Kwa jinsi alivyoongelea namna jeshi lilivyoshirikishwa kwenye miradi ya serikali na hata kuteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali kama ukuu wa mkoa na hususani akaongelea kuhusu ujenzi wa ukuta na ulinzi wa mgodi wa Tanzanite, utaelewa namna jeshi kwa sasa lipo strategically kwenye swala la kuweka jicho kali na hata kujihusisha kwenye kuendesha na kumiliki rasilimali za nchi, labda kwa maslahi ya nchi kijeshi na kiuchumi. Viongozi wa kiraia wanapoongozwa na mihemuko, uchu wa madaraka unaoendeshwa na maslahi binafsi kama ambavyo tumekuwa tunashuhudia namna mabilioni yanavyotumika kununua uongozi kwa baadhi ya makundi ya watu ndo unaona namna jeshi linavyochukua uthibiti na kuendesha mambo muhimu angalau kwa mlango wa nyuma.....