Marekani yasema hakuna kusitisha vita. Nchi za kiarabu zasema hakuna kuhama. Wapalestina wasema bora kufa ndani ya majumba yao. Safari hii ni tofauti

Marekani yasema hakuna kusitisha vita. Nchi za kiarabu zasema hakuna kuhama. Wapalestina wasema bora kufa ndani ya majumba yao. Safari hii ni tofauti

Mpaka jana (tarehe 23 Oktoba) raisi Joe Biden wa Marekani ameendelea na msimamo wake kwamba hataki mashambulizi ya Israel yasimamishwe huku madhambulizi hayo yakizidi kuongezeka na kuzidi kuuwa watu.

======

'Then we can talk': Biden says no ceasefire in Israel-Hamas war until hostages released

Kwa upande wao nchi za kiarabu kwa sauti moja zimesema hakuna kuhama kwa wapalestina kutoka ardhi zao.Wamekumbusha kuwa tayari kuna maazimio ya kuundwa kwa taifa la wapalestina.Hilo taifa litaundwa na nani na wapi kama wapalestina watahamishwa kutoka ardhi zao.

Arab states say Palestinians must stay on their land as war escalates

Hayo yakitokea wapalestina waliowahi kutiii agizo la kuhama maeneo ya kaskazini ya Gaza ili kwenda kusini wameamua kurudi walikotoka wakitoa matamko kuwa ni bora kufa kuliko dhiki wanazozipata huko walikokwenda.Mashambulizi yamewafuata huko huko na wamejikuta wameishiwa na mahitaji yote.Kwa hali hiyo wameona warudi walikotoka ili kufukua visima vya maji japo yenye chumvi wanavyovikumbuka .

Upande wa jeshi la Israel kumeonekana kuwepo kwa msuguano mkubwa baina ya waziri mkuu,Benjamin Netanyahu na waziri wa ulinzi uliopelekea hapo jana kujitokeza kwa pamoja kukanusha habari hizo.Waziri wa ulinzi,Gallant amehimiza jeshi liingie Gaza kwa haraka kwani vijana wameanza kuchoka kusubiri na hamasa zao zimeanza kupomoroka.Waziri mkuu kwa mbinu zake za kivita anasema kuingia Gaza kutafungua lango jengine la mapigano upande wa kaskazini kutoka kwa Hizbulah.

Israel’s military push for Gaza invasion in apparent rift with Netanyahu

Raia wanyonge wa Palestine ndio wanalipia gharama kubwa za uhai wao kwenye huu mzozo.

Mungu awakumbuke wanyonge hawa....🙏🙏🙏
 
Mtu Muhimu sana ni King wa Jordan kakataa Palestina wasiondoke pamoja na Misri, Saudia haya mataifa Marekani na Israel wanayaogopa sana.
Misri na Jordan hawapo tayari kwa mzigo mpya wa wakimbizi, isitoshe wapo Wapalestina wengi tu huko kwenye hizo nchi.
 
Misri na Jordan hawapo tayari kwa mzigo mpya wa wakimbizi, isitoshe wapo Wapalestina wengi tu huko kwenye hizo nchi.
Naona umekurupuka kujibu ufahamu hoja ni nini, mkutqno wa Arabic juzi fuatlia walichosema Rais wa Misri, Jordan, Saudiq Arabia, Qatar.
 
Saizi lazima wapate suluhisho la kudumu, ila sahizi nimependa umoja wa waarabu, wamegoma kutumika kipuuzi, na hio ndio imefanya mambo yawe magumu kwa USA na Israel
kwan huwa inajulikana mapema , subir mwishon mtatunga story zote
 
Si kila siku kuna watu wanasema ni nchi ya watu wenye akili sana.Wanasahau Allah ndiye mwisho wa akili zote.
mnasahau mapema [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kila kitu na wakati wake kijana hata hao waisrael wako waliteswa sana na hitler na farao hadi mungu alipowaokoa, yeye ndio anajua kitu gani atafanya wakati gani na hana mshirika
Na bado hawakufanya shukrani.Allah akawalani..
 
Back
Top Bottom