Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,355
- 14,408
Umelazimishwa kupeleka mtoto huko?,Kwamba wewe unataka usafi watoto wafanyiwe?,hii ni ajabu sana,hivi huyo mtoto atakuwa mgeni wa nani?.Je,huku si kuja kuwa na Watu ambao ni useless ktk Taifa letu?!.Wazazi wapumbavu km wewe ni heri wafungiwe jiwe shingoni watupwe baharini.Nimefuatilia kwa muda mrefu ubora wa shule za Marian hasa Marian Girls iliyopo Bagamoyo nikagundua kuwa ubora wao upo kwenye Masomo tu. Kuhusu huduma ya chakula ni duni sana Kulinganisha na Fedha wazazi wanazolipa ni mwendo wa harage mwanzo mwisho, chakula wanachokula hakina tofauti na wanachokula Tabora boys.
Pili ni kuhusu suala la USAFI, kwa kweli Marian girls wanatakiwa kuhakikisha Mazingira ya wanafunzi yanaendana na sifa ya Shule, kiukweli mazingira hayaridhishi hasa mabwenini na kwenye vyoo.
Halafu pamoja na kwamba watoto wanatakiwa kufundishwa usafi lakini isiwe ndio shule imefanya hao watoto kuwa ndio resources za kufanyia kazi, mzazi anapoamua kulipa fedha nyingi kwa ajili ya mtoto mjue pia anategemea kuwa maisha yake ya shuleni yatapata urahisi fulani, hii ya kuwatumia watoto 100% kusafisha vyoo sio sahihi, ni kwanini msiajiri watu kama wanavyofanya Precious blood, Bright future nk.
Kumbe ndio maana watu wanasema Marian haina kitu kikubwa zaidi ya umaarufu tu.
Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app