1. Kuongezeka kwa uharibifu kwenye kambi zao, na kupelekea vifo au majeruhi wengi zaidi maana bila air defence za kutosha makombora yanashuka tu bila upinzani.
2. Gharama za vita kuongezeka. Kumbuka inabidi bajeti ya vita iongezeke, lakini uharibifu wa mali pia unaongeza hasara. Mfano radar za THAAD zipo kama 10 tu dunia nzima ila kwenye hii vita pekee wamepoteza tayari 4!! Kumbuka kutengeneza 1 tu ni karibu USD 1 Bllion (Tsh 2.6 Trillion) kwahiyo zote hizo ni hasara.
3. Kupoteza ushawishi wa kidiplomasia. Ikionekana USA inapigika au inaweza kuishiwa silaha basi inaondoa ile sifa yao ya "invincibility" na kuonekana "kama sisi tu". Na umeshaona Bahrain huko wanaandamana hawataki makambi ya US na hata Saudi, UAE wote wataishia kujisalimisha kwa Iran kwamba anaweza kuwalinda kuliko USA.
4. USA kupoteza maslahi yake maeneo mengine. Mfano imeondoa Air defenses Korea kusini na sasa wanahamisha za Taiwan je huoni China na North Korea zinaweza pata confidence ya kushambulia ikijua marekani ipo uchi kuliko wakati wowote.
5. Iran kujiimarisha zaidi. Kama Iran wanaona mbinu ya makombora imefanya kazi basi tutegemee hii vita kuwa ya kudumu na mpango wao wa nuclear ndio utaongeza kasi zaidi hivyo watakua hatari kuliko kabla ya vita