Marian Schools huduma ya chakula, usafi ni ovyo sana

Marian Schools huduma ya chakula, usafi ni ovyo sana

Mzazi anahoji hela wanazolipa wazazi kulipia HUDUMA ya elimu watu wanaleta chuki na wivu watoto wa wenzao wateseke, kula maharage ugali na kuosha vyoo kutasaidia nini watoto katika karne ya 21 ukiachana na kuwa ni WIZI wa ada za wazazi.
 
Mpumbavu huyo
Nakubali mimi ni mpumbavu kwa mtazamo wako. Lakini hoja yangu muelewe tu kuwa Ingekuwa kusoma kwa mituringa kuna tija nadhani tungewazidi wazungu na waarabu kifikra na Maendeleo. Sikatai mtoto kufundishwa life skills ni muhimu sana lakini tu iwe ni sehemu ya mafunzo na sio kuwafanya wao ndio resources za kufanya hizo kazi. Pia yaani mzazi ulipe milioni 5 - 6 halafu mtoto chakula ni maharage usiku na mchana mwaka mzima.
 
Mzazi anahoji hela wanazolipa wazazi kulipia HUDUMA ya elimu watu wanaleta chuki na wivu watoto wa wenzao wateseke, kula maharage ugali na kuosha vyoo kutasaidia nini watoto katika karne ya 21 ukiachana na kuwa ni WIZI wa ada za wazazi.
Nashukuru sana kwa kunielewa. Tatizo letu bado tuna fikra za zamani kuwa bila kupitia taabu au msoto hutafanikiwa kimaisha . Yaani mtu anaona fahari kuzungumzia maisha yake ya shule yalivyokuwa ya tabu chakula kibaya , kulima kwa sana na hata kulima mashamba ya walimu au kula viboko kwa sana WAO NDIO WANAONA SIFA. Wengine hatutaki watoto wetu wapitia ugumu tuliopitia.
 
Nimefuatilia kwa muda mrefu ubora wa shule za Marian hasa Marian Girls iliyopo Bagamoyo nikagundua kuwa ubora wao upo kwenye Masomo tu. Kuhusu huduma ya chakula ni duni sana Kulinganisha na Fedha wazazi wanazolipa ni mwendo wa harage mwanzo mwisho, chakula wanachokula hakina tofauti na wanachokula Tabora boys.

Pili ni kuhusu suala la USAFI, kwa kweli Marian girls wanatakiwa kuhakikisha Mazingira ya wanafunzi yanaendana na sifa ya Shule, kiukweli mazingira hayaridhishi hasa mabwenini na kwenye vyoo.

Halafu pamoja na kwamba watoto wanatakiwa kufundishwa usafi lakini isiwe ndio shule imefanya hao watoto kuwa ndio resources za kufanyia kazi, mzazi anapoamua kulipa fedha nyingi kwa ajili ya mtoto mjue pia anategemea kuwa maisha yake ya shuleni yatapata urahisi fulani, hii ya kuwatumia watoto 100% kusafisha vyoo sio sahihi, ni kwanini msiajiri watu kama wanavyofanya Precious blood, Bright future nk.

Kumbe ndio maana watu wanasema Marian haina kitu kikubwa zaidi ya umaarufu tu.

Binafsi ubora wa shule naupima kwa;
1. Ufaulu wa wanafunzi
2. Kufundisha watoto kazi za nje (usafi, kufweka, michezo nk)

Kwa ulivyo andika, nimeona hiyo ndio shule bora kabisa ya kupeleka mtoto
Ukweli watoto waliolelewa kama mayai huku makazini wanakuwa very disorganized kwa kuwa wamezoea kufanyiwa kila kitu. Nafikiri kama unakampuni ya kuajiri watoto wako ni sawa uwalee utakavyo ila kama unategemea waaajiriwe, jua hiyo shule ndio chaguo sahihi.
Nyongeza: Waalimu huchukua hatua ya kuambia wanafunzi wasafishe vyoo kutokana na kuwa na matumizi mabaya ya vyoo na uchafu wa bweni. Na ukute baadhi ya watoto wa kike wanatupa zile taulo zao zilizotumia kila pahala mabwenini na huko chooni hivyo kufanya usafi, hufanya waelimishane wenyewe kwa wenyewe.
Ushauri: Ukisha ona watoto wanafaulu vizuri jua tu hayo mambo mengine yapo sawa. Kama wanakula vibaya ungesikia kila siku wapo hospitalani kwa kuumwa (kukosa vitamin & minerals)
 
Mzazi huyu anaweza kuwa na Jambo la msingi ila hakuweza kukiwasilisha vizuri. Ni hivi hizi shule za private ambazo ndizo mara nyingi zinafanya vizuri zina Ada kubwa na sehemu ya Ada inaonesha inaenda kwenye huduma muhimu kama chakula. Matokeo yake wanaopewa kuongoza hizi shule wanakuwa wapigaji na huduma muhimu hazifanyiki kwa ubora hasa chakula. Ukiona hizo quotations na procurements za watoa huduma na bei zao haziendani na wanacho supply mashuleni huko kwa kuwa wakuu wanaoongoza wanakula na watoa huduma. Marian Schools nao imawakumba. Mzazi umesahsu kuongelea tatizo la kunguni na wapuliza dawa za uchwara. Mfano Marian Boys hata uzio hakuna wakati wazazi ukijiunga kila mwaka kuna malipo ya maendeleo. Lakini niwaambie siyo Marian Schools pekee. Ziko shule nyingi Ada ni kubwa na huduma ni mbovu. Wanachofanya ni kukaririsha wanafunzi wafaulu ili watokrr top 10 Ila wakifika Vyuo vikuu ambalo hakuna spoon feeding wanadondoka vibaya mno wanapokutana na vichwa vya St Kayumba tena vikitoka na one za mkiani na Div 2 wanawahenyedha sana hawa Spoon Feeding..
 
Binafsi ubora wa shule naupima kwa;
1. Ufaulu wa wanafunzi
2. Kufundisha watoto kazi za nje (usafi, kufweka, michezo nk)

Kwa ulivyo andika, nimeona hiyo ndio shule bora kabisa ya kupeleka mtoto
Ukweli watoto waliolelewa kama mayai huku makazini wanakuwa very disorganized kwa kuwa wamezoea kufanyiwa kila kitu. Nafikiri kama unakampuni ya kuajiri watoto wako ni sawa uwalee kama mayai ila kama unatemea waaajiriwe, jua hiyo shule ndio chaguo sahihi.
Ushauri: Ukisha ona watoto wanafaulu vizuri jua tu hayo mambo mengine yapo sawa. Kama wanakula vibaya ungesikia kila siku wapo hospilani kwa kuumwa (kukosa vitamin & minerals)
Mzazi huyo anataka mtoto wake
Akiwa arelax asifanye shuguli yoyote
Hawa ndiyo wazazi wa kizazi hiki wanataka kuwalea watoto wao
Ki hamisa mobeto mobeto na Paula

Ova
 
We ndio mjinga, ada na hela iendane na huduma.. tumelipa pesa ndefu mtoto apewe huduma stahiki sikulipa ada mtoto wangu akafanye usafi chooni
Kwa hiyo wewe mtoto wako hata nyumbani hafanyi usafi? Sawa unaweza ukawa umemuwekea watu wa kufanya usafi nyumbani lakini hilo bomu unalolitengeneza utakuja kukumbuka hizi posts when it is too late!!!!
 
Halafu unategemea badae utuletee mtoto kama huyo kwenye system Ili aolewe au aoe watoto wetu,mtoto asiyejua kusafisha choo?Are you serious mkuu?Is your kid even know how to wipe au unataka walimu wafanye kisa umelipa Mamilioni?
 
Hii ni kuharibiana tu kibiashara. Shule zinazofaulisha na kutomlea mtoto kimayai zinazidi kupotea. Shule nyingi kwa sasa zimekazania watoto kufaulu pepa ya NECTA tu huku mambo mengine wakifanyiwa kitu ambacho sio sawa. Hizi shule za kitaifa Mzumbe, Ilboru, Tanga, Tabora, Old Moshi, Kilakala kwangu mimi zitaendelea kuwa bora kuliko hata hizo Marian na Feza.
 
Nimefuatilia kwa muda mrefu ubora wa shule za Marian hasa Marian Girls iliyopo Bagamoyo nikagundua kuwa ubora wao upo kwenye Masomo tu. Kuhusu huduma ya chakula ni duni sana Kulinganisha na Fedha wazazi wanazolipa ni mwendo wa harage mwanzo mwisho, chakula wanachokula hakina tofauti na wanachokula Tabora boys.

Pili ni kuhusu suala la USAFI, kwa kweli Marian girls wanatakiwa kuhakikisha Mazingira ya wanafunzi yanaendana na sifa ya Shule, kiukweli mazingira hayaridhishi hasa mabwenini na kwenye vyoo.

Halafu pamoja na kwamba watoto wanatakiwa kufundishwa usafi lakini isiwe ndio shule imefanya hao watoto kuwa ndio resources za kufanyia kazi, mzazi anapoamua kulipa fedha nyingi kwa ajili ya mtoto mjue pia anategemea kuwa maisha yake ya shuleni yatapata urahisi fulani, hii ya kuwatumia watoto 100% kusafisha vyoo sio sahihi, ni kwanini msiajiri watu kama wanavyofanya Precious blood, Bright future nk.

Kumbe ndio maana watu wanasema Marian haina kitu kikubwa zaidi ya umaarufu tu.
Unapochukia watoto wa shule kufanya usafi unakuwa hauna tofauti ya mzazi anayemtumikisha housegirl na kuwafanya watoto wake kuwa mayai.Ni muhimu watoto wakapewa kazi ndogo ndogo ni kwa faida Yao.Sisi tuliopita shule za kufanya kazi mbali mbali tunaona tofauti yake.Shule za Katoliki Huwa hawalei mayai na ikiwa zinasimamiwa na masista jua neno ORA ET LABORA(Sara na Kazi) litatumika kisawa sawa.
 
Hii ni kuharibiana tu kibiashara. Shule zinazofaulisha na kutomlea mtoto kimayai zinazidi kupotea. Shule nyingi kwa sasa zimekazania watoto kufaulu pepa ya NECTA tu huku mambo mengine wakifanyiwa kitu ambacho sio sawa. Hizi shule za kitaifa Mzumbe, Ilboru, Tanga, Tabora, Old Moshi, Kilakala kwangu mimi zitaendelea kuwa bora kuliko hata hizo Marian na Feza.
Najivunia sana binti yangu kusoma hoyo shule aise

Ova
 
Hii ni kuharibiana tu kibiashara. Shule zinazofaulisha na kutomlea mtoto kimayai zinazidi kupotea. Shule nyingi kwa sasa zimekazania watoto kufaulu pepa ya NECTA tu huku mambo mengine wakifanyiwa kitu ambacho sio sawa. Hizi shule za kitaifa Mzumbe, Ilboru, Tanga, Tabora, Old Moshi, Kilakala kwangu mimi zitaendelea kuwa bora kuliko hata hizo Marian na Feza.
Naunga mkono hoja

Ova
 
Marian Girls iliyopo Bagamoyo nikagundua kuwa ubora wao upo kwenye Masomo tu.
Ulitaka shule ikupatie nini? Alipeleka mtoto shule ili akanye?
Kuhusu huduma ya chakula ni duni sana Kulinganisha na Fedha wazazi wanazolipa ni mwendo wa harage mwanzo mwisho, chakula wanachokula hakina tofauti na wanachokula Tabora boys.
Ulitaka huko shule watoto walishwe Pizza?
Pili ni kuhusu suala la USAFI, kwa kweli Marian girls wanatakiwa kuhakikisha Mazingira ya wanafunzi yanaendana na sifa ya Shule, kiukweli mazingira hayaridhishi hasa mabwenini na kwenye vyoo.
Inabidi kama wazazi mukae na uongozi wa shule kuwasisitiza wawasimamie wanafunzi wao kuhakikisha wanafanya usafi
kuwatumia watoto 100% kusafisha vyoo sio sahihi, ni kwanini msiajiri watu kama wanavyofanya Precious blood, Bright future nk.
Upo comfortable kabisa mtoto wako asifundishwe kusafisha choo anachikitumia?
Kumbe ndio maana watu wanasema Marian haina kitu kikubwa zaidi ya umaarufu tu.
 
Hii ni kuharibiana tu kibiashara. Shule zinazofaulisha na kutomlea mtoto kimayai zinazidi kupotea. Shule nyingi kwa sasa zimekazania watoto kufaulu pepa ya NECTA tu huku mambo mengine wakifanyiwa kitu ambacho sio sawa. Hizi shule za kitaifa Mzumbe, Ilboru, Tanga, Tabora, Old Moshi, Kilakala kwangu mimi zitaendelea kuwa bora kuliko hata hizo Marian na Feza.
Hizo shule ni zinazomfanyia Mwanafunzi kila kitu ni kama viwanda vya kutengeneza Maroboti tu.
 
Back
Top Bottom