Kwahiyo leo chanjo za wazungu haziaminiki tena kama mlivyokuwa mnadai? Maana humu jukwaani kila aliekuwa anajaribu kuhoji usalama wa hizo chanjo alioneka kituko,wengine wakadai kwamba mzungu hawezi kutuletea kitu chenye madhara kwakua kama angetaka kutudhuru angefanya hivyo kupitia chanjo nyingine tunazipokea utotoni.
Vipi leo zimekuwa na kupitiswa mmeanza kuwa selective,au ndo kusema huwa mnatafuta mijadala ya kisiasa tu? Maana kitu kabla haiijafanywa na serikali huwa mnakishupalia kweli ila kikifanywa tu,kunageuka na kuwa kibaya ilimradi mpate cha kupinga tu, aiseeh 😂