STRUGGLE MAN
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 8,633
- 16,586
Etiiii
Marekani ndie mtetezi mkuu wa uislamu Duniani na waislamu.
Waislamu wengi hutamani kwenda Marekani wakapate uhuru wa kuabudu vizuri, hawatamani kwenda Saudi wala Yemen bali Marekani.
Marekani amekua akitetea waislamu wasali na kufanya ibada zao kwa amani.
Marekani amekua akishughulika na magenge ya wahuni ndani ya uislamu, yanayotumia uislamu kufanya uhalifu dhidi ya binadamu wenzao kwa kigezo cha uislamu.
Waislamu wengi mashariki ya kati hutamani kukimbilia ulaya na marekani wakawe huru kufanya ibada zao badala ya huko salipo chini ya vikundi na magenge ya wahuni wanaotumia uislamu kuwaua, kuwakandamiza na kuwanyima uhuru.
Unafikiri Marekani akiamua kukaa kimia si vikundi vya wahuni vitaua waislamu na kuwamaliza huko mashariki ya kati. Angalia ISIS, Taleban, Hezbollah, sijui vikundi gani vinavyoua watu sasa, fikiri waachwe huru waue watu wanavyojisikia kwa uhuru kwa jina la uislamu, kuna mtu atabaki?