Ndo maana nimesema you're taking it too personal! Yaani kwavile kwao ndo kuna maambukizi na vifo vingi zaidi ndo ulitaka wasitoe tahadhali kwa wananchi wao wanaotaka kusafiri nje ya nchi?
All in all, US hawashutumu nchi yoyote kuwa na COVID-19 bali wanachofanya wao ni kutoa updates kwa wananchi wao wanaotarajia kusafiri nje ya US kwamba "nchi xyz, status ipio hivi, na nchi abcd, status ipo vile so, kama mnataka kusafiri, bear that in mind..."! Sasa tatizo lipo wapi hapo?!
Na wanachofanya US kimsingi ndicho kinatakiwa kufanywa na nchi yoyote inayojali wananchi wake, including TZ!
Usisahau, US hawaoni taabu kutuma Special Force kwenda kumuokoa Mmarekani mmoja tu anayeshikiliwa na watekaji nje ya US!!Sasa kwa taifa ambalo lipo tayari kutuma kikosi maalumu kumuokoa mwananchi wao, utashangaa wakitoa tahadhali kama hiyo?!
Na US hawafanyi hivi kwenye issues za COVID-19 peke yake, kwa miaka kadhaa wamekuwa wakitoa similar alerts kwa nchi wanazoamini kuna vitisho mbalimbali kama vile vya kigaidi!! Tena kwa KE hizo alerts hivi sasa wameshazizoea kwa sababu US wamekuwa wakitoa alerts kama hizo dhidi ya KE for years now, and subject matter ikiwa vitisho vya ugaidi!!