Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

Mara nyingi sisi hupenda kuiga au kujilinganisha na hawa wenye demokrasia yao waliyoitengeneza kwa muda mrefu.

Sasa nauliza, hizi mbinu za CCM ya Samia na CHADEMA ya Mbowe inakidhi kweli mlinganisho wowote na wayafanyayo Democratic Party na Republican wa Marekani au Chama cha Labour na Conservative vya Uingereza; au hata vile vilivyoko Ujeruman kwa namna yoyte ilei?

Nionavyo mimi, haya majadiliano na maridhiano ni njia tu za kutafuta ulaji kwa raha toka kila upande, bila kujali maslahi ya nchi na wananchi wake.

Ninaelewa, kuna mambo ambayo huwaleta pamoja hao wakubwa wa dunia, na yote ni yale yanayohusu siasa za nje, hasa wanapopambania maslahi ya nchi zao dhidi ya mataifa wanayoyaona kuwa hatarishi kwa maslahi yao.

Haiwezi hata siku moja ikatokea watu wa Democratic Party wakawaalika wenzao wa Republican kusherehekea shughuli zao za kichama. Hali ni hiyo hiyo na Labor party na Conservatives; na hata kule Canada, Australia, hata Japan, Korea Kusini na kwingineko.
Hii haina maana kwamba hawapendani kama ndugu, au kwamba kuna uhasama kati ya vyama vyao, lakini ndivyo ilivyo ni kama utamaduni kwao.

Sasa sisi tunaiga kitu gani, kama siyo njia tu za kuhalalisha kugawiana mafao ya jasho la wananchi.
Hata Sudan Kusini wapinzani na watawala wako kwenye maelewano kama haya waBongo acheni fugisu.
 
Nilijuwa toka ulipobababaika kule mwanzo na hoja ya "visheria"kwamba hutakuwa na akili tulivu tena katika kujadili chochote, kwa hiyo nikakudharau tokea hapo.

Endelea kuhangaika mwenyewe upendavyo.
Maswali yote niliyokuuliza umeshindwa kujibu, matokeo yake mara useme "Chadema wamelambishwa asali", baadae ubadilike useme; "tuwape muda", kidogo tena unageuka unasema; "mbona hawajaiga ulaya", baadae tena unageuka unasema; "sio lazima kuiga ulaya kila kitu"

Unajidai mjuaji wakati unaonesha kwa vitendo ulivyojaa huo ubabaifu unaodai ninao, endelea na hao wanaokulea, mimi nimeshakuvua nguo, next time prepare yourself before you drop here.
View attachment 2543347
 
Hata Sudan Kusini wapinzani na watawala wako kwenye maelewano kama haya waBongo acheni fugisu.
LOoooh!

Hata Sudan Kusini iwe mfano kwetu kuiga?

Kweli Tanzania tumeporomoka isivyo kawaida!

Hujasikia huko kila siku wanauana, vita visivyokuwa na mwisho?

Jameni, hebu jaribuni kuwa makini na kuelewa mambo yalivyo kabla ya kuyawasilisha mbele za wengine, maanake matokeo yake ni kujionyesha kiasi cha kutoyajua mambo mnayozungumzia, kama hili na Sudan Kusini.
 
Maswali yote niliyokuuliza umeshindwa kujibu, matokeo yake mara useme "Chadema wamelambishwa asali", baadae ubadilike useme; "tuwape muda", kidogo tena unageuka unasema; "mbona hawajaiga ulaya", baadae tena unageuka unasema; "sio lazima kuiga ulaya kila kitu"

Unajidai mjuaji wakati unaonesha kwa vitendo ulivyojaa huo ubabaifu unaodai ninao, endelea na hao wanaokulea, mimi nimeshakuvua nguo, next time prepare yourself before you drop here.
View attachment 2543347
EeeenHeeee!

Hatimaye umejionyesha utupu mkubwa ulio nao! Sikujua kuwa una utoto unaokusumbua kiasi hiki!

Nimekwisha kudharau.
 
Mara nyingi sisi hupenda kuiga au kujilinganisha na hawa wenye demokrasia yao waliyoitengeneza kwa muda mrefu.

Sasa nauliza, hizi mbinu za CCM ya Samia na CHADEMA ya Mbowe inakidhi kweli mlinganisho wowote na wayafanyayo Democratic Party na Republican wa Marekani au Chama cha Labour na Conservative vya Uingereza; au hata vile vilivyoko Ujeruman kwa namna yoyte ilei?

Nionavyo mimi, haya majadiliano na maridhiano ni njia tu za kutafuta ulaji kwa raha toka kila upande, bila kujali maslahi ya nchi na wananchi wake.

Ninaelewa, kuna mambo ambayo huwaleta pamoja hao wakubwa wa dunia, na yote ni yale yanayohusu siasa za nje, hasa wanapopambania maslahi ya nchi zao dhidi ya mataifa wanayoyaona kuwa hatarishi kwa maslahi yao.

Haiwezi hata siku moja ikatokea watu wa Democratic Party wakawaalika wenzao wa Republican kusherehekea shughuli zao za kichama. Hali ni hiyo hiyo na Labor party na Conservatives; na hata kule Canada, Australia, hata Japan, Korea Kusini na kwingineko.
Hii haina maana kwamba hawapendani kama ndugu, au kwamba kuna uhasama kati ya vyama vyao, lakini ndivyo ilivyo ni kama utamaduni kwao.

Sasa sisi tunaiga kitu gani, kama siyo njia tu za kuhalalisha kugawiana mafao ya jasho la wananchi.
Wewe ulitakaje labda?
 
Back
Top Bottom