Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu

Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu

Watu wanadesturi zao, na Imani zao waacheni kama mioyo yao inaridhika Kuna shida gani? Kwani biblia imeandika kila kitu?
Mkileta mada tu mnataka na ambatanisho la biblia, kwani waroma wao si wanavitabu vyao? Mbona ninyi mnayenu wao hawaingaiki na nyie,?
Ila mwisho kabisa, Mungu mwenye huruma na mjuaji wa kila kitu na upendo hayupo na hajawahi kuwepo
😁 Kwahiyo mkuu ndo ukaamua wewe ndo uwe muweza wa yote
 
1745694319420.png


The Kettle calling the pot Black..., Ukifuata logic yako hata wewe unavyoombea watu kwanini unawaombea na wasijiombee..., Why use Proxy.... (Na sababu na wewe unafanya nadhani jipe jibu kwanza kabla haujauliza swali)
 
Sasa kama wana PhD za theology wewe unahoji vitu gani? Uzuri Wakatoliki wenyewe huwa hawahangaiki na nyie yaani wako kimya wanapiga Sala zao bila shida! Maana hata tukianza kuwafafanulia nyie huwa mmeshajiandaa kubishana! Mfano mdogo kwa kupitishia maombi yetu kwa Mama Bikira Maria, Litrugia inatufundisha kwamba ni rahisi kupitisha maombi yako kwa mtu wa karibu na ukasikilizwa. Kumbuka kule kwenye harusi ya Kana ya Galilee Mama Maria aliwaombea divai baada ya kuwa wameishiwa, kwa vile Yesu alikuwa anamheshimu mama yake hapo hapo akawatengenezea divai hivyo na Sisi tunapitisha maombi yetu kwake kwa kufuata mfano wa Harusi ya Kana! Mfano hata majumbani kwetu kuna vitu watoto hawawezi kwenda moja kwa moja kwa baba yao lakini lazima watapitisha maombi yao kwa mama! Sasa hapo shida iko wapi?
Shida iko hapa, mnampitishia maombi aliyekufa? huo mfano wa galilaya mama alikuwepo na Yesu alikuwepo, inawezekanaje mfu akamuombea aliye hai? una uhakika Huyo mama Maria hakutenda dhambi yoyote?
 
Jibu ni rahisi. Hayajibiwi. Yangekuwa yanajibiwa tusingeona watu wakiishiwa pesa. Tusingesikia watu wanaendelea kuteswa na magonjwa. Tusingesikia watu wanakufa kwa njaa. Shida zote hizo Yesu anaweza kuzitatua. Lakini kwakuwa tunamuomba mtu asiyeweza kutuondolea shida hizo, ndio sababu shida zetu haziondoki na furaha zetu haziwi timilifu. Sikiliza Yesu anavyosema:
Yohana 16:24
"...Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu."

Hilo andiko mbona mimi naona liko wazi sana? Tukimuomba Maria, Yesu anahesabu kuwa hatujaomba neno bado, kwa sababu hajatuagiza tufanye hivyo, ndio sababu hatupati. Na ndio maana furaha zetu haziwi timilifu.
Huko Kwa ambao hawaombi kupitia Maria je matatizo hayo yameisha???
 
Huko Kwa ambao hawaombi kupitia Maria je matatizo hayo yameisha???
Hujaelewa point yangu. Lengo la kuomba ni ili tupate yale tunayoyaomba. Kama hatuyapati ni muhimu tujiulize tatizo liko wapi? Kama tunamuomba Maria tupate pesa, tusipopata maana yake kuna uwezekano mkubwa Maria hatusikii.
 
Shida iko hapa, mnampitishia maombi aliyekufa? huo mfano wa galilaya mama alikuwepo na Yesu alikuwepo, inawezekanaje mfu akamuombea aliye hai? una uhakika Huyo mama Maria hakutenda dhambi yoyote?
Hilo jina limekupwaya mkuu! Bora ungeitwa Mabilika Mpondo!
 
Ulisikia wapi kwamba Wakatoliki wanamwomba Bikira Maria wajibu? Hapo ni kwamba wanamwomba awafishie maombi yao kwa mwana wake ambaye kwa sasa hivi yuko naye huko mbinguni. Kwa hiyo inkuw rahisi zaidi mama akisema kuliko sisi wenyewe! Hayo ni maswala ya imani wewe usiyekuwa Mkatoliki huwezi kuyajua hayo!
Kuna watu umeshuhudia wanafunguliwa shida zao kama magonjwa na mapepo kutoka kwa kusali kwa utaratibu huo?
 
Najiuliza maswali haya:

Yesu alisema tukimuomba Mungu kwa Jina lake Yesu tutapewa (Yohana 14:13-14). Kwanini sasa tunamuomba Maria atuombee?

Maria yuko wapi kwa sasa?

Kuna ushahidi gani wa kibiblia kwamba pale Maria alipo anatusikia na kutuombea?

Aliye na majibu ya maswali hayo, anijuze. Ila naomba majibu yaambatane na mstari/aya/kifungu cha Biblia.
Wasiwasi wako upi kwa Mama wa Mungu ? yaani amzae Mungu wako ashindwe kukuombea kweli!!!
 
Wasiwasi wako upi kwa Mama wa Mungu ? yaani amzae Mungu wako ashindwe kukuombea kweli!!!
Yesu alitoa maagizo ya wazi, tuombeje, tumuombe nani na kupitia kwa nani. Natafuta agizo la kuomba Maria atuombee silioni. Kama ni kufuata harusi ya Kana, ile ilikuwa "live" leo hii Maria hatumuoni "live"
 
Yesu alitoa maagizo ya wazi, tuombeje, tumuombe nani na kupitia kwa nani. Natafuta agizo la kuomba Maria atuombee silioni. Kama ni kufuata harusi ya Kana, ile ilikuwa "live" leo hii Maria hatumuoni "live"
Hata Yesu hatumuoni live mkuu, sioni wewe unapata wapi ujasiri wa kuweka mashaka kwa Mama yake Mungu wako?
 
Yesu alitoa maagizo ya wazi, tuombeje, tumuombe nani na kupitia kwa nani. Natafuta agizo la kuomba Maria atuombee silioni. Kama ni kufuata harusi ya Kana, ile ilikuwa "live" leo hii Maria hatumuoni "live"
Wamejitungia tu, hao akina Petro, Yohana, akina Paulo, Barnaba, Timotheo hakuna mahali wanafanya reference kwa Bikra Maria,. Maria atabaki na heshima yake ya kuwa mwanamke aliyebarikiwa kuliko wanawake wote, lakini suala la kuomba kila mtu ajiombee, ingekuwa watakatifu wanatuombea basi tungekomaa na akina Eliya, Muda, Ibrahimu na Henoko ambao tuna uhakika kupitia maandiko wako Mbinguni
 
Nimekuwa mfuasi mzuri wa RC huko nyuma ila sikuwa nashuhudia matokeo ya kufunguliwa kupitia maombi ya Bikra Maria.
Kama unaenda hila imani utafunguliwaje? Tatizo Walokole mnatafuta miujiza ya papo kwa papo ndiyo maana Mwamposa anawaokota!
 
Ndo Yale Yale kwanini usimwombe Mungu moja kwa moja unamwomba mwanae akuombee
Tuliambiwa Kutoka katika kitabu cha Yohana mtakatifu kua Maombi yenu yatajibiwa ikiwa yatapitia kwa mwanae mpenwa Yesu kristo.
Jichanganye upite ya mkato uone kama utatoboa.
 
Back
Top Bottom