Wanaweza kuvimba kwa kutukaanga wananchi kwa kuwa pesa kiduchu watakopata itakuwa inawasaidia kulipana salaries but mfumo wa uchumi lazima ukolapse ,wakichokana huko ndani ndio huwa wanapinduana
Ukweli ni kwamba hawana misuli ya kiuchumi kushindana na mabeberu,imagine wasinunue madini itabakia magendo tu kwenda china nk, transaction zitakuwa magendo,utalii hakuna,bandari itacollapse kuingiza mizigo,bado misaada yoote ya kibajeti ,elimu na afya ambayo mabeberu wanasaidia vitapigwa chini.
Nakumbuka kipindi Cha JK Tzn ndio nchi pekee ya kiafrika ikiongoza kupata pesa nyingi kutoka Marekani kwenye sekta zote ambazo mabeberu wanasaidia Afrika .Baada ya Magu misaada mingi ilipunguzwa sasa kufidia gepu ndio maana amekopa kuliko kawaida.
Wenzie akina Nyerere pamoja na sera zao za kijamaa walijua kula na kipofu na hata aliponea mapinduzi kadhaa kwa msaada wa mabeberu tena kipindi Cha vita baridi na ukombozi ambapo viongozi wenzie walipinduliwa na wengine kuuwawa.
Duniani hapa tunapita hakuna haja ya kiburi kisicho na tija na kujua tu kula na mabeberu.Tena mabeberu ni wabaya Sana wakipata dikteta anayekula nao wananchi hasa wapinzani mtaumia hakuna wa kuwasikiliza unless mjioorganise muitimue serikali nao wanahamia upande wenu maana wao wako after maslahi tu