama Marekani bado ina uwezo mkubwa wa kijeshi, vita hivi vinaonyesha somo muhimu: katika vita vya kisasa, si suala la nani ana silaha nyingi tu, bali nani ana uwezo wa kuzizalisha upya kwa kasi kuliko zinavyotumika.
Cc Proved