Maria Sarungi: Hili la ahadi ya JWTZ kumtii Samia Suluhu sio la kawaida

Kwani kuna ubaya gani mtu kufurahia kifo cha mbaya wako? Hata Tanzania ilifurahia kifo cha Idd Amin!
 
Hayo ni mawazo ya huyo binti Sarungi.
Kwetu sisi watanzania wa kipato cha kawaida tunamuomba mama Samia atuondolee vikwazo kwenye njia zetu za kujitafutia mkate wetu wa kila siku.
Vikwazo vya mkate wa kila siku vililetwa/wekwa na nani?
Mtu au chama?
 
Umenifilisi, Mkuu wa majeshi kujitokeza pale haikuwa kawaida, achilia mbali maneno yake!
 
Kwani kuna ubaya gani mtu kufurahia kifo cha mbaya wako? Hata Tanzania ilifurahia kifo cha Idd Amin!

hakuna ubaya,hata kufanya tendo la ndoa ni haki yako,shida ni pale unapopayuka wakati unashuka mpaka majirani wanasikia.
kwani akishukuru kimoyo moyo anapata hasara gani???
 
Hahahaha nacheka sana jinsi watanzania walivyo wajuaji
 
Usijifanye hamnazo hujui kuwa huyo baba wa mtu ameua na kujeruhi baba za watu wengi?
 
Umeandika kama unajua ulichokiandika kumbe ni maugoro
 
Usijifanye hamnazo hujui kuwa huyo baba wa mtu ameua na kujeruhi baba za watu wengi?

hata ushahidi huna zaidi y kukisia tu.

kwahiyo unahalarisha visasi viendelee,mfano biggie sasa aanze kutafuta wabaya wa baba yake.
 
Wadau tukumbuke HOTUBA ya jana iliyosomwa na CDF, ilikua inawakilisha vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama.

Kwahiyo ile ilikua kauli ya vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na sio Jeshi peke yake. Hakika tupo salama na Raisi wetu yupo salama. Kutokana na Utii wa vyombo vyetu vya Usalama.

Note:
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinategemeana kwenye utendaji kazi kutoka na Katibu, Sheria na taratibu.
 
Baada ya vyama vingi Ccm iliamua ijilinde. Ndio hizi sheria za ajabu huanzia
 
hakuna ubaya,hata kufanya tendo la ndoa ni haki yako,shida ni pale unapopayuka wakati unashuka mpaka majirani wanasikia.
kwani akishukuru kimoyo moyo anapata hasara gani???
Huyo unayemshabikia alikuwa anabwabwaja hadharani wakati akijeruhi wenzake sasa kwa nini wengine wafurahi kimoyo moyo? Wacha watu watoe nyongo zao!
 
Ukitaka kujua ubaguzi wa jinsia tulionao soma uzi huu. Ndiyo maana naona raisi wetu ana kazi ngumu sana kuingoza nchi ambayo tuna ubaguzi wa kijinsia.
 
Inshort, kuna genge halitaki kumtii RAIS MAMA SAMIA SULUHU. CDF na JWTZ hawataki huo upumbavu, wao watatii na atae leta fyoko fyoko cha moto atakiona
Wafikishie ujumbe wote wanaodhani wana uwezo wa kuhodhi madaraka kinyume cha katiba kwamba wasithubutu wala kujaribu. Yeyote atakaye thubutu au kujaribu kumkwamisha Amiri jeshi mkuu hatokuwa na mwisho mwema.
Hivyo niwatoe wasi wasi ndugu watanzania wenzangu, nchi yetu ni salama na itaendelea kuwa salama wakati wote. Tuendelee kuchapa kazi!!!
 
Watanzania tunawaamini sana waleta maneno kwenye mitandao kiasi wao wanakuwa kama dira yetu.

Tafuteni muda muoongee nao macho kwa macho muwafahamu ili iwape nafasi ya kuwachanganua ili mjitoshe uweledi wao, jee heshima wanayo nunua mitandaoni INAWA STAHILI?

Mkifanikiwa njooni na jibu hapa JF ili mtuhabarishe wakojee.

Itatusaidia kujua kama ndio tunauziwa mbuzi kwenye gunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…