- Thread starter
- #21
Hakuna mwenye 'conviction' wala 'commitment' juu ya jambo lolote katika hawa wanaojiita wanasiasa tulionao sasa hivi. Mwanzo hadi mwisho wao ni kujinufaisha wao wenyewe.Kinachoendelea ni wanasiasa kuungana kuwakandamiza wananchi.
Tukatae huu usanii unaoendelea maana sisi ndio tunaopoteza zaidi.
Kwani hakuna wa kuzungumzia hali ngumu za wananchi katika mazingira haya ambayo wote ni kitu kimoja.
Ndiyo maana watu kama Mbowe, baada ya kupitia kwenye misukosuko mikubwa sana kama ile aliyoipitia, na baada ya kuona kama watu hawatambui kujitoa kwake, amefikia hatua ya "kwa nini nihangaikie watu wasiokuwa na shukrani!
Hii ndiyo tafsiri ninayoipata kutokana na matendo yake na maamuzi yake baada ya kutoka jela.