Marekani yasema hakuna kusitisha vita. Nchi za kiarabu zasema hakuna kuhama. Wapalestina wasema bora kufa ndani ya majumba yao. Safari hii ni tofauti

Marekani yasema hakuna kusitisha vita. Nchi za kiarabu zasema hakuna kuhama. Wapalestina wasema bora kufa ndani ya majumba yao. Safari hii ni tofauti

Raha yake waziri mkuu kapigana vita kwa vitendo alipokua KIJANA.
Sasa ndio wakati wa kila kitu kubadilishwa against the odds ili watu wajue nani mwenye nguvu na akili za kweli.
 
Israel is a terrorist state.
IMG_20231024_083110.jpg
View attachment 2790943
 
Ni mfalme Abdalla mtoto wa king Hussein.Alitayarishwa zamani awe kibaraka daima.Sasa anaanza kuwageuka baada ya ubinadadamu kumrudia.
Huyu ni muhimu sana kwao.Akisema basi ndio itakuwa basi.
Waisrael wanaheshimu sana Jordan baba yeke aliwapa ardhi kubwa Israel.
 
Waisrael wanaheshimu sana Jordan baba yeke aliwapa ardhi kubwa Israel.
Aliwaachia ardhi kizembe sana.Tatizo la mayahudi hawaishi kiu yao na hawana ahadi kabisa.Baada ya kumega ardhi yote hayo wanataka nyengine zaidi.Kuna kipande wamekodishwa walime kwenye bonde la mto Jordana.Wakiambiwa muda umeisha wanaleta maneno na vitisho kwa Jordan.
 
Hayo matumaini tu lkn yy malengo yake yanatimia
Malengo ilikuwa ni kumdanganya Mahmoud Abbas kuwa kuna siku atapewa serikali huku ardhi yote ingekuwa ndio mipaka ya serikali inaliwa pole pole.Upande wa pili ilikuwa ni kuwashughulisha Hamas na utawala wa kpande cha Gaza.Kila wakikaribia kupatana anawagombanisha.Sasa mipango yote hiyo imevurugika mara moja na anatishiwa kutoka kila upande kwa sauti moja.Acha mauaji.
 
Malengo ilikuwa ni kumdanganya Mahmoud Abbas kuwa kuna siku atapewa serikali huku ardhi yote ingekuwa ndio mipaka ya serikali inaliwa pole pole.Upande wa pili ilikuwa ni kuwashughulisha Hamas na utawala wa kpande cha Gaza.Kila wakikaribia kupatana anawagombanisha.Sasa mipango yote hiyo imevurugika mara moja na anatishiwa kutoka kila upande kwa sauti moja.Acha mauaji.
Huo ni Kwa mtazamo wako

Lkn ya jikoni huko Palestine na Israel wanayajua wao sisi kazi yetu ni kuskiliza DW na kuangalia BBC tuone nani mkali wa calculation
 
Mpaka jana (tarehe 23 Oktoba) raisi Joe Biden wa Marekani ameendelea na msimamo wake kwamba hataki mashambulizi ya Israel yasimamishwe huku madhambulizi hayo yakizidi kuongezeka na kuzidi kuuwa watu.

======

'Then we can talk': Biden says no ceasefire in Israel-Hamas war until hostages released

Kwa upande wao nchi za kiarabu kwa sauti moja zimesema hakuna kuhama kwa wapalestina kutoka ardhi zao.Wamekumbusha kuwa tayari kuna maazimio ya kuundwa kwa taifa la wapalestina.Hilo taifa litaundwa na nani na wapi kama wapalestina watahamishwa kutoka ardhi zao.

Arab states say Palestinians must stay on their land as war escalates

Hayo yakitokea wapalestina waliowahi kutiii agizo la kuhama maeneo ya kaskazini ya Gaza ili kwenda kusini wameamua kurudi walikotoka wakitoa matamko kuwa ni bora kufa kuliko dhiki wanazozipata huko walikokwenda.Mashambulizi yamewafuata huko huko na wamejikuta wameishiwa na mahitaji yote.Kwa hali hiyo wameona warudi walikotoka ili kufukua visima vya maji japo yenye chumvi wanavyovikumbuka .

Upande wa jeshi la Israel kumeonekana kuwepo kwa msuguano mkubwa baina ya waziri mkuu,Benjamin Netanyahu na waziri wa ulinzi uliopelekea hapo jana kujitokeza kwa pamoja kukanusha habari hizo.Waziri wa ulinzi,Gallant amehimiza jeshi liingie Gaza kwa haraka kwani vijana wameanza kuchoka kusubiri na hamasa zao zimeanza kupomoroka.Waziri mkuu kwa mbinu zake za kivita anasema kuingia Gaza kutafungua lango jengine la mapigano upande wa kaskazini kutoka kwa Hizbulah.

Israel’s military push for Gaza invasion in apparent rift with Netanyahu


Nawatakufa sana tu,mpaka hamas waishe hapo gaza.
 
Safisha safisha kama ile ya kibiti

sio rahisi kama unavyofikiri wanajichanganya na raia ndo maana israel wameachana na ground bato hujui yupi raia yupi hamas. mwanzo netanyau alisema raia wahame kwasababu hiyoo. ili mkichanganywa msiseme taarifa hamkupata.

kibiti hapo ushirikiano wa raia ulikuwa wa asilimia mia ata mgambo wenye silaa nzuri walitosha kuwapeleka kuzimu.
 
Hao waarabu sio kweli kwamba wanawahurumia sana hao wapalestina ila hofu yao kubwa ni mzigo wa wakimbizi.

Kuna kipindi huko nyuma waliwahi kuwahifadhi hao wakimbizi wa kipalestina na adha waliyopata hawataki kabisa kuipata tena kwani jamii ya wapalestina wana asili ya ukorofi sana kiasi kwamba hawajui kushukuru mnapowapa hifadhi.

Miaka ya nyuma walipewa hifadhi na Jordan na kidogo wampindue aliyekuwa mfalme wa nchi hiyo marehemu Hussein na ndipo alipowafukuza na wakaenda Lebanon ambapo pia wakaingiza hiyo nchi kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1975.

Nchini Misri mwaka 1981 walifanya njama na kumuua aliyekuwa rais wa Misri marehemu Jenerali Anwar Saddat kwa madai kwamba kwanini alisain mkataba wa Camp David na aliyekuwa waziri mkuu wa Israel marehemu Manahem Begin iliyopelekea Israel kuirejeshea Misri jangwa la Sinai waliyokuwa wameteka kwenye vita vya mwaka 1973. Wapalestina ni watu tabu sana.
 
Back
Top Bottom