Kwanza Mama wa mtoto Yesu jina lake sio Maria bali Mariamu:
Luka (Luk) 1:30
Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
Pili Maana ya Ukristo ni Kusikia na kuyatenda maagizo ya Yesu Kristo:
Mathayo 28:18
Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Imani ya Ukristo ni inatokana na kusikia na kulifuata Neno la Kristo peke yake:
Warumi 1017
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Yesu aliagiza hivi:
Yohana (Joh) 14:14
Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
.....................
Sasa kama mtu anayejiita Mkristo na akaonekana akiomba au kufundisha kuomba kwa jina lingine lisilokuwa la Yesu Kristo, huyo ameikiuka imani ya Kristo:
Wagalatia (Gal) 1:8
Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.
Matendo ya Mitume 4:12
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
..........
Ni kwamba hakuna Jina la Maria kwenye Biblia yote:
Labda mtuambie mmelitoa wapi:
Na nani kawaambia tuombe kupitia kwalo: