Mara nyingi sisi hupenda kuiga au kujilinganisha na hawa wenye demokrasia yao waliyoitengeneza kwa muda mrefu.
Sasa nauliza, hizi mbinu za CCM ya Samia na CHADEMA ya Mbowe inakidhi kweli mlinganisho wowote na wayafanyayo Democratic Party na Republican wa Marekani au Chama cha Labour na Conservative vya Uingereza; au hata vile vilivyoko Ujeruman kwa namna yoyte ilei?
Nionavyo mimi, haya majadiliano na maridhiano ni njia tu za kutafuta ulaji kwa raha toka kila upande, bila kujali maslahi ya nchi na wananchi wake.
Ninaelewa, kuna mambo ambayo huwaleta pamoja hao wakubwa wa dunia, na yote ni yale yanayohusu siasa za nje, hasa wanapopambania maslahi ya nchi zao dhidi ya mataifa wanayoyaona kuwa hatarishi kwa maslahi yao.
Haiwezi hata siku moja ikatokea watu wa Democratic Party wakawaalika wenzao wa Republican kusherehekea shughuli zao za kichama. Hali ni hiyo hiyo na Labor party na Conservatives; na hata kule Canada, Australia, hata Japan, Korea Kusini na kwingineko.
Hii haina maana kwamba hawapendani kama ndugu, au kwamba kuna uhasama kati ya vyama vyao, lakini ndivyo ilivyo ni kama utamaduni kwao.
Sasa sisi tunaiga kitu gani, kama siyo njia tu za kuhalalisha kugawiana mafao ya jasho la wananchi.
Soma: Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini