Unajichanganya sana mkuu, katika andiko lako hili, ambalo umetumia "kisheria", sijui mara ngapi katika andiko fupi kama hili.
Ni "sheria" ipi iliyohalalisha uchaguzi na matokeo ya uchaguzi uliofanyika?
Lakini ngoja nirudi mwanzo wa andiko lako.
Unaniuliza "kwa nini ninataka tuige wazungu...", kwani ni mambo mangapi tunawaiga hao wazungu, hili kweli linaweza kuwa swali la kumuuliza mtu ajibu?
Kwa kuwa unaonekana kupenda sana mambo ya "sheria", nikuulize wewe, kwa nini CCM isifuate sheria, kama hao Democrats wanavyofuata sheria kwa kutowanyima haki zao wapinzani?
Kwa hiyo, unaposema "...mazingira yetu hayafanani...", maana yake sisi hatupashwi kufuata sheria tunazoiga kutoka kwa hao wazungu? Tumetunga sheria zetu wenyewe hapa, lakini hatuzifuati hizo sheria, sasa unadai ni mazingira yetu ndiyo yanayotufanya tukaidi kuzifuata?
Hata upende ku'spin' vipi kuhusu maamuzi ya CHADEMA wakati huu, haiwezekani kamwe kuondoa msukumo wa manufaa kwao katika kuingizwa kwao kwenye chaka nene hili waliloingizwa na Samia, kwa ufundi mkubwa sana wa Kinana, na pengine Kikwete.